Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

Kwa mnaompinga mtikila kujiunga na hii forum mtakuwa mnafanya masoka makubwa

nadhani tunamhitaji humu ndani na la muhimu ni kumtreat with respct na kujibizana naye kwa hoja

Nadhani mnajua kuwa JAMBOFORUMS ilizima internet politics za bwana FREEMAN MBOWEamabaye naona ameamua kuwapa kazi hiyo ma KADA wake wamjibie kila kitu

nashanagaa FREEMAN alianza vizuri tuu lakini along the way akaingia mitini kuwajaoin wanasiasa wenzie wanao ogopa mambo ya INTERNET

mleteni MTIKILA kisha mumlete na LIPUMBA
 
DrWho ur kidding ur self, Mtikila humu haji kwa sababu kubwa moja tu, hamna deal humu. The Guy is after money akija humu na kubisha bure atapata nini.

Wewe subiri likokee jambo huko bongo utamuona front (kishazuia kidogo chake)

All sais and done anatusaidia ktk mengi tu though nae anajisaidia
 
Hapa JF hata aje Malaika bado watu watamtukana tu.

Mtikila anafanya kazi ya maana kwa utumishi wa taifa la Watanzania
kuliko sisi hapa JF.

Hapa tunataka watu wawe whiter than white, hao watu tutawapata wapi?

Hivi sisi tumefanya nini cha maana kwa mama Tanzania mpaka tuwe na
haki hiyo ya kuona kila mtu ni mwizi tu?

Angalau Mtikila amejitahidi kuliko sisi humu ambao hata kutaja majina yetu ya kweli tunaogopa.
 
masatu unakosea ,.

mtikila anajituma tu na ana uchungu na nchi yetu ,wala sio after money kama baadhi wanavoweza fikiri ,i know the guy he is living in a two bed apartment pale shule ya uhuru mchanganyiko ,TBL national housing flats for years na hata majirani zake ukiwaambia analipwa watakataa kabisa...mara nyingi hutembea kwa miguu kwenda mahakamani ..au mara nyingine teksi,analo gari bovu old model mercedes lipo juu ya mawe tangu 1990"s ...
sasa huwezi kunishawishi kuwa mtu anayeishi maisha ya mtanzania wa kawaida kama mtikila analipwa...hata hao mawakili anaoweka wengi hujitolea kwa sababu kwa wakili kusimamia kesi ya mtikila ni sehemu ya kujenga jina ...ndio maana anao mawakili lukuki tena wengi wako tayAri hata bila malipo...kesi zake nyingi zinakuwa na LANDMARK RULING na zinamvuto.

tunafanya makosa makubwa sana watanzania kufikiri kuwa mpinzani maana yake ni kuwa hohehahe na mtu wa kununuliwa ,sikatai kunao kina richard hizza na kabourou wengi ...lakini nadhani we have few of guys who are really in business ,let us identify them and give them full support ,this is non partisan ,all of us need watchmen!!!!!!!
 
Kama Mtikila analipwa kutetea Katiba yetu na anashinda, kwanini basi tuwalipe wanaovunja Katiba yetu na kuwalinda? Kama mtu anatumia kipaji chake na kulipwa pesa tatizo ni nini, Tanzania ni nchi ya kibepari, hapendwi mtu isipokuwa pochi tu! Tukipata kina mtikila kumi watakaoichachafya serikali ni bora kuliko kina nanii ishirini wanaolipwa mabilioni kudhoofisha katiba yetu!!
 
Kama Mtikila analipwa kutetea Katiba yetu na anashinda, kwanini basi tuwalipe wanaovunja Katiba yetu na kuwalinda? Kama mtu anatumia kipaji chake na kulipwa pesa tatizo ni nini, Tanzania ni nchi ya kibepari, hapendwi mtu isipokuwa pochi tu! Tukipata kina mtikila kumi watakaoichachafya serikali ni bora kuliko kina nanii ishirini wanaolipwa mabilioni kudhoofisha katiba yetu!!
You got it right,kwa kuongezea Bora kumlipa mtikila kuliko wabunge wanaokaa kimya na kubebisiti Chama na si nchi.................
 
exactly, watu wanaona ni dhambi ya mauti Mtikila kulipwa kutetea Katiba lakini wanaona ni sawa baadhi ya watu kulipwa kuuza nchi yetu, kulipwa ili wakae kimya kujadili Rada, wanalipwa ili wasifurukute... Mtikila ni mwanasiasa na anapozungumza akilipwa siyo kosa na hasa kama kile anachotetea ni kwa manufaa yetu na ya Tanzania.

Je tangu alipoanza ni kweli amekuwa akilipwa na hakuna kitu anachofanya ambacho kinatoka ndani ya moyo wake? Mtu anayelipwa anafuata upepo, je Mtikila anaweza kulipwa na kukubali kutetea muungano ulivyo sasa? Je anaweza kulipwa ili aunge sheria inayokataza wagombea huru? Je anaweza kulipwa ili kesi ya msingi ijayo aiondoe? Ukijibu hapana, basi Mtikila ni zaidi ya wanasiasa wanaofanya mambo kwa kufuata pesa tu.. he must have some principles!
 
Tena kama analipwa bado anafanya kazi nzuri tuchange na humu tumlipe au mnasemaje?Awe mwakilishi wa wanachama wa JF nje ya mtandao......................in a real life!
 
nimelifikiria wazo hizo hasa kama kuna utaratibu mzuri wa yeye kupokea fedha... nitajaribu kuwasiliana naye tuone ni jinsi gani tunaweza kumsaidia katika kesi ya Kikatiba.
 
Mzee MKJJ
Unajua nilisoma mawazo ya na maneno ya Masatu dhidi ya Mtikila nikaamua kukaa kimya maana nilijua atajibiwa . Masatu ni mgeni na mambo mengi nadhani . Mtikila has done a superb job tena ya nguvu zaidi . Mtikila anahitaji kusaidiwa na kwa uwazi maana yeye ndiye pekee anaweza kuwasaidia Watanzania hadi kuona ukweli na kudai haki . Naomba ongea naye na mweleze kabisa kwamba tuko tayari kujitolea kugawana naye kile kidogo tunachokipata

Baada au hapo naomba Masatu sasa sema ni wapi na lini pia kiasi gani alicho kichukua huyu Mtikila na toka kwa nani na ili iwe nini baada ya kupokea pesa . The guy is a very happy man pamoja na maisha aliyo nayo yeye kaweka Tanzania mbele.

Hapa nimesha waomba mkachukue hata majimbo mapema ili mounyeshe matendo lakini maneno meeeeeeeeeeeeeeeeengi tu halafu mnabeza kazi za Mtikila ?


Mbowe everyone here knows kwamba yuko shule . Kusoma si lele mama sasa anaendelea na kazi zake ana akiwa tayari atakuja hapa lakini kwa mtindo wa chuki hizi nadhani hatafurahi akija hapa na kukosa hoja ila mnamtukakana. Ila najua ni muda hana kwa kwua ana kazi ya kusoma , mambo ya chama . Futa usemi wako wa yeye kuingia mitini bila ya wewe kujua why hajaandika . Anaweza pia asione la kuandika baada ya kutukanwa hapa matusi makubwa na baadhi yetu akawa anasoma tu . Mkiweka heshima kwa viongozi wote bila ya kubagua na mkaleta hoja am sure wengi watakuja hapa .
 
Tatizo moja ninaloogopa hapa ni kuwa tunabakiwa kuwa 'waumbuaji' viongozi..! kiongozi gani kala wapi na akalala na nani? Ni kiongozi gani alisema nini alipokuwa chumbani kwa nani! Tunapojaribu kuzungumza mambo binafsi ya viongozi ni lazima tujiulize mambo hayo yanahusiana vipi na utendaji kazi wa kiongozi huyo. Ni pale tu mambo binafsi ya kiongozi yanapoingiliana na nafasi yake ya kazi ndipo hapo hatuna budi kuhoji na kutaka maelezo k.m suala la shahada feki.

