TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitumia vyema mkakati wake wa kuungana na vyama vya CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) na baadaye katika uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani ulifanyika mwezi Oktoba mwaka 2015.
Ni makakati wao(CHADEMA) ndiyo ulipelekea viongozi wakuu wa CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD kuvipa kisogo vyama vyao na kuamua kumuunga mkono mgombea wao, Edward Ngoyai Lowassa. Nawasema Seif Sharif Hammad wa CUF, James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI, na Emmanuel Makaidi(R.I.P) wa NLD.
Ni mkakati wao huo ndiyo uliopelekea Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Tluway Sumaye na Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa kashfa ya Mkataba tata wa kufua Umeme wa dharua ambao serikali iliingia na Kampuni ya RICHMOND, Edward Ngoyai Lowassa kuhamasika kujiunga na Chadema.
Ni mkakati wao huo ndiyo uliopelekea mjumbe wa Kamati Kuu ya CUF na aliyekuwa Waziri katika serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar, Juma Duni Haji kukubali kuwa mgombea mwenza wa Edward Lowassa katika uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kwa kifupi Chadema waliona mbali maana leo tunapoongea hatuna CUF bara, hatuna NCCR-Mageuzi, hatuna NLD.
Changamoto kwa CHADEMA
1. Nani atakuwa mgombea urais wao mwaka 2020? Tayari Lowassa ameshakwenda na utaratibu wa CCM wa kugombea vipindi viwili kwani mara kadhaa amesikika akisema 2020 ni yeye tena bila kujali Katiba ya Chadema haisemi hivyo. Mbowe anaonekana kuvutiwa zaidi na Fredrick Sumaye, tayari ameshamteua kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, lengo ni kumuuza kwa Wajumbe, wanachama na wapenzi wa Chadema.
Changamoto iliyoko hapa ni kwamba WOTE(Sumaye na Lowassa) ni wapenda madaraka(wanaojua wana neno lao wanalolitumia kwa watu wa aina hiyo). Wote walishakuwa Mawaziri Wakuu. Wote ni Wagonjwa ( Kwa mujibu wa Sumayewakati wa uzinduzi wa Kampeni za urais mwaka jana pale Jangwani, Mtanzania yeyote mwenye miaka 50 na zaidi ni mgonjwa). Wote wana tuhuma za ufisadi ila kwa viwango tofauti.
2. Nani atakuwa Mgombea Mwenza wa atakayepeperusha bendera ya urais? Je watamnunua tena mtu kama ilivyokuwa kwa Juma Duni Haji(amesharudi CUF, tena kwa kauli nzito kuwa Chadema kila mtu ni Kijogoo, hakuna mfumo wa Uongozi) au atakuwa Salim Mwalimu ili kumfuta jasho baaga ya kumnyang'anya tonge la kuwa Katibu Mkuu?
3. Chadema wataendelea kuungwa mkono na wafuasi wa NCCR-Mageuzi na CUF? NLD hawapo, walishapotea.
4. Team Lowassa wataendelea kuwa naye au kwa kasi hii ya Magufuli watakuwa wamerudi kundini?
5. Chadema Asili(ile ya akina Dr. Slaa, John Mnyika, Michael Aweda, Ben Saanane, Halima Mdee n.k) -bado itakuwa na bashasha kama zamani au itakuwa imebaki Chadema ya akina Lema, John Mrema, Edward Lowassa, Antony Komu(Kaskazini Line)?
Changamoto kwa NCCR-Mageuzi
1. Chama bado kitakuwa hai na hivyo kusimamisha Wagombea katika nafasi za urais, Wabunge na Madiwani?
2. James Mbatia atakuwa bado ni Kiongozi wa NCCR au ataweka historia ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha siasa ngazi ya Taifa kuhama chama na kujiunga na Chama kingine?
3. Watamuunga mkono mgombea wa CHADEMA?
Changamoto kwa CUF.
1. CUF bara itakuwa hai?
2. CUF zanzibar watakuwa na mkwanja wa Kampeni au tena kampeni zao zitagaharamiwa na LOWASSA ili kuachana na kumsimamisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano?
3. Watamuinga mkono Mgombea urais wa CHADEMA?
Changamoto kwa UKAWA
1. Umoja bado utakuwepo?
2. Watakuwa na mgombea mmoja wa urais?
Mods, mada hii ikiwezekana muiweke juu kabisa ili tuwe tunairejea kadri siku zinapokwenda kuelelea 2020.