Uchaguzi 2020 Mtia nia aliyeongoza Udiwani CCM achukua fomu bila kusubiri idhini ya chama

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Wapo wana CCM wanaojiamini na ambao hawapo tayari kuendelea kusubiri majina ya mfukoni yanayochakatwa na viongozi wao.

Mkoani Kigoma Jimbo la Kigoma Kaskazini kata ya Kagongo, Mgombea Udiwani aitwae Maganga mnano tarehe 15/08/2020 alichukua fomu ya kugombea Udiwani wa kata hiyo kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi huku wanachama wakiwa bado wanasubiri majina kuchakatwa na jina la mgombea wa CCM kurudishwa.

Alioulizwa yeye alisema hiyo ni haki yake Kikatiba na kwa mujibu wa kanuni za CCM na kuwa alishinda kwenye kura za maoni, hivyo haoni sababu ya kuendelea kusubiri kinachoitwa mchakato.

Ujumbe huu uwafikie mnaochelewesha majina.
 
Back
Top Bottom