Mtikila atafuta fedha kumfungulia kesi Pinda................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila atafuta fedha kumfungulia kesi Pinda...................

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 5, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Mtikila atafuta fedha kumfungulia kesi Pinda
  Saturday, 04 December 2010 22:36

  Mwandishi Wetu
  MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Cristopher Mtikila amesema anatafuta Sh 10 milioni za kumfungulia kesi ya kupinga ushindi wa ubunge Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wabunge wengine waliopita bila ya kupingwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

  Kutokana na uamuzi huo wa Mtikila baadhi ya mawaziri na wabunge kadhaa wano watapandishwa kizimbani kuomba mahakama ibatilishe ushindi wao.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mtikila alisema kuwa ameshindwa kutimia azima yake hiyo kutokana na ukosefu wa fedha za kufungulia hiyo kesi.

  Alisema hivi sasa anahamasisha watu wamchangie fedha hizo ili aweze kufungua kesi hiyo ya kikatiba nchini.

  Lengo la Mtikila ni kufungua kesi kwa kile kinachoeleza ni kushinda kwa njia zisizo sahihi kulingana na vipengele vya katiba ya nchi, hivyo kuitaka mahakama itamke kuwa ushindi wao ni batili.

  Mbali na waziri mkuu, mawaziri watakaokumbana na hali hiyo pamoja na majimbo yao katika mabano ni Profesa Anna Tibaijuka (Mbunge wa Muleba Kusini) ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Magharibi) na William Ngeleja (Sengerema) Waziri wa Nishati na Madini.

  Wengine ni Philip Mulugo (Singwe), Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na William Lukuvi (Ismani), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge).

  Wamo pia Celina Kombani (Ulanga Mashariki), Waziri wa Katiba na Sheria; Gregory Teu (Mpwapwa) ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, pamoja na Ezekiel Maige ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii.

  Wengine ni Spika wa Bunge Anne Makinda (Njombe Kusini), na naibu wake, Job Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa, nao wanapingwa na DP.

  Wabunge wengine waliopita bila ya kupingwa ni Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), January Makamba (Bumbuli); Nimrod Mkono (Musoma (Vijijini); na Deo Filikunjombe (Ludewa).
   
 2. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Nadhani hata mahakama ikitengua ubunge wao,basi tunabidi tuiombe mahakama iwaachie uwaziri wao,ili tuwe na mawaziri wasio wabunge kama kilio cha wengi kilivyo. Nashukuru!
   
 3. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu naye sijui yukoje?????????, mbona anaanika utupu wake!!!!!!!!!!! Watamhonga halafu itakuwa kama Tarime!!!!!!!!!! Tarime alikula pesa za sisiemu halafu akambaulia ngeo ikawa ndiyo mwisho!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  hivi huyu mtikila aliishia wapi katika kumfikisha pinda mahakamani? au kakosa hela......................???????
   
 5. N

  Njingo Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ana vigezo vyote ushahidi wa kutosha buruza mahakamani.kwan kupita bila kupingwa kunakua na namna flan flan babuuu.hata mitume walipingwa sasa waliopita bila kupingwa wote ni zaidi ya mitume?
   
Loading...