Mtihani wa Hesabu Kidato cha nne wafutwa leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani wa Hesabu Kidato cha nne wafutwa leo

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Buswelu, Oct 6, 2008.

 1. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mtihani uliko kuwa ufanyike leo asubuhi wa hesabu kidacho cha nne umefutwa nchi nzima mpaka hapo baaada...sababu zinazosemkena ni kuvuja kwa mtihani...Dar es salaam.

  My Take...

  Inawezekana kabisa ni kwa sababu ni maslahi madogo kwa walimu...na mgomo ambao unatakiwa ufanyike leo...
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Isije kuwa imeshavuja kama kawaida ya wabongo atii...wameshapiga baoo wizara na necta yake
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Jamani huu mtihani umekutwa sinza kwa muuza maandazi anamfungia mtu bila kujua ni karatasi gani na toka majuzi umeombwa ufutwe wanafiki wezi fisadi wakubwa mama sitta na kampuni yake
   
 4. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #4
  Oct 6, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni ukweli kabisa wa jinsi tulivyo watanzania.

  Taarifa nilizo nazo ni kuwa kuna uwezekano hata wa civics leo mchana nao ukafutwa au hata mitihani yote.Tusishangae, habari ndo hiyo
   
 5. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kufutwa kwa Mtihani mimi naona SAFI SANAAAAAAAAAAA!

  Hongera WIZARA NA WAHUSIKA

  My take: Kama hatukuweza kukomesha haya basi mwisho wake ndio MAFISADI ++ kwa kizazi kijacho.
   
 6. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #6
  Oct 6, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii mitihani karibu yote imevuja, maana karibu kila mwanafunzi wa kidato cha nne ninayekutana nae wanayo..... jamani inasikitisha kizazi hiki kha !!! Hebu fikiria kuna shule kila mwanafunzi mzazi wake katoa lak 2 la kununuliwa paper "sumu" Inasikitisha halafu shule yenyewe unaikuta eti iko kwenye Top ten khaaaaa...............
   
 7. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa wazazi wanaotoa pesa kwa watoto wakanunue mitihani ndio wanapaswa kushughulikiwa, kama mzazi unajenga msingi gani kwa mwanao?
   
 8. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #8
  Oct 7, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mi mwenyewe huwa najiuliza baada ya kumfanyia mtoto wako hivyo, haya kesha faulu Je huwa mzazi anajisikaije moyoni mwake... yaani nahisi roho yake inakuwa inamuhukumu tu... hata furaha ya kwamba mwanao ana akili unakuwa huna
   
 9. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii haina tofauti na kumtuma mtoto wako akaibe kwa jirani au dukani kwa vile huna pesa za kununua chakula!!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,844
  Trophy Points: 280
  Date::10/7/2008
  Mitihani zaidi kidato cha nne yavuja Necta iko njia panda

  Na Mwandishi Wetu
  Mwananchi

  BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) bado liko njia panda kuhusu hatua za kuchukua baada ya mtihani mwingine wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu kuthibitika kuwa umevuja.

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa siku kadhaa sasa unaonyesha kwamba, wanafunzi wa kidato cha nne tayari walishakuwa na mitihani hiyo, hivyo wamekuwa wakijibu maswali katika maeneo mbalimbali ya nchi kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani.

  Juzi Baraza lilitangaza kuufuta mtihani wa somo la Hisabati ambao ulikuwa uanze kufanywa kwa kile kilichoelezwa kuwa umevuja na kwamba, vyombo vya usalama vinafanya uchunguzi zaidi kwa mitihani mingine ya Kiswahili, Kiingereza, Fizikia na Uraia inayodaiwa kuvuja.

  Lakini jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi lake linawashikilia wanafunzi wawili kutoka kituo cha Perfect Vision, mmoja kwa tuhuma za kukutwa na majibu ya mtihani wa somo la Civics (Uraia) na mwingine kwa kumfanyia mwenzake.

  Kamanda Kova alisema watuhumiwa hao, walikamatwa juzi saa 11:00 jioni wakiwa katika kituo hicho kilichopo maeneo ya Ubungo karibu na nyumba za Shirika la Nyumba nchini.

  Kwa mujibu wa Kamanda Kova, mwanafunzi wa kwanza kukamatwa ni mtahiniwa wa kujitegemea Rhoda Juma Mombora (37) ambaye alikamatwa na majibu ya mtihani wa somo hilo uliofanywa juzi mchana. Mtuhumiwa wa pili, Clara Haule (20) mkazi wa Makumbusho alikamatwa akimfanyia mtihani Anjela Maganga mwenye namba P1475/0023.

  Kova alisema watuhumiwa hao, wanashikiliwa na polisi na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. Idadi ya watuhumiwa inafikiriwa kuongezeka.

  Japokuwa ni watahiniwa hao tu walionaswa, wanafunzi mbalimbali waliozungumza na Mwananchi katika maeneo mbalimbali nchini na jijini Dar es Salaam walidai kuwa wana mitihani yote na kwamba hata waliyofanya juzi walikuwa nayo. Walisema baada ya kuingia katika chumba cha mtihani walibaini kuwa ndiyo yenyewe.