Ila mambo mengi ya kiongozi gani alilala na nani ni kweli yanavutia kusikika lakini sifikiri kuwa ni muhimu kwa uongozi wa Taifa. Hoja ya kuwa wao ni mifano kwa jamii haina msingi kwani anayewaangalia viongozi wa kisiasa kama mfano wa maisha yake yeye mwenye itabidi apelekwe mirembe. Kama wazazi siyo mfano mzuri na ndugu wa karibu siyo mfano mzuri basi viongozi wa kisiasa kujaza nafasi hiyo ni kujaribu kujenga taifa la mazezeta!!
 
Hi all members**
Kwa kweli hata mimi nashauri haka kajamaa kaingie humu.

I really like his confidence especially when comes in the matters of defending the ......though ......
 
Kama tuna watu kama Masatu humu kwa nini tusiwe na watu kama Mtikila?(my sentence is symbolic, meaning that since JF is where we dare talk openly they we should have all sorts of people). Na kila mtu ataheshimiwa kwa hoja zake.

Ninazopongezi nyingi kwa Mtikila lakini kuna mengi vilevile ya kumkosoa ama kumpa changamoto-akifika hapa tutajadiliana.

Kama Masatu alisoma vizuri post ya Mbowe, aliandika bayana katika post yake ya kwanza kwamba hatakuwa mchangiaji wa mara kwa mara ama hata kujibu hoja kwa hoja. Suala si shule tu, ni zaidi ya hapo. Mwenyekiti wa Taifa wa chama na aliyekuwa mgombea urais hawezi kuwa mchangiaji wa JF wa kila wakati hata kama ana muda. Ndio maana ya kujiandaa na u-stateman!

Na mimi binafsi, na hata watu wengi hapa mlishauri asiwe anaandika hapa mara kwa mara ama kujibu kila hoja. Na mimi nilienda hatua moja mbele zaidi kujibu hoja zinazoihusu CHADEMA.

Lakini Mbowe ameanza utamaduni wa kuandika kila wiki ambao pia na wenyewe binafsi sikubaliani nao(ila wengi wameupongeza, kwa hiyo kwa kuwa inasemwa wengi wape na uamuzi ni wake-ni sawa kabisa). Huo ndio uhuru wa fikra.
http://www.chadema.net/makala/mbowe/index.php
Unaweza kuyapata maandiko yake hapa

http://www.chadema.net/makala/mbowe/index.php

Na hizi makala zinaweza kuwekwa kwenye ile Thread ya Tafakuri ya Mbowe aliyoianzisha Eric Ongara siku za nyuma tukazijadili maana hapa tunapaswa kuendelea na mjadala wa Mtikila kualikwa JF

JJ
 
Mnyika the issue hapa ni Mtikila kuingia ama kutoingia ktk forum hii, zaidi hapo kama utakuwa umesoma vizuri posting yangu ya awali nilisema Mtikila hawezi kuja humo (sio kama anakatazwa) bali humu hamna deal na yeye ni mtu wa ma deal hawezi kuja kupoteza muda wake.

Ama kuhusu Mbowe tunashukuru Mh tuko nae na tunafahamu uzito wa majukumu yake ya ki shule na kichama nk. Its up 2 him akitaka achangie kila siku, weekly , monthly or even yearly who cares?

Lunyungu unadai mimi ni mgeni wa mambo, ni mambo gani hayo?

Narudia kusema Mtikila ni after money mnaosema anaishi maisha ya kawaida karagabaho muulizeni ile nyumba yake ilitaka kuchukuliwa na benki kutokana na deni ilikuwaje wahindi ndio waliomlipia? Mtikila ni tapeli tu tena tapeli wa kutupwa.
 
CCM walipo ona kwamnba Upinzani na Mtikila ni threat walianza maneno kama

Amani na utulivu ni CCM, CCM ina jeshi na Polisi,CCM ina viongozi imara , Wapinzani n waroho wa madaraka , Mtikila hana kitu ni mropokaji tu,Wapinzani watamwaga damu kama Rwanda na Burundi na Mengi kuonyesha kweney TV yake .

