Mtikila atupwa rumande! Demokrasia itapatikana?

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,195
590
Ikiwa magazeti yanafungiwa, na wapinzani wanarushwa jela.

Demokrasia itapatikana?


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo imemfutia dhamana Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Mtikila anakabiliwa na tuhuma za kumwita Rais Jakaya Kikwete gaidi.

Mwanasiasa huyo amekiuka masharti ya dhamana yake hivyo amerudishwa rumande.

Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alisema amechukua uamuzi huo baada ya mtuhumiwa kushindwa kufika mahakamani hapo kwa muda muafaka.

Kwa mujibu wa hakimu huyo,ni mara ya pili sasa Mtikila amekuwa akichelewa mahakamani hapo bila kutoa taarifa zozote kwa wadhamini wake kama masharti ya dhamana yanavyoelekeza.

Mtikila amedai mahakamani kuwa alikuwa anaumwa na kuongeza kuwa taarifa za kuumwa kwake alimpatia Wakili wake ambaye naye alidai mwanawe anaumwa na hivyo mahakama kushindwa kupata taarifa zake.

“Ni mara ya pili sasa umekuwa ukirudia kosa hili bila kutoa taarifa zozote kwa wadhamini wako hivyo ninakufutia dhamana utarudi rumande hadi Januari 25, mwaka huu kesi yako itakapoletwa kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya awali,” alihitimisha Hakimu Lema.

Januari 4, mwaka jana, mtuhumiwa hakufika mahakamani hapo ambapo upande wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kutoa kibali cha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kutokana na kutofika kusikiliza kesi inayomkabili bila kutoa taarifa yoyote wala maombi ya kumfanya ashindwe kufika mahakamani.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Victoria Nongwa hakutoa kibali cha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo licha ya kuombwa na upande wa mashitaka.

Januari 6, mwaka jana, Mtikila aliwasilisha barua ya kuiomba msamaha mahakama hiyo, akieleza kuwa alikuwa akimhangaikia ndugu yake ambaye amepooza na kudai kuwa aliwatuma wadhamini wake kutoa taarifa hiyo lakini hawakufanya hivyo.

Inadaiwa kuwa,Oktoba 21, 2007, maeneo ya Ilala katika Shirika la Nyumba (NHC) la Taifa, Mtikila alitoa maneno ya dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali ya Rais.

Katika shitaka la pili, Mtikila anadaiwa kutoa lugha ya uchochezi akidai: “Ahadi zote za Rais Jakaya Kikwete siku zote zinaongozwa na imani yake ya dini tena kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi”

Mtikila alikana mashitaka hayo na alikuwa nje kwa dhamana.

Chanzo: HabariLeo
 
wacha atupwe... demokrasia isivunje sheria za nchi... kutukana wewe, kukaidi mahakama wewe, bado uachwe kisa domokrasia... hell no!!
 
Anatolewa sasa hivi huyo, mimi nilifikiri kuna kesi kubwa, kumbe kuchelewa mahakamani?

I bet muungwana mwenyewe atawapigia simu wamuachie ili asiwe martyred.

Did I hear separation of the executive from the judiciary? Separation my foot, how do you think JF got back online after the dreadful events of the Gestapo?
 
Ikiwa magazeti yanafungiwa, na wapinzani wanarushwa jela. Demokrasia itapatikana?

- Ahsante mkuu, sasa ngoja tuichambue habari tuone kama inafanana na kichwa cha habari!

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo imemfutia dhamana Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Mtikila anakabiliwa na tuhuma za kumwita Rais Jakaya Kikwete gaidi.


Mwanasiasa huyo amekiuka masharti ya dhamana yake hivyo amerudishwa rumande.


- Unaona Mtikila mtuhumiwa amevunja masharti ya dhamana, eti mkuu uliyeleta habari ulitaka sheria imfanye nini? Au kwa sababu yeye ni mwanasiasa sheria iwajibike tofauti na wengine?

- Ndio maana ninasema tunalishana sana sumu humu!

es!



 
Did I hear separation of the executive from the judiciary? Separation my foot, how do you think JF got back online after the dreadful events of the Gestapo?

Mkuu, umeniacha... hebu toa mwanga zaidi mazee
 
Bernard Kerik became the first NYPD commissioner to land in jail Tuesday after a judge revoked his bail for trying to taint the jury pool in his upcoming corruption trial.


Late last night Kerik was taken from White Plains Federal Court to the Westchester County Jail in Valhalla. His lawyers vowed a prompt appeal to try and get him out.A furious Judge Stephen Robinson threw Kerik in the clink after prosecutors said the former top cop and the head of his legal defense fund engaged in a subversive campaign to sway potential jurors.


The judge blasted Kerik for ignoring his prior warnings to bar Anthony Modafferi, the head of the fund, from posting anti-prosecution rants on on the Internet. "Mr. Kerik has a toxic combination of self-minded focus and arrogance that leads him to believe that the ends justify the means, that rules that apply to all don't apply to him in the same way, that rulings of the court are an inconvenience," Robinson said.


The one-time "hero" of 9/11 was led away by U.S. marshals after handing his red tie, religious medals and a ring to his lawyers, standard procedure for all prisoners. Kerik had been out on a $500,000 bond and set to go on trial next week on charges of accepting apartment renovations from a mob-linked contractor seeking a city license.


In Tuesday's unusual and hastily arranged hearing, Assistant U.S. Attorney Perry Carbone revealed that Kerik's supporters were posting on the Web distorted information designed to "try to taint the jury pool."
In June, the judge learned that a nonpracticing lawyer affiliated with Kerik was speaking with witnesses.



- Mkuu mleta habari, tizama hata huko majuu, ukiharibu masharti ya dhamana unaswekwa rumande, hawajali wewe ni nani na rafiki yako ni nani unaswekwa lupango tu kwa hiyo alichofanyiwa Mtikila sio ajabu mkuu!

es!
 
akiwa nje democracy imepatikana si heri ajaribu akiwa ndani labda itapatikana
 
Wanatafuta njia ya kutokea tu hao, kesi yenyewe ya kijinga tu kwani maneno aliyosema yana ubaya gani? Marais wanatukanwa kila siku tena kama huyu mbembeaji anayetafuna pesa ya walipa kodi bila kunawa mikono ni halali yake.

Pesa ngapi za walipa kodi zinapotea kwa kesi ya kijinga kama hii? Kesi ngapi muhimu zinacheleweshwa kwa swala la kutusi. Are we that low? Hii ni sawa na on spot fine ya drink driving.
 
- Mtikila amewekwa Rumande kwa kuvunja masharti ya sheria ya dhamana yake na nothing else, nothing to do na kesi ambayo hajahukumiwa, angekua amehukumiwa then kweli tungeelewa kesi ni ya kijinga jinga, na hasa baada ya kuangaalia sheria inasema nini na kumuita Rais wa jamhuri gaidi.

Es!
 
Wacha akapumzike huko maana wanasiasa wa tanzania walishazoe kumpeleka huko naye utoka. Vitisho havitakuvunja moyo maana si mara ya kwanza, ya pili au tatu kwenda huko.
Hakuna ambaye sheria mfu hizi zikitaka kumpeleka huko hawezi kwenda.
BTW hata nyie wana jf wengi mbona mnatakiwa kuwa mahakani na jela kwa kumsema jmk kila siku?
Yanayofanywa kwa mtikila kwa namna yoyote ni uonevu ule ule ambao hata sisi twaupata tz yote.
Pole mtikila. Nina hakika utatoka tu.
 
Mkuu, umeniacha... hebu toa mwanga zaidi mazee

Rais / Ikulu wanapiga simu mahakamani / polisi kuingilia issues.

Kama hapa watu wa usalama walitaka kuifunga JF kumbe hawakujua hata JK mwenyewe alikuwa anapima joto issues hapahapa, walivyomshika Invisible akawaambia wamwachie.

Sasa na hii issue atawapigia simu wamwachie Mtikila, maana wakimuweka ndani ndio watakuwa wanamfanya kama Ken Saro-Wiwa fulani hivi.

We angalia issue itakavyoenda, atapewa jambajamba ndogondogo ataita mi lawyer yake watamtoa vizuri tu, hawezi kuozea ndani kwa kuchelewa kufika mahakamani, mwenyewe anajua ndiyo maana ana kibri.
 
