Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,203
- 157,369
Kisa Cha DC Jenerali Ulimwengu Na RC Mary Chipungahelo ' Mary Chips'-
Ndugu zangu,
Hoja hii imeibuliwa na Mjumbe wangu Rose-Chiku Rukkiyah mapema leo asubuhi. Niliahidi kuleta jukwaani kisa hiki.
Jenerali Ulimwengu alikuwa DC wa Ilala enzi za Utawala wa Mzee Mwinyi. RC wa Dar es Salaam aliitwa Mary Chipungahelo maarufu kama ' Mary Chips'.
Yumkini wengi wa wajumbe wangu hapa mlikuwa ama hamjazaliwa, au wadogo sana.
Tulikuwepo mtakumbuka, kuwa mwaka 1987 pale Viwanja vya Mnazi Mmoja ilizuka mijadala ya kidini iliyoelekea kwenye wahubiri kukashifu dini za wenzao.
Tunayakumbuka majina kama Sheikh Ngariba Mussa Fundi akiwa na wenzake Kawemba Ahmed Kawemba na Othman Matata. Wawili wa mwanzo walikuwa na asili ya Kigoma wakati Othman Matata alikuwa Mtangazaji RTD. ( Bila shaka alikuwa na undugu na Chama Omar Matata wa BBC).
DC wa Ilala, Jenerali Ulimwengu, ambaye mahali ilipofanyika mihadhara hii ilikuwa ndani ya himaya yake, aliona hatari iliyokuwa inakuja mbele.
Kwamba watu wa imani tofauti wanaweza kuanza kugombana. DC Ulimwengu akapiga marufuku mihadhara ile na kuwataka wahubiri wakahubiri kwenye nyumba zao za ibada.
RC wa Dar Es Salaam, Mary Chips, akatengua katazo hilo.
Ni nani Mary Chipungahelo?
RC Mary Chips alikuwa mtoto wa mjini haswa. Kazaliwa Manzese na kakulia mjini. Alikotoka Manzese paliitwa 'Manzese Kwa Mama Mere' . Mama yake aliendesha biashara ya bar. Iliitwa ' Bar ya Kwa Mama Mere'.
Naam, na Mere mwenyewe ndio huyu Mary Chipungahelo, au Mary Chips.
Mary Chipungahelo aliingia front kupingana na DC wake Ulimwengu.
Jenerali Ulimwengu alikuwa DC wa kufuata paragraph na kuyaangalia mambo kwa miwani ya Kisosholojia. Ni Sayansi inayohusu mahusiano ya wanadamu.
Hata nikatafakari leo, ni dhahiri Jenerali Ulimwengu alikuwa sahihi. Na bado naamini, kuwa migongano iliyokuja kukua ya wahubiri kukashifu dini za wengine kosa lake lilianzia kwa RC Mary Chips kutengua zuio la DC Jenerali Ulimwengu.
Andiko kutoka kwenye Facebook wall ya Maggid Mjengwa.