Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania

Kwa tathmini tu hata tukibadilishana nchi na marekani sie tupewe nchi yao wao waje bongo kujipanga after 10-20 years tutaanza tena kutegemea misaada kutoka Tanzania.

Shithole country as charged!
 
Habari wakuu,
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Bayreuth wamegundua kuwa mti uliopo kwenye mlima Kilimanjaro ni mrefu zaidi barani Afrika ukiwa na urefu wa mita 81.5. Miti 10 mirefu zaidi barani iliyopimwa tangu mwaka 2012 ina urefu kati ya mita 59.2 na 81.5 na upana wa mita 0.98 mpaka 2.55.

Kwa kawaida miti mirefu zaidi duniani huwa haipatikani barani Afrika.

entandrophragma_flm4_2_13-0001.jpg


=======
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.

Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.

Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.

Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.

Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani.

Chanzo: BBC
Kilimanjaro kwa vitu virefu hamjambo
 
wataongea nn akat mpk walipofka waliunga unga tu
Wanasanyansi wa Tanzania hamna kitu kwanza hawajui English ya kuongea! na hawajawahi Gundua chochote kile. haswa hawa wa Awamu hii wanapewa vyeo alafu wanaboronga ''kweli kweli'' karibu wote hawajui hata nzi ana miguu mingapi! ukiachia Jongoo...

@military_Genius
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom