Mtikila atangaza kugombea Urais kama mgombea binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila atangaza kugombea Urais kama mgombea binafsi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Apr 18, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mchungaji Christopher Mtikila akionesha waandishi wa habari walaka wake ambao amesema atausambaza hadi nje ya nchi.

  Akizungumza nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Slaam jana, Mwenyekiti huyo wa DP Christopher Mtikila ametangaza nia yake kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao kama mgombea binafsi.

  Alisema kuwa katika uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba mwaka huu amejipanga kuchukua fomu ya kugombea urais huku akimtaka Rais Jakaya Kikwete kujiandaa kukabiliana naye.

  Lazima Rais Kikwete ajiandae kwa kuwa mimi haniwezi. Katika siasa mimi nina uwezo, naamini hivyo kwa kuwa nina roho ya Kristo ndani yangu,"alisema Mtikila.

  Juzi Mtikila pamoja na kueleza sababu za kuandika waraka huo, alieleza kuwa kukamatwa kwake kulitokana na viongozi aliowatuhumu kupata presha ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini Mwezi Oktoba mwaka huu.

  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa ni mtata lakini anafanya vitu vya maana sana katika nchi yetu. Ameweza kufanya mambo ambayo historia ya nchi hii haitakaa iliweke pembeni jina lake na hasa katika mapambano ya kuleta demokrasia ya kweli. Legacy yake iko juu sana kuliko baadhi ya viongozi wetu wanaofanya mzaha hata kwenye mambo ya msingi kwa uhai wetu na wajukuu zetu. Mungu atamsaidia.
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pengine akigombea huku akiwa na roho ya Kristo anaweza akashinda kwani Kikwete aliekuwa Chaguo la Kristo (kwa mujibu wa maoni ya viongozi wa dini) ameshindwa kutekeleza maagizo ya Kristo hivyo Kristo atahamishia sapoti yake kwa Mtikila.

  Huyu jamaa anamkandia Kikwete kuwa mdini kwa vile anaamini dini tofauti na anayoamini yeye na sasa anatuletea hayo ya Kristo katika jamii yenye dini tofauti! Ama kweli akili ni nywele ................!
   
 4. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #4
  Apr 18, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mchungaji ukimsikiliza juu juu utaona hana hoja ila jamaa huwa na hoja za msingi, tatizo lake ni moja, unapokuwa kwenye nchi isiyokuwa na dini kama TZ, na wewe ni mwanasiasa ili uwe na support ya kutosha lazima kuweka hisia zako za dini vizuri, usipende kusema mimi naamini........ kuliko Imani ya mwingine. hapo ndipo anapokosea na ndiyo maana hasongi mbele.

  Ila ni mtu mzuri sana, anayeijua siasa ya bongo vizuri sana.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Angelipa madeni ya Rostam kwanza, siasa za kuongozwa na njaa haziwezi kulikomboa hili taifa! Ndio maana tunahitaji kuwasiadia vijana kama kina Mnyka.

  Respect.


  FMEs!
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Regardless ya mambo ya nyuma ya Rostam, or whatever the puke, huyu jamaa anaweza bana!..Ni wewe FMES uliyesema pia kuwa Slaa hawezi lolote pindi akisimamishwa na chama, labda awe kibinafsi!..Maajabu haya!..Why do you neglect these fighters, while u dont seem to give the altenative solution?...Unahusika na mfumo kandamizi uliopo nini?..Network Searching@!#%%!||
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Apr 18, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hahaaaaa PakaJimmy.....tunafikiri sawa.
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mtikila anafaa lakini sio kwa URAIS.
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Duh! sasa nitoe alternative na wakati ninajua kwamba hakuna, Mtikila unasema ndio alternative? Mkuu hoja kwa hoja vipi uki-deal na hoja maana kila ninalolisema huwa ni hoja, vipi wewe unahusika na njaa na Mtikila nini? Acha hizi yaani wote ni lazima tuone kama wewe ama sivyo tunahusika na nonsense? ndio maana siku hizi tunakaa mbali kidogo maana ni yale yale tu hakuna mapya!

  FMEs!
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wewe rafiki vipi unasema kumsaidia Mnyika wakati kwenye post ile ya Mnyika ulisema unakuja Ubungo kumsaidia mgombea mwingine?
  Mbona ueleweki? Niweke sawa kwa hili brother!
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Ungesema hujanielewa badala ya what you said, Mnyika anawakilisha new generation ya vijana tunaoweza kuwaamini na samahani mimi siamini sana siasa za Yanga na Simba, akishinda ninayekuja kumtetea au Mnyika yote kwangu ni sawa yaani vijana cha muhimu ni taifa kwanza, pole sana rafiki!

  Respect.


  FMEs!
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bado sikuelewi. Mwanasiasa makini ni lazima akuogope!
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Vipi ukirudi kwenye hoja ya msingi kwa taifa, maana nowadays sina muda wa kupoteza tena na nonishus kwa taifa!

  Later!

  FMEs!
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  :behindsofa::behindsofa:
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  Apr 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mtikila anafaa kwenye mambo ya Mahakamani, urais ni ndoto kwa jinsi anavyoendesha siasa zake! Kwa nafasi ya urais ni Dkt Slaa tu, hakuna mwingine!
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu nitofautiane na wewe, .......... dr slaa naye anafaa kwa ubunge tu.............. ningekuwa na uwezo ningemteua kuwa mbunge wa maisha.............
   
 17. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Tafadhali fafanua sababu zinazokufanya uwe na maoni kama haya. Kwa nini Slaa hafai urais?
   
 18. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  natamani mtikila aingie bungeni!! Bunge letu litachangamka zaidi, na ndipo itakapokuwa aibu ya mafisadi. Urais aachane nao anapoteza muda!!!
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Pamoja na kukubaliana na wewe kwa hili lakini napenda niweke wazi kuwa mtu yeyote (narudia) mtu yeyote muadilifu anaweza kuwa Rais.
  Urais hauna chuo wala sura ya mtu.
  :becky:
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Moja ya viongozi makini sana na pia huwa hayumbishwi na watu maana anasimamia hoja yake siku zote
   
Loading...