Elections 2010 Mtikila atangaza kugombea Urais kama mgombea binafsi

Regardless ya mambo ya nyuma ya Rostam, or whatever the puke, huyu jamaa anaweza bana!..Ni wewe FMES uliyesema pia kuwa Slaa hawezi lolote pindi akisimamishwa na chama, labda awe kibinafsi!..Maajabu haya!..Why do you neglect these fighters, while u dont seem to give the altenative solution?...Unahusika na mfumo kandamizi uliopo nini?..Network Searching@!#%%!||

You can say that again
 
Mtikila anafaa lakini sio kwa URAIS.

anafaa kwa nini sasa??? aha aha aha!!! unataka awe handsome kama Kikwete, au na upara kama Mkapa? au ashike fimbo kama Nyerere? hakuna wapinzani Tanzania bara naam, ukisema wapo ninamjua mmoja tu kasimama kivyake vyake, hata support ya wananchi mara nyingi anakosa lakini anafanya vitu vya kukumbukwa na kasimamia ukweli, haishii kusema anaenda mbali zaidi akitenda, hawa watu wa aina ya Mtikila we ned them most , lakini tumewatenga , tumekumbatia wajasiriamali wa kisiasa wanao zungumza kisomi zaidi na kwa mvuto zaidi, 'compromisers', 'ndiyo mzee wa mbali', shabash after 10 years 20 years tukievaluate what they have done... NOTHING.... hakuna kitu, zero....
 
Huyu jamaa ni mtata lakini anafanya vitu vya maana sana katika nchi yetu. Ameweza kufanya mambo ambayo historia ya nchi hii haitakaa iliweke pembeni jina lake na hasa katika mapambano ya kuleta demokrasia ya kweli. Legacy yake iko juu sana kuliko baadhi ya viongozi wetu wanaofanya mzaha hata kwenye mambo ya msingi kwa uhai wetu na wajukuu zetu. Mungu atamsaidia.
.. Na huyu jamaa unaweza kukuta akiwa rais akafanya mambo ya maana ingawa wengi tunamuona kama hamnazo...Kuliko haya mambo ya kuchagua sura nzuri sijui mvuto watu wanazidi kudoda tu.
 
anafaa kwa nini sasa??? aha aha aha!!! unataka awe handsome kama Kikwete, au na upara kama Mkapa? au ashike fimbo kama Nyerere? hakuna wapinzani Tanzania bara naam, ukisema wapo ninamjua mmoja tu kasimama kivyake vyake, hata support ya wananchi mara nyingi anakosa lakini anafanya vitu vya kukumbukwa na kasimamia ukweli, haishii kusema anaenda mbali zaidi akitenda, hawa watu wa aina ya Mtikila we ned them most , lakini tumewatenga , tumekumbatia wajasiriamali wa kisiasa wanao zungumza kisomi zaidi na kwa mvuto zaidi, 'compromisers', 'ndiyo mzee wa mbali', shabash after 10 years 20 years tukievaluate what they have done... NOTHING.... hakuna kitu, zero....
...Tuko pamoja mkuu. Point kabisa tatizo pa kugongea senksi sipaoni mwenzenu...
 
Hili la mgombea binafsi limekaaje? Nilidhani ni suala ambalo limekuwa challenged mahakamani! Au Mtikila anataka kuleta ubabe wake tu? Napenda sana changamoto inayotolewa na Mtikila, ila angejaribu kuacha kujitambulisha kwa dini yake kwani taifa hili lina watu wa dini nyingi tofauti.
 
Mtikila hafai kuwa RAISI wala MBUNGE kwa sababu;

  • Nimtu anayeweza kuongea kitu chochote bila hata kukifikiria vizuri nini yatakuwa madhala kwa Taifa.
  • Haamini katika Muungano
  • Ni mtu anayependa kuchanganya uongo na ukweli katika mazungumzo yake ili akubalike ( mfana anadai Nyerere aliwahi kumwita wakiwa marekani na kumshawishi aingie CCM na agombee urais!)
  • Anachanganya sana Siasa na ukristu wake.
  • Ni mtu anayeshambulia viongozi waliopo kuliko kuchambua matatizo yetu na kutuonyesha namna ya kuondokana nayo.
  • Anaweka njaa mbele hivyo anaweza kutusaliti ( aliwezaje kukopa pesa kwa Rostam kama hakuwa karibu naye kwa namna moja au nyingine?)
Kkwa ufupi, pamoja na kuwa mkosoaji mzuri wa serikali, kwa mapungufu hayo ninayoyaona, sidhani kama anaweza kuwa kiongozi mzuri kwa Taifa letu. NI MTIZAMO WANGU TU>
 
Angelipa madeni ya Rostam kwanza, siasa za kuongozwa na njaa haziwezi kulikomboa hili taifa! Ndio maana tunahitaji kuwasiadia vijana kama kina Mnyka.

Respect.

FMEs!

kwani kudaiwa kwake na Rostam kuna uhusiano gani na lengo lake la kugombea urais?? kwani kukopa ni dhambi?sijakuelewa
 
Mtikila hafai kuwa RAISI wala MBUNGE kwa sababu;

  • Nimtu anayeweza kuongea kitu chochote bila hata kukifikiria vizuri nini yatakuwa madhala kwa Taifa.
  • Haamini katika Muungano
  • Ni mtu anayependa kuchanganya uongo na ukweli katika mazungumzo yake ili akubalike ( mfana anadai Nyerere aliwahi kumwita wakiwa marekani na kumshawishi aingie CCM na agombee urais!)
  • Anachanganya sana Siasa na ukristu wake.
  • Ni mtu anayeshambulia viongozi waliopo kuliko kuchambua matatizo yetu na kutuonyesha namna ya kuondokana nayo.
  • Anaweka njaa mbele hivyo anaweza kutusaliti ( aliwezaje kukopa pesa kwa Rostam kama hakuwa karibu naye kwa namna moja au nyingine?)

