Tena ingependeza angetoa increment za tokea 2015 ambazo hazijawahi kutolewa.Watumishi wa umma wanamaumivu makubwa mioyoni mwao sio siri, hata kama kipaumbele ilikuwa kumaliza kwanza mambo ya msingi kama ujenzi wa miundo mbinu, kuimarisha sekta ya afya na elimu lakini waalihitaji kuonewa huruma.
Waziri mkuu alikatisha watu tamaa kabisa pale aliposema eti kuongeza mishahara watumishi wa umma ni kusababisha maisha kuwa ghali. Jambo ambalo sio kweli maana kwa miaka hii mitano watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara na maisha yamepanda pia.
Siku hazigandi na leo ni tarehe nne na mei mosi ipo karibu, watumishi wa umma watapata faraja kama wakisikia wameongezwa mishahara yao. Swali linabaki kuwa je, mama Samia rais wa JMT ataweza kufanya maamuzi ya msingi kwa ajiri ya watumishi wa umma?