Mtikila ampa siku 7 Ridhiwan aende mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila ampa siku 7 Ridhiwan aende mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, May 7, 2011.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mambo ndo yamewiva,sinema ndo imekaribia kuanza kaa tayari.

  Mtikila amgeuzia kibao Ridhiwan

  na Janet Josiah


  MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amemtaka mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, kwenda mahakamani ndani ya siku saba alizosema vinginevyo atakwenda yeye kushtaki kutokana na utajiri alionao kwani ni kosa la jinai.


  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mchungaji Mtikila alisema kwa taratibu za kisheria Ridhiwan anapaswa kuwapa kwanza ‘Demand Note Letter'( barua ya kuwataka wamwombe radhi au kufuta kauli zao) yeye na Dk. Willibrod Slaa.


  "Ikiwa Ridhiwan hatafanya hivyo nitajipanga kwenda mahakamani kuwaeleza Watanzania namna mtoto huyo alivyo ni bilionea kupindukia kwa kumiliki mali nyingi zikiwemo fedha za Watanzania ambazo ni mabilioni katika akaunti zake, kampuni ya malori 150 na ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha," alisema Mtikila.


  Kwa mujibu wa Mtikila, hawezi kuthibitisha kwa vielelezo aliyoyasema wakati alipokutana na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusu utajiri wa mtoto huyo wa Rais kama hatapelekewa barua hiyo.


  "Yawezekana Ridhiwan anazungumza maneno asiyoyafahamu kisheria na yeye tunasikia ni mwanasheria, kama unamtaka mtu akuombe radhi na kama akishindwa utampeleka mahakamani…maneno hayo kisheria huenda na demand note letter, sasa yeye hajatufikishia je tujipeleke? Alihoji Mchungaji Mtikila.


  Alieleza kuwa kama kweli Ridhiwan ni mwanasheria na anazifahamu sheria, siku ile aliyozungumza na waandishi wa habari angekuwa na barua hizo mkononi tayari kwa kuwapelekea na kusubiri matokeo yake.


  "Sasa naamini kwamba ni kweli Ridhiwan hajui sheria na kama angezifahamu, ningeshapata barua yangu mapema kwa kuwa anayafahamu makao makuu ya DP pale Ilala Msikitini na kama hazifahamu ofisi hizo angeniletea nyumbani kwangu Mikocheni B tuko jirani."


  Juzi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, naye alimtaka Ridhiwan kwenda mahakamani haraka kwa kuwa yaliyozungumzwa na kinywa chake yana ukweli.


  Baada ya tamko hilo la Dk. Slaa siku chache baadaye Ridhiwan alizungumza na waandishi wa habari na kutoa siku saba kwa Dk. Slaa na Mtikila akiwataka kukanusha tuhuma walizomtupia au kuthibitisha kwa vielelezo, vinginevyo angewaburuza mahakamani kwa kumchafua yeye na familia yake.


  Mwanzoni mwa wiki hii Ridhiwan aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona akiendesha magari ya bei ghali na wazipuuze kauli zinazotolewa na wanasiasa hao wa upinzani kwamba ni za uongo.


  Ridhiwan alikaririwa na vyombo vya habri akisema, "Hapa mjini jamani tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake."


  Alisema yeye si bilionea kama wanavyodai wanasiasa hao, na kutaja mali zake kuwa ni shamba la ekari 1.5 lililoko Bagamoyo, gari aina ya Toyota Cami na akaunti katika benki za Stanbic na NBC na CRDB.

  Source: Tanzania Daima online
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Teh tih teh....this is really funny to me.
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu sinema ndo imeanza nunua popcorn kaa tayari usisahau Coke ya Baridiiiiiiiiiiii
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Haya Mkuu sijui Sterling atakuwa nani katika sinema hii na title yake sijui itakuwa ni ipi.
   
 5. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Zikiwa zimepita siku chache Tangia mtoto wa rais JK kuwaambia waandishi wahabari kuwa anawataka Dr Slaa na Mtikila kukanusha habari za kuwa yeye ni bilionea la sivyo anawaburuza mahakamani. wanasiasa hao nguli wamemwomba mtoto huyu wa raisi awahi mahakamani kwani wao wanaushahidi.

  Naye Mtikila amekwenda mbali zaidi kwa kumtahadharisha Rizone kuwa asipokwenda yeye mahakamni basi itamlazimu Mtikila kumburuza Rizone mahakamani.

  Watanzania wanashauku kubwa sana ya kushuhudia kesi hii, haswa katika kipindi hiki ambapo baadhi ya viongozi na familia zao kutumia vibaya madaraka yao na kunufaisha familia zao, marafiki au ndugu zao.

