Mtikila Adai Kakobe ni Nabii wa Uongo, Amtaka Akae Kimya !!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila Adai Kakobe ni Nabii wa Uongo, Amtaka Akae Kimya !!!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Apr 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,339
  Likes Received: 3,229
  Trophy Points: 280
  KAZI KWELI KWELI

  Mtikila Adai Kakobe ni Nabii wa Uongo, Amtaka Akae Kimya


  Mchungaji Mtikila Saturday, April 18, 2009 4:43 AM

  Mchungaji Mtikila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha DP amemtaka Askofu wa Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe kutulia kimya kwani Kakobe anajulikana ni nabii wa uongo na mengi yanayomhusu yeye na kanisa lake yanajulikana
  Mtikila aliyasema hayo alipotakiwa kujibu hoja ya mwandishi mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa.

  Swali, Wewe na Kakobe wote ni wachungaji wa kondoo wa Mungu inakuweje mkapingana maana yeye hivi karibuni alisema DECI ni ya shetani na wewe unasema kuwa ni sehemu ya ukombozi wa mtanzania je hili likoje

  JIBU, Kakobe yeye anajulikana maana anaposema DECI inashirikiana na mashetani wa kuzimu je yeye ameshawahi kufika huko, lakini hatushangai kwa Kakobe kwani hata waumini wake wanajua anavyowaongoza kwa maana inafikia hata kuwalazimisha wavue heleni za Dhahabu wampe yeye kama sadaka pia hupita nyumba hadi nyumba kuorodhesha mali za waumini ili wamtolee yeye, Yote haya si mambo mageni kwa Kakobe.

  Pia ni nabii wa uongo Maana alitabiri kuwa Mrema atachua Urais lakini hakuchukua ,pia kipindi kingine alisema Mrema asipokuwa Rais anaacha kazi ya Uaskofu je ameacha?.

  Mtikila aliyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa habari juu ya Taasisis ya DECI ambayo imekuwa gumzo katika jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

  Deci imeweza kujizolea umarufu mkubwa kwa kuwajaza mapesa watanzania wenye kipato kidogo kwa kutumia kauli mbiu isemayo Panda Mbegu Vuna mbegu ambapo ukipanda Shilingi 200,000. unavuna 500.000 kila baada ya miezi 4.

  Hivi karibuni serikali ilitoa tamko kwa wananchi kuwa Deci haina vibali na inaendesha shughuli zake kama upatu jambo ambalo linaweza kuwasababishia hasara.


  Na Kaimanzila, Dar

  Mtumie Rafiki Yako
   
  Last edited by a moderator: Apr 19, 2009
 2. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh patamu hapo...wacha tumsikilizie Kakobe atajibu nini!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,339
  Likes Received: 3,229
  Trophy Points: 280
  uzuri ama ubaya wa kakobe anafuata nyakati ama anasoma nyakati wapi pa kushabikia akijua soln yake ni positive;sasa mtikila kilichofanyika mwanzoni alisema ni ufunuo wa mungu baada ya kuona serikali inawabana na dalili za kufungwa DECI akahama fasta;akujua mwenzake alisoma nyakati;
  waache wafu wazike wafu wao
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 8,388
  Likes Received: 5,212
  Trophy Points: 280
  hivi mtikila ni mchungaji wa kweli au ni mvurugaji?
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,619
  Trophy Points: 280
  Ni mchungaji wa kweli wa tumbo lake, ni mbabaishaji, oportunist besides all, he is insane. Akiwa katika hali nzuri, ana argument za maana kama hoja ya serikali ya Tanganyika na mgombea binafsi. Anacheza na oportunities kuvuta fungu kwa Mengi kumkandia Manji na kuvuta kwa Manji kumkandia Mengi etc.

  Uthibitisho kuwa he is in sane niliupata kwenye sakata la uchaguzi wa Tarime, akitoa signed statement hii kwenye ITV, na kesho yake kutoa completely opposite statement akidai ile ya jana yake, ilighushiwa. The same applied kwa fungu alililoomba kwa Manji na kudai alikopa huku saini yake imeghushiwa.
   
 6. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  I'll be greatful to see Kakobe's reaction
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,938
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Lipi alilosema mtikila ni la uongo?
  //
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Apr 19, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 10,437
  Likes Received: 2,692
  Trophy Points: 280
  Hey wachungaji wenzangu vipi??

  1. Sioni sababy ya Mtikila kutoa comments kama hizi, it was enough just to say 'hayo ni mawzo ya ke au mtazamo wake' na akathibitisha from Bible where he thinks DEC IS RIGH?

