Uchaguzi 2020 Mtia nia Udiwani CCM adondosha kibuyu chenye dawa

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mgombea udiwani katika Kata ya Sungwizi Tarafa ya Simbo wilayani Igunga mkoani Tabora, Katambi Sospeter amejikuta katika wakati mgumu baada ya kudodosha kibuyu cha dawa za kienyeji alipokuwa akiingia kwenye ukumbi wa kupigia kura za maoni katika Shule ya Msingi Sungwizi.

Tukio hilo limetokea Julai 25, 2020 muda wa saa 5:38 asubuhi ambapo mgombea huyo wakati akijaribu kupanda ngazi ili kuingia katika jengo hilo kibuyu hicho chenye dawa kilidondoka kwa bahati mbaya kutoka kwenye mfuko wake wa suruali mbele ya wajumbe.

Wajumbe wa mkutano huo walipoona tukio hilo walimwambia kuwa ameangusha kifaa chake ambapo alishikwa na bumbuwazi na mmoja wa wajumbe hao Therezia Bleki alikiokota na kumkabidhi ambapo askari mgambo wawili waliokuwa wakilinda eneo hilo walimtoa nje ili kumhoji.

Sospeter alikiri kuwa kibuyu hicho ni cha kwake na kuongeza kuwa kwenye familia yao wamezaliwa mapacha hivyo kiutaratibu wanatakiwa kutembea na kibuyu cha dawa wakati wote.

Aidha, alipotakiwa kukikabidhi kwa walinzi (mgambo) ili asiingie nacho ukumbini aligoma, na baada ya majadiliano yaliyochukua takribani dakika 30 bila mafanikio mgombea huyo aliwatoa pembeni mgambo hao pamoja na mwandishi wa habari na kuomba wamruhusu aingie nacho kwa ahadi ya kuwapatia fedha kidogo.

“Ndugu zangu naomba mniache niingie na kibuyu changu nitawapatia chochote, haya ni maisha tu ndugu zangu,” amesema.
Aidha, baada ya juhudi zake kugonga mwamba aliamua kukipeleka nyumbani na kurudi kupiga kura za maoni.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Sungwizi, Emmanuel Mpya alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alionesha kushangazwa na mgombea huyo huku akibainisha kuwa ni kutokujiamini tu, huku akimtaka kutorudia tabia hiyo.

Baada ya sakata hilo zoezi la upigaji kura liliendelea ambapo Njeri Ibrahim alipata kura 21, Katambi Sospeter kura 22 huku diwani aliyemaliza muda wake Matikito Gaspar akiibuka kidedea kwa kura 62.

Chanzo - TimesMajira Online
Hawa akina Katambi mbona wachawi sana ! kuna mmoja alipewa cheo bila hata kufikiriwa , ila tunashukuru kajitumbua mwenyewe
 
Hii stori mbona kama imekaa kama vile ni ya kutunga tu? Anway suali muhimu hapa ni hili, jee kutumia uganga katika uchaguzi ni marufuku? Ikiwa si marufuku basi kwa nini askari wa mgambo walimzuia kuingiaukumbini?

Tuangalie suali hili kwa mtazamo huu:- kuna wagombea wanakwenda katika sehemu zao za ibada kuomba kwa wanaemuabudu wapate ushindi, si na hawa waabudu mizimu nao waachiwe wafanye maombi yao? Im just thinking out loud!
 
Huko ni kujibainisha kwa wenye chama chao kuwa sisi tunashinda kwa kutumia vibuyu, bila vibuyu tunazimwa kweupe.

Aibu sana kwa CCM maana huyo ni kiwakilishi tu kuwa hayo ndo wanayofanya chaguzi zote kuanzia udiwani/ubunge/urais.
 
Mbele ya wajumbe,kibuyu lazima kidondoke...wamejidhatiti,,LOL
IMG-20200726-WA0065.jpg

Jr
 
Back
Top Bottom