Uchaguzi 2020 Mtia nia Udiwani CCM adondosha kibuyu chenye dawa

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mgombea udiwani katika Kata ya Sungwizi Tarafa ya Simbo wilayani Igunga mkoani Tabora, Katambi Sospeter amejikuta katika wakati mgumu baada ya kudodosha kibuyu cha dawa za kienyeji alipokuwa akiingia kwenye ukumbi wa kupigia kura za maoni katika Shule ya Msingi Sungwizi.

Tukio hilo limetokea Julai 25, 2020 muda wa saa 5:38 asubuhi ambapo mgombea huyo wakati akijaribu kupanda ngazi ili kuingia katika jengo hilo kibuyu hicho chenye dawa kilidondoka kwa bahati mbaya kutoka kwenye mfuko wake wa suruali mbele ya wajumbe.

Wajumbe wa mkutano huo walipoona tukio hilo walimwambia kuwa ameangusha kifaa chake ambapo alishikwa na bumbuwazi na mmoja wa wajumbe hao Therezia Bleki alikiokota na kumkabidhi ambapo askari mgambo wawili waliokuwa wakilinda eneo hilo walimtoa nje ili kumhoji.

Sospeter alikiri kuwa kibuyu hicho ni cha kwake na kuongeza kuwa kwenye familia yao wamezaliwa mapacha hivyo kiutaratibu wanatakiwa kutembea na kibuyu cha dawa wakati wote.

Aidha, alipotakiwa kukikabidhi kwa walinzi (mgambo) ili asiingie nacho ukumbini aligoma, na baada ya majadiliano yaliyochukua takribani dakika 30 bila mafanikio mgombea huyo aliwatoa pembeni mgambo hao pamoja na mwandishi wa habari na kuomba wamruhusu aingie nacho kwa ahadi ya kuwapatia fedha kidogo.

“Ndugu zangu naomba mniache niingie na kibuyu changu nitawapatia chochote, haya ni maisha tu ndugu zangu,” amesema.
Aidha, baada ya juhudi zake kugonga mwamba aliamua kukipeleka nyumbani na kurudi kupiga kura za maoni.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Sungwizi, Emmanuel Mpya alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alionesha kushangazwa na mgombea huyo huku akibainisha kuwa ni kutokujiamini tu, huku akimtaka kutorudia tabia hiyo.

Baada ya sakata hilo zoezi la upigaji kura liliendelea ambapo Njeri Ibrahim alipata kura 21, Katambi Sospeter kura 22 huku diwani aliyemaliza muda wake Matikito Gaspar akiibuka kidedea kwa kura 62.

Chanzo - TimesMajira Online
 
Jisaidie na ww utasaidiwa, acha kila mtu atumie kile anachokiamin.
 
Kitu cha kufurahisha hapa mgombea hakuweza kusahau silaha kuu ya CCM inayowapatia ushindi kwa kujaribu kuwahonga mgambo ili wamuruhusu kuingia na kibuyu chake.
 
Mmoja wa wagombea wa Udiwani Kata ya Sungwizi, Katambi Sospeter aliagusha kibuyu chenye dawa za kienyeji wakati akiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa kura za maoni za CCM.

Tukio hilo lilitokea wakati mgombea huyo alipokuwa akiingia kwenye jengo la ukumbi wa mikutano, ndipo kibuyu hicho kilipochomoka kutoka kwenye mfuko wa suruali mbele ya wajumbe wa mkutano huo.

Mgombea Katambi alikiri kibuyu ni cha kwake huku akisema yeye amezaliwa mapacha hivyo utaratibu inatakiwa awe na kibuyu cha dawa wakati wote.

“Jamani ndugu zangu mgambo na wewe mwandishi wa habari naomba mniache mimi niingie na kibuyu changu, ngoja niwape fedha kidogo za maji na vocha haya ni maisha ndugu zangu,” alisema mgombea Katambi.

Aidha pamoja na maombi hayo mgambo waligoma kupokea fedha baadaye Katambi aliamua kukipeleka kibuyu hicho nyumbani na kurudi kupiga kura za maoni.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Sungwizi, Emmanuel Mpya alithibitisha mgombea huyo kuangusha kibuyu cha dawa kabla hajaingia kupiga kura.
 
Back
Top Bottom