Mtikila: Kuna CHADEMA MBILI - 'CHADEMA Chumbani' na 'CHADEMA Sebuleni'

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Mchungaji Christopher MTIKILA azidi kupiga msumali wa MOTO katika JENEZA la Chadema mashumbulizi yake yamuelekea Edwin MTEI

"Amemtuhumu mmoja wa wanzilishi na m/kiti wa kwanza wa chadema Edwin MTEI, akidai kuwa ni muasisi wa dhana ya UKABILA na UKANDA katika chama hicho huku m/kiti wa sasa Freeman MBOWE na Katibu wake SLAA wakidaiwa kuboresha mfumo huo KISASA zaidi kwa kuweka NAKSH NAKSH"

Hata kinacho wafukuza Zitto na wenzake ktk Chadema ni matokeo ya kuota mizizi kwa mfumo wa UKABILA na UKANDA ambao hauruhusu mwanachama yoyote kuhoji mapato na matumizi ndai ya chama"

WATANZANIA waelewe Chadema si chama cha siasa na VIONGOZI wake si wanasiasa wa kweli, kwani hawana MAONO wala MALENGO ya kuwakomboa watanzania

KWA UJUMLA NI GENGE LA WALAJI TU!!!

Ndani ya chadema kuna kundi linaitwa "BIG EIGHT " ambalo linaudwa na wazee wa KICHAGA na kiongozi wao mkuu ni Edwin MTEI akisaidiwa na akina Mariale na Ndessamburo,

Hawa ndio wenye chadema yao ambapo moja ya MAJUKUMU yao ni kulinda maslahi ya kichaga ndani ya chama,Kuna Chadema mbili kuna chadema ya CHUMBANI na Chadema ya SEBULENI"

Source gazeti la Umma Tanzania 4/12/2013


---------------------------------

Ukweli nimekuwa nafurahishwa sana na "role" ya CDM kama chama cha upinzani Tanzania ingawa kwangu mie CDM na CCM ni kama mashetani wawili, hivyo basi between the two evils choose the lesser one. Kwa kuwa nilishavutiwa sana na CDM kwa hivi karibuni, mapungufu yanayojitokeza ndani yake hivi sasa ukweli yananifanya tumbo linikate kiasi fulani. Katika jitihada za kujaribu kupata mawazo ya jinsi ya kuepusha mgogoro zaidi kwa kutumia njia ya kidiplomasia nimefanya jitihada binafsi za kuongea na viongozi wa juu kama saba hivi wa pande zinazovutana bila wao kujua natafuta nini (sikufanikiwa kuongea na Mbowe tu). Katika maongezi yangu ambayo ilikuwa ni kama wa kitafiti nimegundua yafuatayo:

1. Ukweli ugomvi mkubwa ni kati ya Mbowe na Zitto (hawa wamesababisha makundi yanayosigishana).
2. Kundi la Mbowe lingependelea Zitto awe nje ya CDM na sio ajirekebishe.
3. Kundi la Zitto, likiongozwa na Zitto mwenyewe linajiona lina mchango mkubwa sana kuisababisha CDM iwe ilipo na hivyo basi iwapo Zitto atatimuliwa atakuwa kaonewa sana.
4.Kundi la Mbowe limebambika kashfa kuwa Zitto ni Msaliti ili kumsababishia aonwe mbaya na asiyefaa ilihali likijua kuwa Zitto kamwe hawezi kuisaliti CDM kwa mapenzi aliyonayo kwayo.
5. Kundi la Zitto linaona akina Mbowe pamoja na kuminya demokrasia zaidi ndani ya CDM, wanatumia rasilimali za CDM isivyo, na kupakaza kuwa akina Mbowe wananufaika zaidi katika rasilimali za CDM kwa kuwanyima haki viongozi wa chini.
6. N.K

Hayo ni baadhi tu ya matokeo ya utafiti wangu usio rasmi kwa jambo hili uliotokana na hao vigogo saba wa CDM niliowahoji.

Baada ya kupata matokeo hayo niliamua pia kuhoji namna ambavyo mgawanyiko huo unaweza kutatuliwa na nikapata baadhi ya majibu kama hivi:

1. Kundi la Mbowe linadai hamna namna ya kumaliza mgogoro huo sababu Zitto hawezi tena fanya kazi na viongozi wa sasa (haaminiki) na wanaamini hawezi kushuka chini, na dawa ni kumtimua au mwenyewe ajitoe CDM.
2. Kundi la Zitto linadai Zitto asafishwe kwanza asiitwe Msaliti na apewe nafasi zaidi ndani ya CDM, hapo mgogoro utaisha.
3. Pande mbili zikutanishwe na kila upande ukiri makosa yake then wale viapo vya kutoangushana, kashifiana na kusalitiana ili wasonge mbele (hili ni pendekezo la mmoja tu kati ya 7 niliowahoji).