Wacha akapumzike huko maana wanasiasa wa tanzania walishazoe kumpeleka huko naye utoka. Vitisho havitakuvunja moyo maana si mara ya kwanza, ya pili au tatu kwenda huko.
Hakuna ambaye sheria mfu hizi zikitaka kumpeleka huko hawezi kwenda.
BTW hata nyie wana jf wengi mbona mnatakiwa kuwa mahakani na jela kwa kumsema jmk kila siku?
Yanayofanywa kwa mtikila kwa namna yoyote ni uonevu ule ule ambao hata sisi twaupata tz yote.
Pole mtikila. Nina hakika utatoka tu.

- Hatujamuita Gaidi, believe me siku tukimuita watashuka hata hapa, ndio sheria zetu mfu hizi hizi ambazo kuna wakati Mtikila ameshazitumia kuishinda serikali, na wala sio mara moja!

Respect.


FMEs!
 
Utawala wowote wa kidikteta ndio hutumia njia hizi za kusumbua sumbua wapinzani.Sasa alifika mahakamani kwa kuwa amesema kitu kisichompendeza JK.

Ndio maana nikasema kwa namna hii tutafika?Mpinzani na wananchi waachiwe waseme wanavyotaka, serekali isipoteze nguvu za walipa kodi kwa kunufaisha CCM.

Majuzi gazeti limefungiwa kisa limesema mambo yasiopendezesha JWTZ.Sasa kama serekali haina kazi ya kufanya ni bora hao viongozi wajiuzulu tuu...maana hapa nasikia hadi JF ilitaka kufungiwa.Sasa kama utaanza kudili na website ngapi zipo kwenye Internet, mafisadi wasiweze kuitafuna hii nchi wafanye nini?
 
Kuna mambo mengine ni ya kujitakia tu ni mara ngapi amekuwa akichelewa kwa hii kesi nakuonywa, alijua kabisa akichelewa ataadhibiwa angalia na sababu zake yeye na za wakili wake. Kwa hili sim-support Mtikila wala Mahakama kukaa na ka kesi kasiko na maana muda wote huo sijui toka 2006, hapa sitetei crime ndio maana kuna wakati kezi za kijinga zinatupiliwa mbali kupunguza gharama. Badala ya ku deal na kesi kubwa kubwa walizonazo wanakazania kukimbizana na wanasiasa ambao wengine wanafanya hiyo kwa interest zao.
 
inaudhi sana mijitu inayojiita mipigania haki............halafu inavunja sheria namna hii............

Ikipewa madaraka itakuwaje........si ndio itawaachia mindugu/mirafiki yao kwa kuvunja sheria....damn!
 
mi sijaelewa alimwita JK gaidi kwenye mkutano wa hadhara au wapi?
 
wacha akapumzike huko maana wanasiasa wa tanzania walishazoe kumpeleka huko naye utoka. Vitisho havitakuvunja moyo maana si mara ya kwanza, ya pili au tatu kwenda huko.
hakuna ambaye sheria mfu hizi zikitaka kumpeleka huko hawezi kwenda.
btw hata nyie wana jf wengi mbona mnatakiwa kuwa mahakani na jela kwa kumsema jmk kila siku?
yanayofanywa kwa mtikila kwa namna yoyote ni uonevu ule ule ambao hata sisi twaupata tz yote.
pole mtikila. Nina hakika utatoka tu.

update news ?
 
Ukisoma gazeti la Mwananchi la leo 12.01.2010, utaona kuwa sababu aliyotoa Mtikila ya kutotokea mahakamani kwa wakati huu ni kuwa "alikuwa anamfuatilia daktari aliyemfanyia upasuaji baada ya kung'atwa na nyoka aina ya cobra"

Mashaka yangu ni
1. Kwa nini kila mara sababu zake ni za misingi ya afya? Mwaka jana alidai kuwa anafuatilia tiba ya nduguye aliekuwa amepooza
2. Toka lini mtu aking'atwa na nyoka anafanyiwa upasuaji?
3. Nyoka aina ya cobra wapo katika maeneo ya Dar-es-Salaam?
4. Je ameshapewa nafasi na yeye "apimwe akili"?
 
inaudhi sana mijitu inayojiita mipigania haki............halafu inavunja sheria namna hii............

Ikipewa madaraka itakuwaje........si ndio itawaachia mindugu/mirafiki yao kwa kuvunja sheria....damn!

Ogah,

Huyu alishamaliza kupigania haki pale njaa ilipomzidi!! sasa hivi he is just a radicalised dude!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom