Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Habari wakuu,

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Bayreuth wamegundua kuwa mti uliopo kwenye mlima Kilimanjaro ni mrefu zaidi barani Afrika ukiwa na urefu wa mita 81.5. Miti 10 mirefu zaidi barani iliyopimwa tangu mwaka 2012 ina urefu kati ya mita 59.2 na 81.5 na upana wa mita 0.98 mpaka 2.55.

Kwa kawaida miti mirefu zaidi duniani huwa haipatikani barani Afrika.

entandrophragma_flm4_2_13-0001.jpg

=======
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.

Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.

Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.

Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.

Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani.

Chanzo: BBC
 
Wapendwa wadau..tungependa kuweka picha lakini mti hauenei kwenye camera..una MB nyingi!

Asanteni.

Ukizingatia kila ununuapo muda wa maongezi au kifushi unapigwa VAT .
Kila wakipiga picha, inaandika to be continued....camera za smartphone zinaonyesha wait for part 2
 
Ndo sifa pekee nchi hii tunazoweza kuwa nazo... ni God Made na ukikuta sifa ambayo ni MAN MADE basi ni sifa mbaya! Afadhali, hata ukiwa US, huwezi kutaja giant players kwa kizazi hiki bila kumtaja Hasheem Thabeet! Hii nayo, ni kwa fadhila za Jalal!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom