game over
JF-Expert Member
- Jan 1, 2016
- 10,388
- 23,300
Tunavyo vingi sana mkuu, vivutio maelfu kwa maelfu, hicho ni kimoja umekiona, hata nikikupeleka kijijini kwetu utaduwaa.Jameni vivutio mnavyo, lakini kujinadi hamnazo. Sasa mtalaumu wajanja wakiutangaza na kupiga hela.
==================================
Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania
Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.
Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.
Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.
Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani.
Mti mrefu zaidi Afrika wagunduliwa Tanzania - BBC Swahili
Relaax,
Our time is coming and we are almost there... Ngoja tumalizie JNIA terminal3, (to be the largest in east and central africa), na tufufue ATCL.
Halafu mtaelewa kwa nini no body can stop reggae.