  Siasa za ujamaa zilizaa unafiki mkubwa na ndio unaotumika mpaka leo na wahujumu uchumi kuficha mali kwa majina ya jamaa au majina yasiyofahamika. Ni kitu ambacho kinachanganya wengi pale ambapo mishahara ya wengi inafahamika lakini watu wanakuwa mamilionea au bilionea bila vyanzo kujulikana na usalama wa taifa, takukuru nk kukaa kimya bila kuhoji au kuchunguza. Fedha holela zimekuwa zikitumika Tanzania.

  Fedha za rushwa, ulaghai, wizi, mikataba mibovu ndio chanzo cha mfumuko wa bei , kwani fedha hizi zinaingia kwenye mzunguko bila ya uwiano wa kazi au biashara. Ndio manaana leo bidhaa zinapanda bei bila uwiano wowote na vipato.

  kesi hii kama kweli itanguruma itatoa mwanga mkubwa wa jinsi fedha chafu zinaingizwa mtaani. Sheria itasaidia kuangalia na kuchambua na kuweka mizani. Ni ukweli usiopingaka kesi kama hizi huwa ngumu kwani nyaraka nyingi zinakuwa sio za wahusika. Ila kwa sababu mali zisizohamishika zipo tutajua mbichi na mbivu.

  Nina muomba mwanasheria kijana awe jasiri aende mahakamani kwani kama ni kweli yeye sio bilionea hana la kuogopa, ila siku saba zikiisha nisipomwona kisutu nitastaajabu sana.

  Tanzaia huru kiuchumi inawezekana, tukimaliza kasumba ya kuogopa wanaotufilisi.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  May 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Tunasubiri hizo siku saba tushuhudie huu mtanange!
   
 7. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Riziwani alikurupuka. Angekaa kimya kama mmiliki wa Kagoda
   
 8. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama alikurupuka mkuu. Lazima alipata ushauri kwa wakubwa, na Docs nyingi zitakua zimebadilishwa.
   
 9. S

  Sio Mwanasiasa Senior Member

  #9
  May 7, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mtikila me hata simuamin,alisemaga sumaye fisadi thn juzi hapa kasema alikosea kipind kile kusema vile hivyo sumaye mtu safi..na anachukuaga hela kwa rostam huyu..ha ha haa..TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE
   
 10. Guyton

  Guyton JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ngoja tuone, ila kwa vyovyote vile dogo alikulupuka hasa alivyotaja mali zake kwani kama kesi itaunguluma basi lazima ukweli utajitenga na uongo hatakama watamtetea kuwa sio mali zake.
   
 11. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  kazi ipo!!
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mzee wa kesi anataka amfunze mwanasheria wakusadikika..
   
 13. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,128
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  Mtoto kaingia meli ya wagiriki huyo..haya sasa,..yetu macho..slaa + mtikila...atatoka kweli?
   
 14. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,128
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo hapo..mtikili ichi kichwa nakiaminia..lazma atakuwa na ma' evidence ya kutosha tu.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  huyu dogo ataupata urais?
   
 16. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tusubiri baada ya siku saba tuone part 2 ya hii movie!!!
   
 17. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Kama sikosei hii muvi sasa iko part two au three na episode ya tatu, episode ya kwanza ilibebwa na Mheshimiwa Dr. Slaa, Ya pili ikabebwa na main Character wake Rev.Mtikila ya tatu ikabebwa na RizOne oooh sorry hii ya Rev Mtikila itakuwa Part two episode four! Mnikumbushe twende sawa ili tusichanganye hili muvi! Kama PRISON BREAK vilee eeeh
   
 18. kawakama

  kawakama JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  ni kama hadith za sungura na fisi..sungura(dr na rev) lazima ashinde tu
   
 19. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nchi hii bwana! Sijui hizi sarakasi zitaisha lini? Hapa inanikumbusha kibao cha Prof J kiitwacho bongo dar es salaam ambapo alisema ALYEUZA CHENI KAPEWA PESA YA BANDIA NA ALIYETOA PESA KAPEWA CHENI YA BANDIA!!! Hapo waswahili mnasema ngoma droo!

  Ngoja tuisubiri hiyo extra time itakuwaje kwani mshindi ni lazima apatikane hata kwa njia ya matuta.
   
 20. M

  Mountainmover Member

  #20
  May 7, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hiyo jeuri ya kwenda mahakamani anayo? SIKU ZOTE WAMESHINDWA KUMPELEKA DR. SLAA MAHAKAMANI KUPINGA SHUTUMA ANAZOIBUA.
   
Loading...