Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
Mtikila aenguliwa mwenyekiti mwakilishi TCD
2008-07-23 09:38:34
Na Simon Mhina
Umoja wa vyama visivyo na wabunge umemuengua mwenyekiti wa chama cha Democratic, Mchungaji Christopher Mtikila kuwa mwenyekiti mwakilishi katika Kituo cha Demokrasia Nchini (TCD) kwa madai kwamba ana tabia ya kutotaka ushauri na ni kigeugeu.
Mwenyekiti wa UPDP, Bw. Fahmi Dovutwa moja ya chama kinachounda umoja huo, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa, Mchungaji Mtikila ameenguliwa rasmi wadhifa wake wa kuwa mwenyekiti mwakilishi TCD.
Alisema wenyeviti wa vyama vya NLD, SAU, PPT-Maendeleo, CHAUSTA, Jahazi Asili, UPDP, TADEA na UMD wamekubaliana kumuondoa kwenye nafasi hiyo ya kuwakilisha TCD na nafasi yake amechaguliwa Bw. Kasim B. Ali ambaye ni mwenyekiti wa Jahazi Asili kuanzia Julai 20 mwaka huu.
Akifafanua Bw. Dovutwa alisema wana umoja huo walikutana jijini Dar es Salaam Julai 20 mwaka huu, kujadili tabia ya mwenyekiti mwakilishi wao Mchungaji Mtikila ambapo walifikia makubaliano ya kumuengua.
``"Kadhia hiyo ya Mchungaji Mtikila ni matamshi yake ya mara kwa mara ambayo yanamuondolea uadilifu katika uongozi wa kijamii. Sifa ya mtu au kiongozi kutotaka ushauri ina maana anajua sana au anajua kila kitu, sifa ambayo haipendezi kuwa nayo binadamu,`` alisema Bw. Dovutwa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Alisema baada ya mjadala wenyeviti waliridhika kwamba matamshi ya Mchungaji Mtikila mara kwa mara yanayolenga chuki pamoja na kumwita lakini amekuwa hataki.
Hata hivyo, akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mchungaji Mtikila alisema hatambui kuenguliwa katika wadhifa aliokuwa nao.
Alisema madai ya kuenguliwa kwake yana mkono wa mafisadi.
Mchungaji Mtikila alimshutumu aliyetangaza uamuzi wa kumtimua, kwamba ni kibaraka 'aliyeonjeshwa' bahasha na mafisadi.
Akijibu madai ya Bw. Dovutwa kwamba amekuwa haeleweki kutokana na kutokuwa na msimamo, na kuwashambulia baadhi ya wanasiasa waziwazi, Mchungaji Mtikila alisema tabia hiyo ni kweli anayo na ndiyo siasa yenyewe.
``Ni kweli walio wengi hawanielewi, lakini ninachokifanya huo ndio msingi wa siasa, leo naweza kukusifia na kuwa pamoja nawe kama umefanya jambo jema, lakini ukienda kinyume na taratibu nitakukosoa na kukusema hadharani, hata kama ulikuwa rafiki yangu, hii ndiyo siasa,`` alisema.
Hata hivyo, alisema amewasiliana na wenzake katika umoja huo na wamebaini kwamba hakuna kikao kilichoketi kumfukuza, bali kilichofanyika ni utumishi uliotukuka wa Bw. Dovutwa kwa mafisadi.