Kwa mtazamo wangu, nikaelewa mgogoro huu umefikia pabaya na nikawa nimependekeza njia ya kuzifanya pande mbili zikae na kukigawa CDM, yaani iwepo CHADEMA ASILI na CHADEMA MABADILIKO. Wengi wa viongozi saba niliowachomekea hili waliona kitu hiki hakiwezekani kata kata. Upande wa Mbowe ndiyo ulikuwa na msisitizo zaidi kuwa CDM haiwezi gawanywa kwani kumtimua Zitto ni kazi rahisi kwao na hilo ndilo litamaliza mgogoro.

Kwa kumalizia, mtazamo wangu umekuwa tofauti na hoja hizi na ninawashauri (pande zote) kuwa waangalie uwezekano wa kukigawa CDM kuwa vyama viwili, wagawane rasilimali (kwa kuwa kila upande umechangia upatikanaji wa rasilimali zilizopo). Kwa sisi wanachama na mashabiki tutaona wenyewe ni upande upi twende kati ya CHADEMA ASILI (Ya Mbowe) na CHADEMA MABADILIKO (Ya Zitto).

Mwisho: Ikitokea inakuwa hivyo wewe MwanaCDM mwenzangu utaenda CDM ipi?
 

Attachments

  • M4C.jpg
    M4C.jpg
    31.8 KB · Views: 2,337
Huyu alipgwa jiwe kule Tarime unakumbuka ? Alikuwa anawaidia CCM hatakaa akasema lolote na hata wewe una akili kama yake au unabisha ?
 
chadema ni chama safi tu, ila ndani ya chadema kunawanyang'anyi na mafisadi.wamekimbia ccm,nccr,tlp wamekuja chadema.

Hawakitakii cdm mema,wao nikujali maslahi yao tu.hawajali maslahi ya taifa na chama.
 
Unahangaika kumjibu mtu aliekuja na stori kutoka kwenye gazeti la kufungia vitumbua? Kwani mchaga sio mtu? Jana tu rafikiangu kafunga ndoa na bint mrembo wa kichaga nailehali yeye nimsukuma alizaliwaga shanga mwalugesha
 
kwa story zile zileee..mbona yeye na chama chake cha DP katibu mkuu ni mkewe? watu wengine bhana

Hivi kuna vyombo vya habari ambavyo bado vina muhoji na kuchukua habari za Mtikila na Kuziandika Magazetini? duh hii Nchi Bwana...Hivi wame muuliza kama zile hela alizokopa kwa Manji alisha zirudisha!
 
Ili kuondoa dhana hii ambayo imetawala kwa vichwa vya watz wengi kuwa CDM ni chama cha ukabila, wazo langu naomba MBOWE & SLAA wawapishe watu wengine au mmojawapo aachie ngazi na huyo atae shika nafac ya aliyejiengua km SLAA au MBOWE asiwe MCHANGA, kidogo watz wanaweza kuwaelewa nini mnafanya
 
Mchungaji Christopher MTIKILA azidi kupiga msumali wa MOTO katika JENEZA la Chadema mashumbulizi yake yamuelekea Edwin MTEI

"Amemtuhumu mmoja wa wanzilishi na m/kiti wa kwanza wa chadema Edwin MTEI, akidai kuwa ni muasisi wa dhana ya UKABILA na UKANDA katika chama hicho huku m/kiti wa sasa Freeman MBOWE na Katibu wake SLAA wakidaiwa kuboresha mfumo huo KISASA zaidi kwa kuweka NAKSH NAKSH"

Hata kinacho wafukuza Zitto na wenzake ktk Chadema ni matokeo ya kuota mizizi kwa mfumo wa UKABILA na UKANDA ambao hauruhusu mwanachama yoyote kuhoji mapato na matumizi ndai ya chama"

WATANZANIA waelewe Chadema si chama cha siasa na VIONGOZI wake si wanasiasa wa kweli, kwani hawana MAONO wala MALENGO ya kuwakomboa watanzania

KWA UJUMLA NI GENGE LA WALAJI TU!!!

Ndani ya chadema kuna kundi linaitwa "BIG EIGHT " ambalo linaudwa na wazee wa KICHAGA na kiongozi wao mkuu ni Edwin MTEI akisaidiwa na akina Mariale na Ndessamburo,

Hawa ndio wenye chadema yao ambapo moja ya MAJUKUMU yao ni kulinda maslahi ya kichaga ndani ya chama,Kuna Chadema mbili kuna chadema ya CHUMBANI na Chadema ya SEBULENI"

Source gazeti la Umma Tanzania 4/12/2013

acha majungu wewe. kaoneshe demokrasia yako kwenye poll hapo juu ili kumpa nguvu huyo msaliti.
kura ziko wazi sahihi, kosa au huna uhakika. mengine majungu tu...
 
Chama chake cha DP ni kama upatu wa yeye na mkewe,

Tangu wasajiliwe hawajawahi kufanya uchaguzi, mtikila ni mwenyekiti wa maisha wa DP,

Mtikila nihuni na ni tapeli wa kimataifa aliyejificha kwenye mgongo wa siasa nchini,
 
Huyu mzee ni kati ya wale wazee wachumia tumbo, kila kukicha na mafaili yake mahakamani, hadi wale makarani wa mahakamani wameshakachoka haka ka dingi. kesi haziishagi miaka nenda rudi.
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom