Mtifuano jimbo la Ukonga Makonda Vs Waitara. Mjumbe amtuhumu Waitara kumhonga bia ili asizungumzie maendeleo jimboni

Wananchi wa jimbo la ukonga wameanza kuchoshwa na aina ya uwakilishi wa mbunge wao Mwita Waitara baada ya kumshitaki kwa rc wa mkoa wa dsm Paul Makonda.

Wamedai Waitara amekuwa akishindwa kufuatilia kero zao na badala yake anashinda vilabuni anakunywa pombe.

Waitara awajia juu na kusema kuwa hizo ni mbinu chafu za kutaka kumfukuza kwenye jimbo hili ambalo kimkakati anatarajiwa kugombea mmoja wa wakuu wa mkoa mmoja maarufu hapa nchini.
Amakweli malipo ya usaliti ni hapa hapa duniani.
20191008_145340.jpeg
 
Njaa ndugu yangu!

Hata Makonda alishasema kinachomsumbua ni njaaa.

We ulidhani njaa anayo makonda peke yake??

Hata waitara licha ya kwamba ni m binge na waziri,bado ana njaa mbaya.

Tena njaa yake bora hata ya makonda,njaa yake imemjaa kichwani mkurya yule
 
Hata wale wasaliti wenzake nao wana wakati mgumu sana wa kuwashawishi wenye chama chao, kuwapa nafasi nyingine.

Ni bora mara mia wakatumia vizuri mafao yao watakayolipwa baada ya kuvunjwa kwa bunge hapo mwakani.
 
Yeye kama nani hadi apewe taarifa na rais wa mkoa. Anapaswa kujua ratiba za mambo yanayojiri jimboni kwake.

Kama wote wamemficha aanze kujipanga bado mapema dalili za mawingu hizo..
Sasa kwa nini rais asiingilie akamuonya makonda kuhusu kwenda jimboni kwa waitara bila kumjulisha, lakini hapo na mimi nime note point, ukiona kiongozi wa serikali anakuja eneo lako la kazi bila kukujulisha wewe either uwe mbunge ama diwani ujue wazi kwamba haukubaliki kwake, nami natamani wakamtosa ili ajue faida za kuwatelekeza wapiga kura wake waliomchagua kwa tiketi ya chadema, au anadhani alikuwa peke yake ??!!
 
Hata wale wasaliti wenzake nao wana wakati mgumu sana wa kuwashawishi wenye chama chao, kuwapa nafasi nyingine.

Ni bora mara mia wakatumia vizuri mafao yao watakayolipwa baada ya kuvunjwa kwa bunge hapo mwakani.
Kweli, subiri tuone watakavyotoswa mwakani, au magufuli ataingilia kati atoe amri kwamba wote waliotoka upinzani lazima waendelee na nafasi zao ??
 
Kweli sisi wana Ukonga hatumtaki Waitara tunataka Makonda.

Tuna imani na Makonda.
Makonda kama anawania kugombea ubunge DSM, akagombee jimbo la Mnyika au lile la Halima Mdee. Au ana waogopa hao? Hilo la Ukonga tayari lilishakombolewa. Kama ana ubavu akakomboe moja ya majimbo ya DSM ambayo bado hayajakombolewa. Halafu kumlaumu kada mwenzako kwamba hajajenga barabara, kwani barabara si zinajengwa na JPM? Mbunge ana uwezo gani wa kujenga barabara? Si ni kumwonea tu? Makonda akagombee ubunge kwao Kolomije kwa Kitwanga au kama ni DSM basi akapambane na Halima au Mnyika au Kubenea.
 
Mbunge gani barabara za jimboni kwake zote mbovu. Kama Buza kuna lami alafu kitunda, kivule kuna mahandaki tuseme tuna viongozi jimboni?
 
Tuliambiwa wameunga mkono juhudi kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi. Wamefika huko wamepewa madaraka wameanza kubweteka na kutuambia tunywe bia tuache kuhoji maendeleo waliyotuahidi.

Wanafanya hivi kwa sababu wameakikishiwa kuwa kura zetu siyo muhimu kwani zinaweza kubadilishwa na tume na vyombo. Japo tume na vyombo vyaweza kujipangia Nani achaguliwe lakini hatukustahiki kuambiwa tunywe pombe barabara siyo kitu.

Lakini kunywa pombe hatukuanza kunyweshwa leo, kila uchaguzi ukikaribia tunapigwa pombe, Ela ya nauli na t-shirt...Ila waliokuwa wanatunywesha walijua kula na kipofu Sasa hivi wamejengewa kiburi KUNYWA POMBE.

CCM mmetudharau sana ila poa IPO siku tutakuwa na uwezo wa kuchagua tumtakae na kumwondoa tusiyemtaka.

Kunywa pombe bila kujali imani yetu, kwamba tunywe bia kweli? Fedhea
 
"Mbunge wetu (Mwita Waitara-Ukonga) hatoshi, japo yupo CCM na ana wadhifa mkubwa. Nilikutana naye Dodoma nikamuuliza kuhusu barabara, alichofanya alininunulia bia halafu akaniambia, we kunywa bia, mambo ya barabara yatakusaidia nini."- Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam.

-
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, amedai wananchi waliomlalamikia RC wa DSM Paul Makonda, kuwa ametelekeza jimbo lake, na kumtaka Makonda kugombea Ubunge jimbo hilo, amekiita ni hujuma na kilipangwa. Amesema Makonda angemshirikisha wakati anafanya ziara jimboni kwake.

Wee kunywa Bia, barabara itakusaidia nini bnana??
 
Namaanisha hata akikatwa ndani ya CCM atakuwa hajapoteza chochote maana hata angekuwa CDM hiyo 2020 chama kisingempitisha kutokana na kutokuelewana na Mbowe na alikuwa ameambiwa kabisa asahau ubunge.
Nimekupata mkuu
 
"Mbunge wetu (Mwita Waitara-Ukonga) hatoshi, japo yupo CCM na ana wadhifa mkubwa. Nilikutana naye Dodoma nikamuuliza kuhusu barabara, alichofanya alininunulia bia halafu akaniambia, we kunywa bia, mambo ya barabara yatakusaidia nini."- Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam.

-
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, amedai wananchi waliomlalamikia RC wa DSM Paul Makonda, kuwa ametelekeza jimbo lake, na kumtaka Makonda kugombea Ubunge jimbo hilo, amekiita ni hujuma na kilipangwa. Amesema Makonda angemshirikisha wakati anafanya ziara jimboni kwake.


Wacha ' waparurane ' na ikibidi hata ' wauwane ' tu na Kwetu Sisi itakuwa ni furaha kwani wote wawili sioni uwajibikaji wao.
 
Ushirikishwe ili ujipange,mwendo ni mshtukizwe hivyo hivyo hadi akili ziwakae sawa
 
Back
Top Bottom