Mti wa Xmas wazua simanzi kwa wafanyakazi wa The Guardian Limited

Kampuni ya the Guardian Ltd mbele ya sheria ina utu (personality) na inatakiwa ijitegemee (ijiendeshe). Mmiliki wake hawezi kutoa hela zake za mfukoni kulipia gharama za uendeshaji. Kama inashindwa kujiendesha itakufa yenyewe na Dr. Mengi pamoja na makampuni mengine tofauti yataendelea kudunda tu. No hard feelings, that is business
 
Kama Mengi anadaiwa mishahara, Semvua na wahindi wametajwa wa nini humu?

Hapa kuna majungu tu hakuna zaidi. Kama ni mishahara hakuna asiyejuwa kudai kisheria.
Wew una akili sana, yaani umetoka nje ya box... Hapo kuna zaidi ya madai..

Sisi wabongo ni wachawi kama kawaida yetu
 
kadoda11
usijidanganye kuwa wakitaka kukufahamu wanashindwa,as long as unatumia Simcard yenye jina lako halisi kuingia internent
 
Miezi mitatu pasipo mshahara na bado hakuna kesi mahakamani inayohusu madai ya maslahi???
 
Hapa Naona kuna majungu tu, anaetafutwa ni Semvua tu.

Semvua aliwaajiri nao wafanyakazi au Mengi?

Kama uongo anaufanya Mengi siyo Semvua.

Huo mti na hiyo mishahara ni zuga tu.

Kwa ufataani na majungu haya uliyoyaandika simshangai Mengi kuagiza wafanyakazi kutokana India.

Watanzania badala ya kufanya kazi mmekalia uongo, majungu, ufataani na uvivu tu.

Wahindi wamewashika pabaya mnaona mie na majungu.

Tuondolee huu upuuzi na waliokuunga mkono nawashangaa sana.

Wacha kazi badala ya kuendeleza fitna.
Naomba kujuwa dini ya huyu Semvuwa kwanza.
 
Kwa hiyo marehemu kakosa mshahara akaamua kuanza kuuza nazi....duh mbona ngumu kumeza hiii
 
Mkuu Sokoine, poleni sana!.
Mode naomba mlinde Sokoine, kitendo cha kutoa siri za kampuni humu, akijulikana atapoteza kazi.

Hii taarifa kuwa Kampuni ya Mzee Mengi inadaiwa, ni sawa na Mzee Mengi mwenyewe kudaiwa. Taarifa ya Mzee Mengi, ambaye ndiye tajiri mkubwa Tanzania, kudaiwa na wafanyakazi wake, sio taarifa mzuri kabisa, hivyo mimi nakubaliana na mtoa mada kuwa Mzee Mengi mwenyewe hajui kuwa wafanyakazi wake wa the Guardian Ltd, hawajalipwa mishahara ya miezi mitatu, hivyo kwa taarifa hii sasa, habari ndio zitamfikia, atachota akiba yake na kulipa hiyo mshahara, kati ya kesho na Ijumaa watalipwa.

Poleni sana
P.
 
Mengi anahusikaje na wafanyakazi wa Gurdian kukosa mishahara?
nilivyoona mimi ni kwamba hiyo kampuni ni ya mengi sasa kwanini asihusike na mshahara ila inabidi atuambie alikosa mameneja wazawa mpaka awachukue hao wahindi huo sio uzalendo kabisa ajitafakari watu wetu wanateseka
 
nilivyoona mimi ni kwamba hiyo kampuni ni ya mengi sasa kwanini asihusike na mshahara ila inabidi atuambie alikosa mameneja wazawa mpaka awachukue hao wahindi huo sio uzalendo kabisa ajitafakari watu wetu wanateseka
"Watu wetu" wanajitesa wenyewe, ni wezi, waongo, mafataani.

Ushahidi wa hayo unajidhihirisha wazi kabisa kwenye post namba moja.
 
Magazeti kwa sasa yanapitia kipindi kigumu sana kwani wanunuzi ni wazee tu tena wasio na smartphone!
Technology ina + na- zake magazeti kwa sasa online unaweza kuyasoma yote kwa MB10 .
 
Mkuu embu fikilia kidigo tu kwa elimu ya msingi Mimi Niko kwenye upande wa production sales na marketing zinanihusu vipi wakati mkataba unataka nilipwe siku nilizofanyia kazi
WASIPOUZA UTALIPWAJE ? hiyo karatasi ya mkataba itakulipa ?
Kwanza kabisa unapaswa kujua mnyororo mzima wa thamani wa kazi/kampuni yako, mfano mkulima wa karanga lazima ajue fika, wadau wote wa shamba lake ni wakina nani, aanze na mbegu bora, rutuba, majira, hadi kuvuna haitoshi mpaka soko la karanga, bado mpaka bei na kulipwa hadi AFIKIE MALENGO YAKE.

Mesenja/mfagiaji ofisini kwako anapaswa kujua yupo kwa sababu anauza gazeti kiasi fulani, na gharama zipo ni pamoja na karatasi ,mishahara n.k sio kwa sababu ana mkataba ? sheria za kazi ?

WAELEVU(smart people, Intrapreneurs-wajasiriakazi) hawalipwi tokana na sheria /mkataba wanalipwa tokana na uzalishaji/anachozalisha (per value added) hii ndio itakayo mhakikishia mapato/mavuno yake na kwa muda mrefu, ni wabunifu, wanajiongeza sana kuboresha, hakubali kushindwa, mfumo mzima wa kampuni au kazi anajitahidi kuuelewa.

WATUMWA ndio wana asili ya kulipwa kwa mkataba/sharia za nchi anadai hata kama hakuzalisha na hana haja ya kujua mnyororo wa thaman wa kazi yake hata akielezwa hatajua, anasubiri nyampala amtume akimaliza hiyo kazi anakinga mkono. Hakuna ubunifu wala kujiongeza, hakuna haja ya tija walalamishi sana sababu hajui root cause ya tatizo.

Kwa taarifa tu TANZANIA wengi tulionao ni WATUMWA sio WAFANYAKAZI.

SAMAHANI SANA KAMA NTAKUWA NIMEKUUDHI SIO LENGO LANGU.
 
Back
Top Bottom