  2. kwa upande mwingine sijaona mantiki ya Kakobe kusema kuwa DECI ni ya kishetani na ina nguvu za kuzimu!! ilikuwa tosha sana aseme kimaadili ya Kikisto hiyo haikubaliki , na akamalizia msumari kwa kutoa maandiko!

  My take I can relate DECI and gambling;

  The Sin of Gambling
  Is gambling a sin? What does the Bible say about gambling?

  Inaweza tu isiwe kama gambling pale tutakapopata taarifa in details kuwa DECI huwa wanafanyia nini hizo pesa?? na mtu anapataje faida?

  Kama hatutarelate DECI na Gambling basi ni kuwa ina promote uvivu na inadumaza ubongo wa watu kutofanya kazi, inaongeza kutokumtegemea Mungu(spiritual point of view) na vyote hivi ni dhambi mbele za Mungu.

  Ikiwa kila kitu kiko genuine kama kupeana mishahara kati ya watu wanne, then no problem!
   
 9. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 2,861
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180
  Well-done kwa reply yako imenena yaliyo sahii kabisa,Mambo ya Mtikila kila mtu anayajua ni mlopokaji kweli anatumia kupakazia watu.
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  ...Hii interview ulimfanyia wewe au kulikuwa na press briefing?? halafu kama umeikata vile ina maana haijaja kamili maana nimjuavyo mtikila hufafanua hoja zake kwa undani sana akishawishi tumwelewe.
  Lakini vyote ni kwamba DECI imeshaundei na yeye anasima a wapi sasa?? sijaona msimamo wake ktk post yako.
  tafadhali tafadhali
   
 11. M

  Magehema JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 446
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  The good thing with Kakobe is that he will buy time trying to contemplate before making any counter statement.
   
 12. R

  Renegade JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,412
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Walau Kakobe anayo makanisa ya FGBF yamepandwa sehemu mbalimbali nchini. Lakini Mtikila sijasikia kuwa na kanisa.
  Hiyo haishangazi maana Biblia inasema Kuna Wachungaji wa kweli na wa Mshahara.Naona huyu ni wa mshahara, na wanatambuliwa kwa matunda ya kazi zao.
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kwamba Kakobe ni tapeli, kama most of maaskofu na wachungaji, including Mtikila.
   
 14. m

  mdm.brown New Member

  #14
  Apr 23, 2009
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtikila ni mwongo sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
  hii jamaa mambo ya uchungaji wa kondoo wa Mungu yalimshinda siku nyingi. He has lately been some sort of a guy ambaye anaongea pumba tuuu!!!!Haeleweki hata nukta.
  hebu tizama alivoitisha mkutano wa hao wanacham wa DECI siku chache zilizopita, hakuna aliyetokea? Ni kwasababu huwa hana la msingi la kuzungumza zaidi ya kurusha matusi tu na mtu anaitwa ati mtumishi wa Mungu.
  kwanza yule ni mtumishi wa Mungu wa kondoo wepi? Au DP ni kanisa?
  wengi wa wanaoitwa watumishi wa Mungu these days wanapotetea utumbo wao hutumia maneno matupu na hawaquote vifungu vya vitabu vitakatifu wanavyoviamini in this case The Holy Bible. Wanongea siasa tu na waumini wao LAKINI with Kakobe it's different. Anapotetea hoja fulani ni lazima ataquote kifungu cha bible. Kwa wale wafuatiliaji wazuri wa vipindi vyake ni mashahidi katika hili.
  anaposema waumini wake wasivae dhahabu ana ushahidi wa kibiblia lakini kwasababu watu wengi hatupendi kuappear bila hizo accessories tunaona jamaa anabana kumbe ukweli wa Bibli ndio huo. Kama kiongozi wa dini kama Mtikila anashindwa kuwaongoza waumini wake kwa msingi wa Biblia NA AKAE KIMYA KABISA MAANA BIBLIA HAIJUI............
  Kakobe hana haja ya dhahabu za watu, watu tuache zogo, watu wengi wanamzushia maambo tu maana anavohubiri anasema kweli halafu anatuchoma alafu sisi tunammaind kwa kusema ni muongo. Mbona washirika wake wako pina tu hawapati taabu wala hawajawahi kumpa hizo dhahabu walizokuwa wakizivalia zamani zao? Washkaji fanyeni research badala ya kuchonga na kumsikiliza mpuuzi kama Mtikila, hajui hata analolizungumza.
  ninamsupport kakobe kwa kusema DECI sio kitu cha kiMungu maana Holy scriptures zinatuagiza kufanya kazi ili tule na sio kupata pesa za kibure kama za deci.
  hata kwa maarifa madogo ya kiuchumi, DECI sio kitu kizuri kwa uchumi wa nchi kaulize BOT uambiwe.........
  ndio maana serikali huwa inafuta michezo yote ya kiupatu inapoibuka na kukusanya wananchi wengi kama ilivokuwa DECI.
  Ni heri DECI imefutwa it's for the betterment of Tanzanians pamoja na kwamba watu wengi baaaado hatuelewi..................
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  MDM.Brown
  Nakuunga mkono nishawahi kuwa muumini pale kwa kakobe nilipokuwa mtoto.
  usemacho ni amini nakweli.
  Amani Iwe nanyi
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,625
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mambo ya Kakobe ni hatari maana yanawatayarisha wengi kwenda jehanamu. (Hold on) Najua wengi wataanza kunishambulia lakini ni hivi:-
  Watu wengi sana wana negative attitude toward Kakobe, na kila mtu amekuwa akijaribu kusema lake, hata kama ni kweli au ni hearsay.
  Lakini nawaonya wale wasio na hakika na Kakobe maana wanaweza kupotelea mbali.
  Kuna mfano ulio hai. Kwa miaka ya nyuma kidogo nadhani 1990's wengi walimsema Kakobe vibaya sana. Wachungaji na washirika wa makanisa mengi walikuwa wakisema ovyo kuhusu huyu bwana. Hata yeye naye alikuwa katika mtililiko huo huo kama anavyofanya leo kwa Deci.
  Mara baada ya uchaguzi wa 1995 alipokuwa akim backup Mrema alipotea kwa kipindi cha miezi mitatu hivi akiwa hajulikani alikokuwa. Yeye anajua. Inasemekana alikuwa katika maombi na toba kwa kusema unabii wa uongo. Sijui ni kweli au la lakini inaweza kuwa kweli maana alipotoka huko kitu cha kwanza alikana kuhusika tena na TLP. Kisha akaanzisha toba na wachungaji wenzie aliokuwa na beef nao. Kwa kuanzia mzee Kulola.
  Hapo tukaona woooooote hawa wachungaji wakiingia katika toba kila mmoja kwa ajili ya kumsema mwenzie vibaya. Ukaanzishwa na huu umoja wa kipentekosti na wakafanya maazimio ya ajabu ajabu.
  Nilibaki najiuliza je wale wachungaji wa makanisa mengine ya kipentekosti na wachungaji wa Kakobe ambao hawakupata nafasi ya kufanya hii toba na walishafariki, je wako wapi katika ulimwengu wa roho? maana wao hawakupata nafasi ya kutubu kwa mambo yaliyoanzishwa na Kakobe na colleagues wake. Sasa kwa hili wako wapi? Na wale wachungaji wengine plus wale wa mchungaji Kakobe waliokuwa wanaongoza hizi kampeni za kuchafuana na walifanya toba hii wanafikiri walifanya vema kuwa lead wenzao kwenda jehanamu?
  Mimi siwezi kusema mengi kuhusu Kakobe. Nimekuwa nikifuatilia sana uongozi wa kanisa lake na hata makanisa yake ya kule mikoani. Yeye kama yeye ana mapungufu mengi tu ambayo asipotubu pia kuna hatari mbele ya safari. Asijihesabie haki. Mbinguni hatutaingia kwa sababu tulikuwa maaskofu au maaskofu wakuu. Hatutaingia mbinguni kwa sababu tulifanya miujiza mingi. Bali tutaingia mbinguni kama tu tuna chapa ya mwana kondoo wa Mungu na tumevumilia mpaka mwisho tukiwa na imani na utakatifu.
  Kakobe anatakiwa achunge sana ulimi wake maana hivi ndivyo biblia inasema. Kwamba huu ulimi ni kitu kidogo lakini unaweza kuendesha meli au kuizamisha. Mara nyingi ile tabia ya kuwasema ovyo wapakwa mafuta wengine wa Mungu si kitu cha kimungu. Mara nyingine katishia watu walio critical naye kuwapleka mahakamani na kuwadai pesa nyingi. Ni lazima ajichunge sana. Tena si yeye peke yake bali hata watumishi wengine wa kanisa lake wameambukizwa kaugonjwa haka. Kusema kweli anawapoteza.....
  Niliwahi kusikia story kutoka kwa rafiki yangu mmoja ambaye pia alikuwa ni rafiki yake Kakobe miaka ya nyuma wakati akianza huduma kuwa Kakobe aliwahi kumwambia kuwa alikutana na Shetani na shetani akamwambia ampe upako ili awe na karama za miujiza. Lakini Kakobe alikataa. Mimi nilijiuliza maswali mengi sana kwamba hivi huu mwanzo wa majadiliano ya Kakobe na shetani yalianza vipi? Na nilitia mashaka sana hii story kuwa ni propaganda tu kama kawaida inayoendeshwa dhidi yake na sikupenda kuamini kwamba huu ni ukweli na hii ndiyo hearsay. Lakini nilishangaa niliposikia akitoa ushuhuda wa jambo hili hili katika tv kwenye vipindi vyake mwaka jana. Nilibaki nikijiuliza je yale ambayo niliambiwa na huyo bwana ambayo hakuyasema yote kumbe ni kweli?
  Kakobe si mtu wa kuamini sana ingawa anaitumia biblia na kufanya miujiza mingi. Kuna mengi yanatufanya tusimwamini yeye ingawa tunakubaliana na yale anayofundisha. Maana neno la Mungu li hai nalo lina nguvu.
  Naomba Mungu amsaidie pia na kumponya na kiburi (proud) maana Mungu anachukizwa na hili pia.
  Watu wa Mungu tuwe makini. Kakobe atapeleka wengi jehanamu, hata wasiokuwa wa kanisa lake.
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Aisee dogo tanguliza shikamoo..
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  nani mie au dogo mwingine?
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,339
  Likes Received: 3,229
  Trophy Points: 280
  Walau Kakobe anayo makanisa ya FGBF yamepandwa sehemu mbalimbali nchini. Lakini Mtikila sijasikia kuwa na kanisa.
  Hiyo haishangazi maana Biblia inasema Kuna Wachungaji wa kweli na wa Mshahara.Naona huyu ni wa mshahara, na wanatambuliwa kwa matunda ya kazi zao.


  WEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE HUYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
  NGOJA NIWAAMBIE CHANZO CHA KUJIITA MCHUNGAJI.......
  MTIKILA ALIKUWA ANASALI KANISA MOJA LILILOKUWA LIKIABUDU PALE SHULE YA JAMHURI 90'S BAADA YA HAPO ALIKUWEPO MCHUNGAJI WA HILO KANISA AMBAE ALIKUWA ANASAFIRI MARA KWA MARA USA...BADA YA KUONA HIVYO MTIKILA AKAANZA KUHOJI UKO NJE UNAEDNA KILA SIKU KUHUSU KANISA MBONA UTUPI FEEDBACK....LINGINE LILOMKIMBIZA HILO KANISA MWEKA HAZINA ALIKUWA MKE WA MCCHUNGAJI WATU WAKAFUMBWA MACHO KABISA ...ALIPOANZA KUHOJI AKAAMBIWA KAMA UNAHOJI UHALALI WA HILI KANISA KIMBIA NA USIONEKANE KANISANI...HAPO NDIPO ALIPOKAA N A WATUMISHI BAADHI AKAWAKOMNVVINCE JAMANI HAPA MCHANGA WA MACHO...AKAENDA NAE KUANZISHA KANISAA LILE LIE LINAITWA FULLSALVATION CHURCH...BAADA YA HAPO JAMAA NAE AKAANZA KULA PESA ZA SADAKA WASHARIKA WAKAKIMBIA NDIPO FILAMU YA UCHUNGAJI WA MTIKILA ULIPOISHIA....ANYAWAY ALISOMA NYAKATI MAANA BAADAE HILO KANISA ATI LIKAITWA ARKFOUNDANTION CHURCH...KISA TU KULIKUWA NA SPONSER MMOJA ALIKUWA MAREKANI ANATOA MSAADA SO MISAADA INAINGIA WATUMISHI HAWAIONI...
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,339
  Likes Received: 3,229
  Trophy Points: 280
  Kakobe si mtu wa kuamini sana ingawa anaitumia biblia na kufanya miujiza mingi. Kuna mengi yanatufanya tusimwamini yeye ingawa tunakubaliana na yale anayofundisha. Maana neno la Mungu li hai nalo lina nguvu.
  Naomba Mungu amsaidie pia na kumponya na kiburi (proud) maana Mungu anachukizwa na hili pia.
  Watu wa Mungu tuwe makini. Kakobe atapeleka wengi jehanamu, hata wasiokuwa wa kanisa lake.


