Mtikila Atangaza Kumpandisha Kizimbani Waziri Marmo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila Atangaza Kumpandisha Kizimbani Waziri Marmo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamadari, Feb 16, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mchungaji Mtikila Sunday, February 14, 2010 7:42 PM Akiongea na waandishi wa habari leo hii, Mchungaji Mtikila amemtaka rais Kikwete ajiuzulu ili kulinda heshima yake na pia amesema atampandisha kizimbani waziri Philip Marmo iwapo ataendelea kupinga kuwepo kwa wagombea binafsi kwenye uchaguzi mkuu. Ifuatayo ni hotuba ya mchungaji Mtikila aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya Traventine ya jijini. == == == == TUMEPOKEA hoja zenye hofu na wasiwasi mwingi kutoka kwa wananchi mikoa karibu yote, kutokana na kauli ya hatari aliyoitoa Waziri Marmo, bungeni Dodoma katika hali ya kupinga au kuasi tamko la Mahakama ya rufaa lililobariki amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Mei 5 2006 kwamba taasisi zote zinazohusika na uchaguzi nchini zihakikishe kuwa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 unahusisha wagombea binafsi wa urais, ubunge na udiwani. Kwa vile kauli hiyo ambayo imevunja Katiba ya nchi na inaashiria kuangushwa kwa utawala wa Sheria nchini na kuleta machafuko, tumelazimika kuzuia uhaini walioazimia akina Marmo kwa ufafanuzi na ushauri ufuatao. Kwanza kabisa wananchi wayapuuze matamshi ya ajabu ya Waziri Marmo aliyoyatoa bungeni kwamba mgombea binafsi eti hawezi kupata nafasi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa madai kwamba muda wa maandalizi eti hautoshi! Kwa sababu ya tabia yao ya kutojali Taifa na kuichezea nchi, Marmo pamoja na mkubwa wake aliyemtuma hawana habari kwamba nchi hii si biashara ya mtu binafsi, bali ni Taifa la watu Milioni 41 linaloongozwa na Katiba ambayo ina mihimili mitatu ya utawala yaani bunge, Serikali na Mahakama. Mbali ya utoaji haki katika Taifa, Mahakama ndicho chombo maalum cha kusahihisha makosa ya mihimili ya bunge na Serikali kwa ajili ya kuhakikisha utawala bora katika nchi. Ndio maana katika ulimwengu wote wa tawala za Kidemokrasia ni marufuku kabisa kwa bunge na Serikali kuongelea jambo lolote ambalo lipo mahakamani na wajibu wa mihimili hiyo ni kutekeleza tu maamuzi ya mahakama kama ilivyoelekezwa. Kwahiyo matamshi ya Waziri huyu ni mwiko kabisa! Amekiuka vibaya sana katiba ya nchi kiasi watu wengi wanatafuta kujua kiwango chake cha elimu na busara. Kwa ajili ya kulinda Katiba ya nchi na heshima ya Taifa letu ni lazima sasa Philip Marmo achukuliwe hatua kali za kisheria awe mfano. Uchaguzi ni kipengele cha Katiba ya nchi na mahakama kama chombo maalum cha ulinzi wa Katiba ndicho kilichoamuru kwamba uchaguzi Muu wa mwaka 2010 lazima uhusishe wagombea binafsi wa urais, ubunge na udiwani ambapo kwa mujibu wa Katiba yenyewe watekelezaji wa amri hii ambayo kiuzito ni sawa na sheria ni Serikali na bunge binafsi ni haki ya msingi ya kibinaadam na uraia ambayo imelindwa na Katiba ya nchi, hivyo porojo ya kura ya maoni ni tatizo la kiakili kwa sababu haki ya msingi ni sehemu ya maumbile kama kiunga kingine cha mwili ambacho hatuwezi kukitolea maoni kama tuwe nacho au la! Mahakama Kuu ilitoa haki hii ya ugombea binafsi Mei 5 2006 pamoja na amri ya kutekeleza amri