Kkwa ufupi, pamoja na kuwa mkosoaji mzuri wa serikali, kwa mapungufu hayo ninayoyaona, sidhani kama anaweza kuwa kiongozi mzuri kwa Taifa letu. NI MTIZAMO WANGU TU>

na ubakie kuwa msimamo wako tu
 
Mimi nazani huyu jamaa anaweza akafanya mambo ya maana ingawa wengi tunamuona kama amechanganyikiwa!
Consigliori usimkandie Mtikila tu bila kuangalia upande mwingine wa shilingi
Ngoja nikuambie mambo ya Muhimu kwa taifa aliyo fanya Mtikila
> Kwanza Ndiye aliye changia sana kwenye uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa Kuongea.
>Ndie aliye wafumbua Watanzania wengi kujua uhuru wa Mahakama.
> Mtikila ndie aliyepambana mpaka Takrima Ikafutwa Japo wa Bunge wa CCM na serikali yake walikuwa wameibariki wakidai si Rushwa!
> Mtikila ndiye anayepigania Uhuru wa kuwa na Mgombea Binafsi.
> Hata mambo ya Uzalendo kama Utaifa na vitambulisho vya Taifa amekuwa akisisitizia sana.
Sasa wewe Consigliori mpaka hapo haujaona umuhimu wa huyu mtu.
Mimi si mpambe wake ila nachukizwa kwa kumponda bure bure tu.
 
Mageuzi asante, mimi wala sijamponda, ila nikimtazama kwa jicho la tatu namwona kama nilivyomwelezea kwenye post yangu. Labda kama unaona nimemsingizia kitu, lakini kama hayo niliyoyataja na wewe unayaona, hakika huwezi kumfikiria kuwa kiongozi wa nchi. Mkuu najua yeye ndo aliyeanza kudai kuwepo kwa mgombea binafsi, kufutwa kwa takrima na kadhalika, lakini kwa maoni yangu ana mapungufu katika mambo ya msingi.
 
Watu waelewe kuwa kwa hili la kugombea kama mgombea binafsi anafanya hivyo ili kuona kama Serikali hii itajaribu kutumia vyombo vyake kama Tume ya Uchaguzi kumfanyia mizengwe ili awakabe tena kisheria.

Suala la kushinda au hapana hapa ni irrelevant, kilichopo ni kuwa HAKI YA KUGOMBEA kama mgombea binafsi IPO, HIVYO ISIWEKEWE MIZENGWE.
Mtikila ni Mwanaharakati mahiri. Hapa anataka haki hii ya kugombea binafsi Urais itumike. It's a litmus test so to say.

Mtikila anaweza sana kupigania mambo ya msingi sana. Na anayapigania KISHERIA kwa njia za Mahakama.

Alifanikiwa hadi Mahakama Kuu wakati ule chini ya Jaji Kahwa Rugakingila (baadaye Jaji wa Mahakama ya Rufani) ikatamka kuwa sheria kama za wagomgea binafsi, za kuomba vibali kufanya mikutano ni kinyume na Katiba ya nchi hivyo ni batili.

Big up!
 
Re: Mtikila atangaza kugombea Urais kama mgombea binafsi Mtikila hafai kuwa RAISI wala MBUNGE kwa sababu; Nimtu anayeweza kuongea kitu chochote bila hata kukifikiria vizuri nini yatakuwa madhala kwa Taifa. Haamini katika Muungano Ni mtu anayependa kuchanganya uongo na ukweli katika mazungumzo yake ili akubalike ( mfana anadai Nyerere aliwahi kumwita wakiwa marekani na kumshawishi aingie CCM na agombee urais!) Anachanganya sana Siasa na ukristu wake. Ni mtu anayeshambulia viongozi waliopo kuliko kuchambua matatizo yetu na kutuonyesha namna ya kuondokana nayo. Anaweka njaa mbele hivyo anaweza kutusaliti ( aliwezaje kukopa pesa kwa Rostam kama hakuwa karibu naye kwa namna moja au nyingine?) Kkwa ufupi, pamoja na kuwa mkosoaji mzuri wa serikali, kwa mapungufu hayo ninayoyaona, sidhani kama anaweza kuwa kiongozi mzuri kwa Taifa letu. NI MTIZAMO WANGU TU>

Lakini lazima tutambue mchango wake katika Taifa hili. Ni moja kati ya watu waliotoa mchango mkubwa katika sheria na uongozi kandamizi wa Tanzania kuliko hao wanaokwenda kusinzia bungeni badala ya kutunga sheria. Chukua issue moja tu ya mgombea binafsi ni suala la msingi sana kikatiba kama ungekuwa mjadala bungeni nani angekuwa na point kumzidi? Kuna mbunge aliwahi kwenda na Hoja hiyo binafsi bungeni pamoja na kuwa na nafasi hiyo kwa kanuni za bunge?

Maoni yangu: Anafaa sana kwa Ubunge; Urais hapana.
 
Back
Top Bottom