  MKUU MCHUKIA FISADI HALLEEEEEEEEYUUUUUUUUUUUUUUUUAAAAAAAAAAA
  KWANZA UABARIKIWE NA BWANA WAONEKANA MTU WA KIROHO....
  BIBLIA INASEMA NA ALAANIWE AMTEGEMEAE BINADAMU....NA HAPO HAPO BIBLIA IANSEMA TUWAAMINI MANABII ,WATUMISHI NA MITUME ....KAMA UNAKUMBUKA ELISHA ALIPELEKEWA MKOMA MMOJA ALIPOFIKA YULE MWENYE UKOMA ALIKUWA NA HELA AKAAMBIWA AKAJICHOVYE KWENYE MTO MARA SABA WENYE MATOPE...AKA KATAA..AKIWA NJIANI MJAKAZI WAKE AKAMUHIMIZA NDIPO ALIPOENDA KUFANYA ALIYOAMBIWA ..ALIPOPOONA ALIENDA KUTAFUTA SADAKA KUBWAAAA NA KUMPELEKEA ELISHA ...ELISHA ALIZIKATAA NA KURUDI NAZO..ILA ALIKTAA SABABU KWANZA HAKUWA NA IMANI NA ELISHA NDIO MAANA AKUTAKA KUPOKEA ...MAANA KUNA MAMA MWINGINE ALIMTENDEA MIUJIZA AKAWA ANAKULA KWAKE KILA MARA....NINI MAANA YANGU TUNAITAJI KUAMINI WATUMISHI WA MUNGU NA SI KUFANYAYALE WANAYOFANYA..........KWELI KAKOBE NI KAMA WATUMISHI WENGINE ,SIKATAI NI BINADAMU ANA MAPUNGUFU YAKE ...MI NILICHOKUWA AMA NIACHOPENDA NI WEWE JE UMEITAYARISHAJE ROHO YAKO BAADA YA KUFA;AMA SIKU YA MWISHO MAANA BIBLIA INATUAMBIA HATUTALALA WOTE.......NDUGU YANGU NA WENGINE WOTE MNAOSOMA jf

  kama UNATAKA KWENDA MBINGUNI NJIA NI MOJA TU

  KUOKOKA

  2WAKORINTHO 6:2 INASEMA ""KWA MAAANA ASEMA WAKATI ULIOKUBALIKA NALIKUSIKIA SIKU YA WOKOVU NAKUSAIDIA;TAZAMA WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA SIKU YA ((WOKOVU NDIO ((SASA)) MPENDWA HAKUNA WOKOVU BAADA YA KUFA...NANI AMEKWAMBIA MI NITAENDA KUTUBU UKO KWA MUNGU WAEBRANIA 9:27 INASEMA KAMA VILE WANAVYOWEKEWA KUFA MARA MOJA NA BAADA YA KUFA ((HUKUMU)) TENGENEZA MAISHA YAKO SASA......BADILISHA MAISHA YAKO SASA.....UKISHAKUFA INAYOBAKIA NI HUKUMU TU WACHA KUJIDANGANYA NA DINI ULIOKUWEPO NA KANISA UNALOSALI NA MCHUNGAJI ANAEKUHUDUMIA...TENGENEZA MAISHA YAKO SASA

  HAWA WATUMISHI SIKATAI WANAMAKOSA YAOOOO LAKINI MI NAWASHAURI MWACHIENI MUNGU AWAFINYE KWENYE KONA KWA MUDA WAKE....NAKWAMBIA UKWELI HATA KAMA KAKOBE AMEKOSA KAMA MUNGU ALIPANGA ROHO YAKE KUWEPO MBINGUNI SIKU YA MWISHO ATAKUWA HUKO.......TAZAMA WENGI WANAWASEMA WATUMISHI OOOOOOOOOOOOHHHHH WANAKULA HELA ZA SADAKA ....ZA MICHANGO.....SOMA MALAKI 3:11 ANASEMA NAMI NITAMUDHIBU YULE ALAE HEKALUNI MWANGU........
  HAKUNA SEHEMU ILIOANDIKWA MWANADAMU AMUADHIBU MCHUNGAJI....NI MUNGU ATASEMA NAO NYIE MSIWE NA WASIWASI WE TENGENEZA MAISHA YAKO KWANZA AMENNIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII JINA LABWANA LIBARIKIWE

  SHALOM
   
Loading...