Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania

Mkoa wa Kilimanjaro uliopo kaskazini mwa Tanzania, ni maarufu kwa shughuli za utalii. Kila mwaka watalii huja kwa lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro. Lakini hivi sasa, watalii wamepata kivutio chengine mkoani humo. Hii ni baada ya serikali ya Tanzania kutangaza kuwepo kwa mti mrefu zaidi barani Afrika.Mti huu aina ya Mkukusu una urefu wa mita 81.5 na unaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).

Ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Dk. Andreas Hemps na mkewe wote kutoka nchini Ujerumani ndio waliobaini kuwepo kwa mti huo umbali wa mita 1600 kutoka usawa wa bahari baada ya utafiti uliohusisha nchi nyengine barani Afrika kwa kipindi cha miaka mitano.

"Nimefika hapa ilikuwa Krismasi mwaka 1996 na nimeingia kufanya utafiti wa msitu. Nimeona miti hii na kusema hii ni kitu kikubwa lakini nilikuwa sijajua kama ni mita 80. Natumia leza skana. Napima mara tatu halafu ndio napata urefu kamili. Wageni wengi watafika hapo kushuhudia mti huu, pamoja na watafiti vilevile. Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro pia nayo imeanza kuangalia mazingira haya ili yasiharibiwe," Dk. Andreas Hemps amemweleza mwandishi wa BBC Aboubakar Famau.

Licha ya mti huu kuwa kivutio ambacho kinaweza kuiingizia serikali fedha za kigeni, lakini changamoto iliopo ni ugumu wa kuufikia mti huo.

Ili kufika katika eneo la Mrusungu ambapo ndipo ulipo mti huo mrefu zaidi, ni safari ya kutembea kwa mguu kwa takriban muda wa saa nne kwenda na kurudi kwa kupita katika milima, mabonde, mito na makorongo.

Kazi iliyofanywa na watafiti hao, inaonekana kuupa heshima mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa jumla na mti huo utaongeza chachu ya watalii kupanda Mlima Kilimanjaro na wengine kwenda kushuhudia mti huo.

Kwa upande wake, Charles Ngendo ambae ni mhifadhi wa utalii katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro amesema hifadhi inatarajia kuboresha miundombinu ya kufika katika mti huo ili kuwawezesha watalii kwenda kwani miundombinu ya sasa hivi sio rafiki kwa utalii.

"Niseme tu kwamba Kinapa tutaweka mikakati ya kuhakikisha kwamba eneo hili linaendelezwa ili liwe sehemu ya utalii katika hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro. Tutaweka katika bajeti zetu za hifadhi kuhakikisha kwamba tunaboresha miundombinu. Kama unavyoona mahala hapo kuna makorongo, kuna miinuko. Na ili paweze kufikika lazima kuwe na miundombinu. Kwa mfano tutaweza madaraja baadhi ya maeneo," ameeleza Charles Ngendo.

Mti huo wenye umri wa zaidi ya miaka 600 hivi sasa uko chini ya ulinzi wa KINAPA ili kuulinda kutokana na majangili na hata wale wanaotaka kuutumia kama dawa. Mti huo tayari umeingizwa katika rekodi ya dunia kwa kushika nafasi ya sita kwa urefu duniani.

Utafiti wa kuwepo kwa mti huo tayari umewekwa katika mitandao na vituo vya utalii katika nchi mbalimbali duniani, ili kuleta changamoto ya utafiti mwengine utakaoweza kuonesha mti mwengine mrefu katika nchi nyengine yoyote Barani Afrika.

BBC SWAHILI
 
Bila kapicha ka mti huo Mimi ntaendelea kuongoza kambi ya kina Thomaso Wa JF (JF non-believers)
Hata kama habari hiyo imeletwa na BBC
 
KASKAZINI Mashariki mwa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kuna mti mrefu kuliko yote Afrika. Mti huo wenye kilometa 81.5 unapatikana katika moja ya bonde la mlima huo.
Kulingana na utafiti uliofanywa na mwanazuoni Adreas Hemps toka Chuo kikuu Bayreuth nchini Ujerumani akinukuliwa na jarida la Biodeversity and Conservation ambalo limeeleza kuwa Andreas aligundua mti huo miaka 20 iliyopita katika hifadhi hiyo na baadaye kati ya mwaka 2012 na 2016 alikuja na wataalamu wenzake na kuupima urefu wake ambapo kutokana na vipimo hivyo walikadiria umri wa mti huo ni kuanzia miaka 500 hadi 600.
Mti huo unaojulikana kwa jina la Colossus umevunja rekodi ya dunia kwa urefu wake na uliwahi kufananishwa na mti aina ya Sydney uliopo Limpopo Afrika Kusini ambao ulikufa mwaka 2006.Pia fahamu kuwa mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu zaidi duniani kwa milima isiyo na safu na una kilele chenye mita 5895 kutoka usawa wa bahari ukiwa na vilele maarufu vya Kibo na Mawenzi.
 
The tallest trees in the world are redwoods (Sequoia sempervirens), which tower above the ground in California. These trees can easily reach heights of 300 feet (91 meters).

Among the redwoods, a tree named Hyperion dwarfs them all. The tree was discovered in 2006, and is 379.7 feet (115.7 m)
 
KASKAZINI Mashariki mwa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kuna mti mrefu kuliko yote Afrika. Mti huo wenye kilometa 81.5 unapatikana katika moja ya bonde la mlima huo.
Kulingana na utafiti uliofanywa na mwanazuoni Adreas Hemps toka Chuo kikuu Bayreuth nchini Ujerumani akinukuliwa na jarida la Biodeversity and Conservation ambalo limeeleza kuwa Andreas aligundua mti huo miaka 20 iliyopita katika hifadhi hiyo na baadaye kati ya mwaka 2012 na 2016 alikuja na wataalamu wenzake na kuupima urefu wake ambapo kutokana na vipimo hivyo walikadiria umri wa mti huo ni kuanzia miaka 500 hadi 600.
Mti huo unaojulikana kwa jina la Colossus umevunja rekodi ya dunia kwa urefu wake na uliwahi kufananishwa na mti aina ya Sydney uliopo Limpopo Afrika Kusini ambao ulikufa mwaka 2006.Pia fahamu kuwa mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu zaidi duniani kwa milima isiyo na safu na una kilele chenye mita 5895 kutoka usawa wa bahari ukiwa na vilele maarufu vya Kibo na Mawenzi.
Unajua maana ya kilomita lakini? Vipimo uko vyema kweli?
 
Duu mpka waje wadhungu yule waziri mwenye dhamana kashinda Twitter kubishanaaa upuuuzi
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom