Mtendaji wa kijiji atuhumiwa kwa ujambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtendaji wa kijiji atuhumiwa kwa ujambazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 28, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MTENDAJI wa kijiji cha Nyamililo wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Charles Lushibika (48), na wenzake watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisikwa tuhuma za kishirikina na majambazi.
  Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtendaji huyo alikamatwa na polisi Desemba 24 mwaka huu majira ya saa 12 baada ya kupata taarifa za kishirikina na majambazi.

  Aliwataja wengine waliokamatwa na mtendaji huyo kuwa ni pamoja na Mayalla Skikoneka ambaye ni mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akiwasafisha majambazi baada ya kufanya uhalifu ili waonekane kuwa ni watu wema, Anastazia Koloneli (30) pamoja na Siwema Julius (18) ambao ni marafiki wa majambazi.

  Alisema kuwa baada ya watu hao kukamatwa walihojiwa na kuonyesha sehemu ambapo silaha zinafichwa ambapo polisi walipokwenda eneo hilo hawakufanikiwa kuzikukutwa.

  Alisema kuwa usiku wa Desemba 23 watu watatu ambao ni miongoni mwa watu watano waliotajwa walikamatwa wakiwa wamepanda pikipiki wakienda eneo la Nyamililo kwa nia ya kuvamia na kwa kuwa wananchi walikuwa wakiwafahamu walianza kuwafukuza na kupiga yowe na kutiwa nguvuni baada ya kupekuliwa walikutwa na bunduki ya SMG.

  “Majambazi hao walikimbia na kuacha mfuko uliokuwa na bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili UA 8353 ukiwa na risasi 20 pamoja na pikipiki yenye namba za usajili T592 BKM ambayo ilichomwa moto na wananchi na hivyo kushindwa kujulikana ni ya aina gani,” alisema.
   
Loading...