Lakini kila kukicha CCM ndiyo vyanzo vya vurugu, kejeli , wizi , uropokaji , Uongo, kuanzia Bungeni hadi baraza la mawaziri watu wamedanganya kuhusu Eliumu , Rushwa nk .

Masatu kwa kazi ya Mtikila anayo fanya ukisema yote sawa . Mhindi anaweza kuwa kalipa kwa msaada ama kama rafiki . Ukianza haya CCM imeoza na tutayaweka hapa mengi utashangaa. Ndiyo maana nasema mawazo ya aina hii ya Ki CCM hapa hayana maana . Je Mtikila akitokea kaja hapa na kujibu utasemaje ? Maana unasema hana deal hapa na sisi tunajua ana deal na tanzania na haki za watanzania wazi wazi na kule kwenye kila aina ya uonevu. Je akija utasemaje ?Mambo wenye deal akiwemo Rais anaogopa hata kuhojiwa na Mzee MKJJ ? Wewe umelifanyia niji Taifa ? Mtikila ana makesi namadeni kwa kusimamia haki ya kila Mtanzania akiwemo JK anayepinda haki zile wewe unasemaje ?

Kulipiwa nyumba ? Utapeli upi wa Mtikila unao usemea ? Si utueleze hapa tujue kama umesema ni tapeli means ana kesi za aina hii Mahakamani na kwingineko .Hivi wewe unaweza kumjua Mtikla zaid ya CCM na serikali ambayo hadi sasa hawajasema lolote anawasumbua tu ? Tulisikia maneno kama yako juu ay Mrema kwamba ni mwizi mkubwa aliwaita watu Moshi kuchukua chake tukangoja ushahidi wa system na CCM hadi sasa Mrema anakufa Kisiasa hana kashfa ya wizi ama swindling .

Mtikila ni shujaa.
 
Kwa kweli anayofanya behind the scene mimi siyajui na sitaki niyajue kwasasa ,Lakini yale ambayo ameyafanya kwa kusimamia kauli zake na kutetea Haki kwa gharama yeyote na kwa mujibu wa sheria hilo kwa kweli anastaili sifa na Umma wa Tanzania utamkumbuka kwa hili.
 
Hayo ya sirini hata yeye Masatu hawezi kuleta ushahidi ni mzushi tu huyu . Lakini ni sawa pia Masatu ana haki ya kutompenda lakini si kuleta uongo na uchochezi , na fitina za ajabu . Kama ana ushahidi wa Usanii ama utapeli weka hapa tujadili . Maana daina tunajadili hapa kila kitu kwa uwazi .
 
Hayo ya sirini hata yeye Masatu hawezi kuleta ushahidi ni mzushi tu huyu . Lakini ni sawa pia Masatu ana haki ya kutompenda lakini si kuleta uongo na uchochezi , na fitina za ajabu . Kama ana ushahidi wa Usanii ama utapeli weka hapa tujadili . Maana daina tunajadili hapa kila kitu kwa uwazi .

haki ya kutompenda ni yake wala sipingi hilo, Lakini ninapoanisha haki ya kutompenda na sababu za kutompenda kwake ambazo amezitoa hadi hivi sasa naona Hakumtendea haki Mtikila.Hata mimi sikusema ninampenda au simpendi laah, bali nimesema kwa kile ambacho ameshafanya hadi hivi sasa ukilinganisha na tulio wengi humu na nje ya humu au Karibu wote humu na nje ya humu,kwa kweli anastahili sifa.
 
....Kama Masatu alisoma vizuri post ya Mbowe, aliandika bayana katika post yake ya kwanza kwamba hatakuwa mchangiaji wa mara kwa mara ama hata kujibu hoja kwa hoja. Suala si shule tu, ni zaidi ya hapo. Mwenyekiti wa Taifa wa chama na aliyekuwa mgombea urais hawezi kuwa mchangiaji wa JF wa kila wakati hata kama ana muda. Ndio maana ya kujiandaa na u-stateman!.....

JJ

JJ, sijui baadhi yetu tuwe offended na sentensi hiyo ama vipi. Hivi kuchangia sana humu JF inamfanya mtu awe un-statesman?
 
Back
Top Bottom