Mtendaji wa Kijiji amchapa vibao Mwananchi kisa kuvuta sigara hospitali

Hongera mtendaji kwa kutoa haki ya kumchapa kibao mvutaji huyo. Maana juzi jaji mkuu alisema chombo chochote cha serikali kinatoa haki ingawa mahakama ndio chombo cha mwisho kutoa haki...
 
Sheria zimetungwa kwa ajili ya nini? Unampiga ngumi au kibao mwenzako, km anakisu akakuchoma tumboni utamlaumu?
Hiyo mambo huwa inawakuta wananchi wanyonge tu. Mtu kavuta sigara, ita polisi wamkamate.
Ila kusema ukweli kuna watu mambo wanayofanya natamani niwatandike makofi au viboko....mfano madereva wa bodaboda!
 
Umempiga kibao, anatoa kisu anakuchoma tumboni. Utamlaumu? Cheo chako siyo kigezo cha kuwaonea watu. Sheria zipo. Mm ukijichanga hata ungekuwa raisi wa nchi fulani, utajuta.
safi ni bora ufanye maamuzi hata ukosee kuliko kutokufanya kabisa
 
Sheria zimetungwa kwa ajili ya nini? Unampiga ngumi au kibao mwenzako, km anakisu akakuchoma tumboni utamlaumu?
Hiyo mambo huwa inawakuta wananchi wanyonge tu. Mtu kavuta sigara, ita polisi wamkamate.
Hata wewe sasa hivi natamani nikukate kibao!
 
Kipindi ananipiga hao mabodigadi watakuwa wamenishikilia? Kitendo cha sekunde tu, mtu ameshadhurika. Ushawahi kujitoa mhanga? Dunia hii si kila mtu unaweza kumfanyia kila unachofikiria halafu akakuangalia haijalishi una cheo gani.
Weka akilini hilo.
Rais anao uwezo wa kukuchapa viboko na hufanyi chochote ana mabodigadi

Ukiamsha unaweza kamatwa wakakuchinja kama kuku anavyochinjwaga au mateso makali zaidi

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kipindi ananipiga hao mabodigadi watakuwa wamenishikilia? Kitendo cha sekunde tu, mtu ameshadhurika. Ushawahi kujitoa mhanga? Dunia hii si kila mtu unaweza kumfanyia kila unachofikiria halafu akakuangalia haijalishi una cheo gani.
Weka akilini hilo.
You watch a lot of SMACK DOWN!
 
Kwann ww haujafuata sheria? Dunia hii siyo kila mtu unaweza kumfanyia unachotaka halafu akakuangalia.
Unamkumbuka Ditopile Mzuzuri yule mkuu wa mkoa wa Tabora? Aliishia wapi pamoja na cheo chake?
Unamkumbuka yule jaji aliyekuwa anakula rushwa na kuwabambikia watu kesi mpaka uzi uliletwa humu wa kumtahadhalisha hajirekebishe? Alidhani cheo chake kitamlinda. Aliishia wapi?
Wewe si mfuata sheria?! Kwani usiende kuripoti polisi wanipeleke mahakamani?! Zilongwa mbali zitendwa mbali.
 
Kwann ww haujafuata sheria? Dunia hii siyo kila mtu unaweza kumfanyia unachotaka halafu akakuangalia.
Unamkumbuka Ditopile Mzuzuri yule mkuu wa mkoa wa Tabora? Aliishia wapi pamoja na cheo chake?
Unamkumbuka yule jaji aliyekuwa anakula rushwa na kuwabambikia watu kesi mpaka uzi uliletwa humu wa kumtahadhalisha hajirekebishe? Alidhani cheo chake kitamlinda. Aliishia wapi?
Ha ha ha yaani ungekuwa karibu yangu ningekukata kibao akili ikukae sawa.
 
Utakuta hapo kna kibao cha NO SMOKING lakini bado utakuta mtu anavuta

Ova
 
Hapo nasimama Upande wa Mtendaji, tena hizi habari zinavyozidi kusambaa inabidi huyo aliyevuta Sigara kwenye Umma akamatwe afunguliwe mashtaka nadhan Faini ni 8Mil au Kifungo cha miaka miwili. Hongera sana Mtendaji kwa kuokoa Afya za Wananchi wako dhidi ya taahira mmoja.
 
Mkazi wa kijiji cha Mbwemkuru mkoani Lindi, Athumani Ndumba amelalamika kitendo cha mtendaji wa kijiji hicho, Azidu Mwenda kumpiga makofi hadharani kwa madai ya kuvuta sigara katika kituo cha afya Kitomanga.

Tukio hilo limetokea Januari 31, 2021 katika kituo hicho na kushuhudiwa na waliokuwa wamekwenda kuwajulia hali wagonjwa.

Ndumba ambaye mke wake amelazwa katika kituo hicho amesema alitoka nje kwa ajili ya kuvuta sigara na ndipo alipokumbana na mtendaji huyo.

Amesema wakati akiendelea kuburudika na sigara ndipo alipovamiwa na mtendaji huyo na kupigwa vibao viwili na hakujibu lolote wala kuzusha ugomvi kwa madai kuwa alikwenda kwa ajili ya kumjulia hali mkewe ambaye ni mjamzito.

“Nilipomaliza kuvuta sigara alitokea mtendaji na kutaka kujua aliyekuwa anavuta na nilipojibu alinishambulia kwa kunipiga makofi. Alinipiga la kwanza kabla sijakaa sawa akanipiga la pili. Waliokuwa karibu walimtaka aache kunipiga ndio akaacha,” amesema Ndumba huku Sharifa Rashid aliyeshuhudia tukio hilo akisema kitendo kilichofanywa na mtendaji huyo sio cha kiungwana.

Kwa upande wake Mwenda alikiri kufanya hivyo kwa madai kuwa alipomuuliza Ndumba alikana kuvuta sigara.

"Nilipofika kituo cha afya nikasikia harufu ya sigara na nikamuona Athumani anazimia sigara yake chini nilipomuita akaleta ubishi ndio tukaanza kuvutana" amesema Mwenda.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho, Gidion Edward amesema hajapata taarifa zozote za malalamiko kutoka kwa Ndumba kauli iliyotolewa pia na mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomari Satura.

“Tukio hilo silijui lakini kama limetokea mtu aliyeshambuliwa anatakiwa akaripoti polisi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake,” amesema Satura.

Chanzo: Mwananchi
Safi, angempiga na mtama kabisa
 
Back
Top Bottom