Mtikila ashinda kesi ya 'ugombea huru' Mahakama ya Haki za Binadamu Africa

Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
9,539
12,654
Arusha. Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

Katika hukumu iliyosomwa leo jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.

Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa.
SOURCE:GAZETI LA MWANANCHI ONLINE​

nadhani mtikila ndiye mwanasiasa wa upinzani anaevutia zaidi, yeye ana utaatibu sahihi tofauti wa mapambano . ili serekali yetu ionyeshe nayo ustaarabu ni vema ikatekeleza huo uamuzi au ikakata rufaa kama nafasi ipo.
kwa ujumla utaratibu sahihi wa kuendesha mambo unatakiwa ufuate sheria ,kinyume chake serekali na wapinzani wakidharau sheria ndipo inapozuka fujo na maafa kutokea.
mimi ni mfuasi wa utaratibu anaotumia mtikila ktk kudai kile anachodhani kua ni haki..... naomba serekali ijali na kuheshimu sana huu utaratibu.
 
Pumzi zake ni ndogo kwa siasa ya nchii naona atatuvurugia sana, Lingine ameegemea kiubaguzi.. Huo ni mtazamo wangu!!
 
Kama kuna mwanasiasa mzalendo wa kweli katika nchi hii, Mtikila ni number ONE!
Hakika mapambano ambayo Mtikila amekuwa akiendesha dhidi ya serikali sikivu ya CCM ni ya kisayansi na ya kupigiwa mfano! Na mara zote huibuka kidedea!
 
Napenda the way jamaa anavyopigania haki ...japo kuwa huwa inacheleweshwa lakini mwisho wa siku anaipuka kidedea bila kumwaga damu

Ndugu
 
Arusha. Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

Katika hukumu iliyosomwa leo jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.

Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa.
SOURCE:GAZETI LA MWANANCHI ONLINE​

Is the judgement binding to Tanzania govt. or just persuasive!
 
Hakika mapambano ambayo Mtikila amekuwa akiendesha dhidi ya serikali sikivu ya CCM ni ya kisayansi na ya kupigiwa mfano! Na mara zote huibuka kidedea!

Halafu kinachoendelea? Je akishinda huwa yanafanyiwa kazi na Serikali ya Magamba? Tueleze ni mangapi aliodai kisayansi yakatekelezwa?

Akumbuke alivyotubu baada kukiri kuhongwa na CCm ili avuruge uchaguzi wa Tarime. Adhabu iliyompata hataisahau, wakurya walipolibaini hilo walimpopoa kwa mawe jukwaani naye akasema hiyo ni adhabu toka kwa Mungu kwa kukubali kuhongwa. Huyu haaminiki kwani ananunulika kwa shekeli kidogo tu.
 
Hoja ya msingi hapa ni kuwa Mtikila ana uwezo wa kujenga hoja alizozifanyia utafiti wa kitaalam na kuibuka kidedea mahakamani! Suala la serikali yako ya CCM kutotekeleza hukumu za mahakama ni udhaifu na ukosefu wa uadilifu wa kutotii sheria ambazo serikali yenyewe imezitunga au kuziridhia!

Sasa hapa nakushangaa kwa kuchanganya mada; yeye kuchukua hongo na kuibuka kidedea mahakamani, wapi na wapi?!
 
Back
Top Bottom