  "Mitihani yote tunayo hata ule wa jana (juzi) wa somo la Uraia (Civics), tulikuwa nao na baada ya kuingia katika chumba cha mtihani tulibaini kuwa ndiyo wenyewe, swali mpaka swali," alidai mwanafunzi mmoja wa jijini Dar es Salaam (jina tunalo).

  Mwanafunzi huyo alidai kuwa walipata mitihani hiyo kutoka kwa watu walio karibu na Baraza baada ya kuchanga fedha na kuwapatia watu hao.

  Mazingira ya kuvuja kwa mitihani hiyo yanaonyesha kuwa iliibwa kutokana na mpango wa ndani uliosukwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kwa lengo la kujipatia kipato.

  Kwa mujibu wa uchunguzi huo baada ya kupata mitihani wanafunzi hao wamekuwa wakitumia simu za mikononi kupeana maswali au majibu kabla ya kuingia katika chumba cha mitihani.

  Katika hatua nyingine Umoja wa Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya juu nchini (Tahliso) umetaka mtihani wote wa kidato cha nne ufutwe na kisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na watendaji wakuu wa Baraza kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo ambayo mara ya mwisho ilitokea mwaka 1998.

  Katibu Mkuu wa Tahliso, Mtatiro Julius alisema jana jijini kuwa, kashfa ya kuvuja kwa mitihani hiyo inawahusu viongozi hao moja kwa moja na hivyo hawapaswi kukwepa kuwajibika.

  "Waziri anapaswa kuwajibika mwenyewe kwa kulinda heshima yake, lakini zaidi kwa manufaa ya umma kwani ameshindwa kuwasimamia vema watendaji wa chini yake," alisema Mtatiro na kuongeza:

  "Kitendo cha mitihani kuvuja na serikali kuufuta mmoja na kuacha mingine iendelee kitazalisha wasomi wasiokuwa na uwezo,".

  Kwa mujibu wa Mtatiro, inasikitisha kuona serikali inakiri kuvuja kwa mtihani wa Hisabati kwani kauli hii inaleta uwezekano wa mitihani yote kuwa imevuja kwa kuwa mitihani hiyo iliandaliwa pamoja na kusambazwa pamoja.

  "Hali ya kuvuja kwa mitihani nchini imekuwa ya kawaida sana ingawa miaka mingine serikali inakanusha tuhuma hizo. Katika hili la mwaka huu, ni lazima Rais Jakaya Kikwete atumie nafasi yake kuwawajibisha watendaji wake," alisema.

  Mtatiro alibainisha kuwa tatizo la kuvuja kwa mitihani nchini linatokana pamoja na mambo mengine tamaa ya fedha na walimu kutolipwa mishahara mizuri.

  Aliitaja sababu nyingine ya kuvuja kwa mitihani kuwa ni ubinafsi na uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu katika kusimamia mitihani na upole wa Rais Kikwete katika kuwachukulia hatua watendaji wake wanaoboronga kazini.

  "Upole wa Rais Kikwete ndiyo unaosababisha watendaji wa chini wajione kuwa wako huru na hakuna wa kuwawajibisha," alisema.

  Juzi Baraza lilifuta mtihani wa Hisabati baada ya kubainika umevuja. Hata hivyo Baraza halikuwa tayari kutaja sehemu wala watu waliokamatwa na mtihani ambao sasa utatungwa mwingine na kufanywa Oktoba 27, mwaka huu.

  Mwaka 1998, Baraza hilo lilifuta mitihani yote baada ya kubaini kuwa mingi ilivuja na hivyo kulazimika kusogeza mbele tarehe ya kuanza kwa mitihani na hali inaonekana inaweza kujirudia mwaka huu kutokana na mitihani hiyo kuzagaa kama njugu.

  Awali Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dk Joyce Ndalichako alisema baraza hilo limeanza kufanya uchunguzi wa uvujaji wa mitihani mingine nchi nzima baada ya kupata taarifa juu ya kuwepo kwa mitihani zaidi kwenye mikono ya watahiniwa ikiwemo Kingereza, Kiswahili, Fizikia na Uraia.

  Akizungumza na waandishi wa habari juzi kuhusu kuvuja kwa mitihani, Dk Ndalichako alisema vyombo vya usalama vimekamata mitihani ya Kiswahili, Kiingereza, Uraia, Fizikia pamoja na Historia na kwamba, uchunguzi zaidi unafanyika, lakini hakutaja sehemu ambazo mitihani hiyo ilikamatwa kwa kile alichoeleza kuhofia kuharibu uchunguzi unaoendelea.

  Kashfa ya kuvuja kwa mitihani ni mwendelezo wa kashfa mbalimbali zinazoendelea kulikumba Baraza hilo baada ya hivi karibuni kuripotiwa kuibwa vyeti 4,000 vikiwa na namba bila ya majina.

  Imeandaliwa na Jackson Odoyo, Kuruthum Ahmed, Tausi Mbowe na Festo Polea.
   
 11. hamix manko

  hamix manko Member

  #11
  Sep 27, 2016
  Joined: Aug 1, 2016
  Messages: 96
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  B+
   
Loading...