Mtikila azua balaa, asambaza waraka,yuko chini ya ulinzi wa polisi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MCHUNGAJI Christopher Mtikila anashikliwa katika kituo kikuu cha jeshi la polisi kwa kilichodaiwa kuwa ni anavunjisha amani ya nchi, kwa kusambaza waraka unaomkashifu Rais Kikwete. Mtikili ambaye pia ni MWenyekiti wa chama cha DP alikamatwa nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam majira yan asubuhi na askari

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam alisema Mtikila alikamatwa kwa tuhuma za kusambaza waraka wa uchochezi wa udini dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

Alisema Mtikila anadaiwa kusambaza waraka huo unaomhusisha Rais Kikwete katika mpango wa kuuangamiza Ukristo nchini.

Baadhi ya maneno yanayodaiwa kuandikwa katika waraka huo ni pamoja na ``dunia imeusikia mpango wa hatari wa Kikwete, wa kuingiza katika mfumo wa sheria wa nchi yetu siyo tu mahakama ya kadhi ,bali na 'sheria' za kiislam.’’

Ilidaiwa kuwa mtikila ameandaa kitabu cha kumkashifu Rais na tayari jana mpango huo ulishagundulika na jeshi hilo kwa kusambaza waraka huo.


Hata hivyo jeshi hilo limeahidi waandishi wa habari kuwa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo litawajulisha.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4361138&&Cat=1
 
Back
Top Bottom