Mtifuano kortini mgogoro familia ya Marealle

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,378
4,033
Moshi. Malumbano ya kisheria yameibuka baina ya mawakili wa pande mbili kuhusu maombi ya kuzuia mazishi ya Veronica Mlang’a (105) ambaye alizikwa Jumamosi iliyopita.

Wakili Julius Semali anayemtetea mtoto wa marehemu, Acley Marealle, alieleza mahakama kuwa maombi hayo yamepitwa na wakati kwa kuwa mazishi yalishafanyika.

Hata hivyo, Modestus Njau, wakili anayemtetea, Frank Marealle alililaumu Baraza la Ardhi na Nyumba Moshi kuwa limechangia maombi yao kupitwa na wakati.

Njau alisema lengo lilikuwa ni kuzuia mwili wa Veronica kuzikwa mahali alipozikwa na alitegemea lingetoa amri hiyo, lakini halikufanya hivyo na kusababisha taratibu za mazishi kuendelea.

Maombi hayo yalifunguliwa Jumatano ya wiki iliyopita chini ya hati ya dharura, lakini mwenyekiti wa baraza hilo, Silas James hakutoa zuio, badala yake akapanga kusikiliza maombi hayo jana wakati mazishi yalikuwa yamepangwa kufanyika Jumamosi.

Hata hivyo, walipofika mahakamani hapo jana, kulikuwa na mabadiliko ambapo Silas alimpangia mwenyekiti mwingine, Prosper Makwambi kusikiliza shauri hilo linalovuta hisia za wengi.

Wakili Njau alisema alitarajia jana angekutana na Silas ili aweze kumuuliza kwa nini hakutoa zuio kwa sababu hafahamu ni nini ambacho kilitokea mpaka baraza hilo likashindwa kutoa zuio.

“Baraza limechangia kuonekana mgogoro huu unaanza upya, kutokana na kushindwa kutoa order (amri) ya kuzuia kuzikwa katika eneo hilo hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa,” alieleza Njau.

Mwenyekiti wa Baraza, Prosper Makwambi alisema ikiwa waleta maombi walitaka zuio kwa hati ya dharura, walipaswa kumuona mwenyekiti badala ya kupeleka na kukaa kusubiria.

“Maana mlitaka zuio kwa hati ya dharura, mngemwona mwenyekiti. Lakini kama mlileta maombi na ikatolewa summons (wito), hiyo si oder (amri) ni wito na halikuwa zuio,” alieleza mwenyekiti.

Baada ya kauli hiyo, Wakili Njau alisema “kwa kuwa baraza limechangia (kutotolewa zuio la kuzika), tunaomba mwongozo kama ni kufukua mwili tukafukue.”



Hata hivyo, Wakili Semali alisema maombi yaliyopo mbele ya mahakama yamepitwa na wakati na hakuna kesi ya msingi, na kama bado mleta maombi anaona maombi hayo yana mizizi, basi na mjibu maombi apewe muda kuyajibu.

Wakili huyo alisisitiza hakuna kesi ya msingi, na kama ni suala la kufukua mwili basi yanapaswa kuwa maombi mengine na kuiomba mahakama iwape siku 14 ili wajibu maombi yale ya awali.

Wakili Njau alisema kuna uwezekano wa wao kuleta maombi mengine ambapo mwenyekiti huyo aliwaeleza kuwa wako huru kupeleka maombi hayo na kesi hiyo sasa itatajwa Aprili 6, 2020.

Katika maombi hayo, Frank alitaka Acley azuiwe kumzika marehemu katika eneo alikozikwa, akidai ni lake, jambo ambalo limepingwa na mjibu maombi
 
Hivi kinachosababisha watu kugombea maiti ni kitu gani?

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
 
Urithi

Jr
Chief naamini kila familia ina warithi wake na namna ya kugawa hiyo mirathi ikiwa ni kisheria (kidini) sasa linapokuja swala la kugombea kumzika maiti hii ndio inashangaza badala ya wanafamilia kushikamana ili kuzika mpendwa wao kwanini wanaparaganyika? Kwani kumzika marehemu ndio kuchukua urithi kutoka kwake? (Kwa mtazamo wangu mdogo nilionao. Utagombea kumzika marehemu iwapo tu ameacha wasia kuwa azikwe sehemu fulani na sio vinginevyo).

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
 
Chief naamini kila familia ina warithi wake na namna ya kugawa hiyo mirathi ikiwa ni kisheria (kidini) sasa linapokuja swala la kugombea kumzika maiti hii ndio inashangaza badala ya wanafamilia kushikamana ili kuzika mpendwa wao kwanini wanaparaganyika? Kwani kumzika marehemu ndio kuchukua urithi kutoka kwake? (Kwa mtazamo wangu mdogo nilionao. Utagombea kumzika marehemu iwapo tu ameacha wasia kuwa azikwe sehemu fulani na sio vinginevyo).

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
Eneo lenye kaburi lina changamoto wakati wa kuliuza!
 
Wapi maiti imegombewa.?
Sorry! Sio kugombea maiti kwa moja kwa moja bali mmoja anataka izikwe hapo ilipozikwa wakati mwengine hataki izikwe hapo ilipozikwa.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
 
Back
Top Bottom