hii kuanzia uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Muda huu ulitosha kabisa kuitekeleza ila rais Kikwete hakutaka kwa ajili ya kulinda maslahi yake binafsi akapotoshwa kwamba angeweza kujihami na athari ya mgombea binafsi kwa kupoteza tu muda kwa ujunja wa rufaa isiyo na kichwa wala miguu! Kwani kwa kutumia uenyekiti wake katika CCM pamoja na Wataalam wa idara ya usalama wa Taifa na mbinu zingine chafu, Kikwete angeweza kujipitisha kwa kipindi cha pili lakini akiinuka mgombea binafsi hata humo humo CCM anaweza kufuatwa na chama chote kutokana na jinsi Kikwete asivyotakiwa, akausindikiza urais kwa macho! Ndio sababu tamko la kihistoria la jopo la waheshimiwa majaji saba wa mahakama ya rufaa limechanganya vibaya akili, kiasi cha Marmo kuropoka yasiyoropokeka. Hatari inalikabili Taifa sasa ni pale rais Kikwete anapothubutu kung'ang'ania kurudi Ikulu kwa nguvu yaani mapinduzi, licha ya kutotakiwa na wananchi na hata ndani ya chama chake baada ya kushindwa kuongoza nchi kwa miaka minne huku akitakiwa kuwajibika kwa ajili ya uporaji wa Matrilioni ya fedha ya nchi kwa kashfa mbalimbali za kifisadi, nyingi zikimgusa yeye binafsi na chama chake kama zitakavyozidi kuwekwa wazi kuanzia sasa. Tunasema Waziri Marmo ameropoka kwa sababu kwa mujibu wa Katika na sheria uchaguzi lazima uwe huru na wa haki na amri ya Mhakama ya rufaa inayolazimisha ugombea binafsi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 inalinda haki na uhuru wa kikatiba wa wananchi. Waziri Marmo ana akili na elimu ya kutosha kufahamu kuwa uchaguzi Mkuu usipokuwa na uhuru na haki ya ugombea binafsi ni kinyume kabisa cha Katiba ya nchi ni uchaguzi batili au haramu! kichaa cha kuchezea mapesa ya nchi kwa uchaguzi batili hakiwezi kuvumiliwa katika taifa la watu wenye akili timamu. Yaani uchaguzi batili hauwezi kufanyika. Tukiacha wahuni wateke urais kwa kuua utawala wa sheria nchini na kudhulumu haki ni lazima Taifa litatumbukia katika machafuko yatakayolimaliza kabisa. Ushauri mzuri kwa rais Kikwete ni kuachia ngazi hata kabla ya uchaguzi kwani atajipatia heshima kubwa. Saa ya ukombozi ni sasa !! http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4074830&&Cat=1
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hii quotation hapo juu ina ukweli ndani yake, CCM kwa sasa wanatumia delay tactics!
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mahakana kuu ina uwezo wa kupeleka uchaguzi mbele kama maagizo yake yaliyotolewa 2006 hajakufanyikwa kazi na serikali - Mtikila yupo sahihi kwa hili - ni njanja tu ya serikali kusogeza mbele suala hili kwa kulitatia rufaa mahakama ya rufani.

  Kama rufaa ya serikali itatupiliwa mbali - kuna uwezekano mkubwa uchaguzi ukasogezwa mbele ili serikali kulishughulikia suala hili la mgombea binafsi - ingawa watu wengi mnaweza kusema hili halitawezekana - linaonekana dogo lakini kumbukeni muhimili huu ndiyo unaotafasiri katiba yetu na nchi.

  Nakupongeza Mchungaji - ingawa bado wananchi hatujakuelewa msimamo wako hasa - upo vuguvugu
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  At least this guy pamoja na mapungufu yake historia inamuhesabu kama mwanamapinduzi anayeweza kudeliver, kuliko wapiga makofi na vigelegele waliojaa CCM ya muungwana.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...