Uchaguzi 2020 Humphrey Polepole: Dkt. Magufuli atachukua fomu ya Urais 06 Agosti Dodoma. Mwanachama aliyepiga mazonge kwenye kura za maoni atashikishwa adabu

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi ndugu Polepole ataongea na watanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Mkutano utafanyika ofisi ndogo ya CCM - Lumumba, Dar es Salaam. Usipange kukosa kufuatilia.



Juzi tulikuwa na NEC ilituita vyama vyote, taarifa muhimu tumepewa, kikao kilichopita tulimaliza kikao cha maadili na tukasaini, sheria iko vizuri asiwadanganye mtu, tukikaaga na tume wote tunazungumza lugha moja ni unafiki tu wa wachache. Tena kuna menu na kuna wengine hawaondoki mpaka wale msosi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetutangazia kuanzia leo tunaweza kuchukua fomu kwa ajili ya wagombea wa nafasi ya Urais, Mgombea Urais CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli atachukua fomu wiki hii Dodoma

Hili sikutaka kulisema lakini limetuuma kama WaTZ, juzi wenzetu wamebadilisha maneno ya Wimbo wa Taifa wameweka maneno ya chama chao, najiuliza sisi CCM tuna nyimbo nzuri lakini huu tunauheshimu hatuwezi kuunajisi kwa kuweka mambo binafsi. Nchi hii inatambulishwa na vitu vitatu ambavyo ni jina yaani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pili inatambulishwa na Bendera ya Taifa na mwisho ni Wimbo wa Taifa.

Tufanye siasa lakini tusiguse vitu vinavyotambulisha taifa letu wimbo wa taifa huwa tunaimba tukiwa katikati ya vita, mapigano na ndio kiunganishi chetu kimaombi kati ya taifa letu na Mwenyezi Mungu, waombe radhi Watanzania kwa kuushushia hadhi.

Wawaombe radhi Watanzania ila mimi najua hawataomba radhi, kama mnabisha tu-bet hapa, ni desturi yao nimefanya nao chaguzi nyingi wanavunja sheria, juzi wamemsema vibaya kila mtu kwenye nchi hii, chama hiki ni tatizo kubwa

Siku amerudi jamaa yao, nakuambia siku ile watu hawakutembea barabarani, waliambiwa pita moja, wee wamepita zote na siyo kwamba walikuwa wengi ni kama walikuwa wanapita zigizaga, mimi nimekutana nao pale Kinondoni Studio wapo huku na huku

Unajua wamefika mpaka kwenye ofisi zao Mtaa wa Ufipa, wakaanza kusema mbona hawajatukamata, nikasema kumbe mpango wao ilikuwa kukamatwa sasa hawajakamatwa wanalalamika, hiki chama sikielewa hivi nidhamu ni zero na kutii sheria bila shuruti ni zero

Halafu wanajenga hoja wanasema tuambieni wapi tumevunja sheria, hivi kwenye nchi hii kuna sheria inasema usichukue Mke wa Kaka yako?, mimi nawaachia Watanzania hiki ndiyo chama kabla hakijaomba dhamana kishabadili Wimbo wa Taifa kishafanya wa chama.

Wana-CCM ambao mmeomba dhamana na mlizingatia katiba na kanuni hamkujishirikisha kwenye makatazo na miiko muwe na amani na sisi kama chama hatutawaangusha watu waaminifu na wanyenyekevu na wenye nidhamu, ila wale mlipiga mazonge tutafundisha watu adabu kipindi hiki. Kila mwanachama aliyeshiriki ‘uovu’ katika kura za maoni, atashikishwa adabu.

Nampa pole TID sababu hawa majamaa ni mazulumati wametudhulumu wimbo wa Taifa. TID anapambana mtu wa watu ametengeneza Ni Yeye na ile ilikuwa Magufuli, wale majamaa wameichomeka kule. Hawajamshirikisha hawajamuomba kwa kweli sisi kama Watanzania tutawachukulia hatua.
1596643964326.png
 
Si ange ongelea kwenye lile kongamano la wadada Mh alio wapigia simu? Huu ni mwendelezo wa kuzuia vyombo vya habari visitangaze mkutano wa ACT WAZALENDO. Hawezi kuwaita waandishi muda ule ule ambao ACT wana anza mkutanobaao live.

Sijui anae wapa CCM hizi mbinu za kizamani ana toka wapi kwenye hii dunia. Na tujiulize, Ccm wana ogopa nini?
 
Chama kinatoa tamko pale inapolazimika,sio kama CDM wao kila mtu kila siku ni matamko tu.
 
Si ange ongelea kwenye lile kongamano la wadada Mh alio wapigia simu?
Huu ni mwrndelezo wa kuzuia vyombo vya habari visitangaze mkutano wa ACT WAZALENDO. Hawezi kuwaita waandishi muda ule ule ambao ACT wana anza mkutanobaao live..
Sijui anae wapa Ccm hizi mbinu za kizamani ana toka wapi kwenye hii dunia. Na tujiulize, Ccm wana ogopa nini???

Unaipenda sana CCM sio?

Kama unapenda kuanagalia ACT sasa CCM inakupa shida gani?

Nawaza tu kwa jinsi unavyolalamika, kumbe CCM huwezi kuikwepa ni sawa na maji katika maisha.
 
Bana jipya huyo..sana sana ni panic tu iliyotawala Lumumba nzima!!
 
Back
Top Bottom