Mtendaji wa Kijiji amchapa vibao Mwananchi kisa kuvuta sigara hospitali

Mamlaka ya kutoa hukumu na adhabu huyo mtendaji anayapata wapi?... Tusiishi Kama ng'ombe huku taratibu na kanuni zipo.

Kuchapana bakora na kupiga watu huu Ni ukoloni wa kidikteta..
Yeye kaenda kuona mgonjwa au kuvuta sigara? Kama anafanya hivyo tena hospital huyo baba hata hako katoto hata kaonea huruma atakuwa anavuta tu katoto kanavuta moshi, unajua moshi unaotolewa ndiyo mbaya kwa wale wanaopokea nje!
 
Kipindi ananipiga hao mabodigadi watakuwa wamenishikilia? Kitendo cha sekunde tu, mtu ameshadhurika. Ushawahi kujitoa mhanga? Dunia hii si kila mtu unaweza kumfanyia kila unachofikiria halafu akakuangalia haijalishi una cheo gani.
Weka akilini hilo.
Kazi za watu hizo mambo ya kufikirika hayo

Ungekuwa una uzoefu na magereza ambako kuna jamaa wana maamuzi kama yako ,kupiga askari n.k huwa wanapigwa rungu mpaka mifupa ya miguu migumu inavunjika licha ya ubishi wao

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Nimeishia hapo akanipiga Kofi la kwanza kabla sijakaa sawa akanipiga Kofi la pili...🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mtendaji sasa nilipomuona akaizima kwa chini halafu alipoulizwa akaanza ubishi, kwahiyo hivyo vibao vilikuwa vyakumkumbusha na alijua kama anafanya kosa ndiyo maana aliizima baada ya kumuona mtendaji
 
Safi.

Wavuta sigara ni watu wasio na akili kabisa, wako kama bata, bata akijisikia kunya hata kwenye sufuria ya ugali anakunya. Mvuta sigara akishikwa kiu popote tu anavuta.

Wanasayansi wanasema wavuta sigara ni binadamu wenye kiwango kidogo sana cha akili.

Wanazingua sana hawa gari moshi
 
Ni kweli kabisa Wavutaji sigara ni watu wasio na akili kabisa maana hata kwenye packet ya sigara kuna maandishi yanasomeka Cigarette smoking is dangerous to your healthy Lakini bado wanavuta hata akili ya kusoma kilichoandikwa hawana!!
Kwenye packet pameandikwa

"Ni salama, ni poa, ni yako"

Onyo: "uvituaji wa sigara ni hatari kwa afya yako"

Lakini hawa mbuzi bado wanavuta
 
Mkazi wa kijiji cha Mbwemkuru mkoani Lindi, Athumani Ndumba amelalamika kitendo cha mtendaji wa kijiji hicho, Azidu Mwenda kumpiga makofi hadharani kwa madai ya kuvuta sigara katika kituo cha afya Kitomanga.

Tukio hilo limetokea Januari 31, 2021 katika kituo hicho na kushuhudiwa na waliokuwa wamekwenda kuwajulia hali wagonjwa.

Ndumba ambaye mke wake amelazwa katika kituo hicho amesema alitoka nje kwa ajili ya kuvuta sigara na ndipo alipokumbana na mtendaji huyo.

Amesema wakati akiendelea kuburudika na sigara ndipo alipovamiwa na mtendaji huyo na kupigwa vibao viwili na hakujibu lolote wala kuzusha ugomvi kwa madai kuwa alikwenda kwa ajili ya kumjulia hali mkewe ambaye ni mjamzito.

“Nilipomaliza kuvuta sigara alitokea mtendaji na kutaka kujua aliyekuwa anavuta na nilipojibu alinishambulia kwa kunipiga makofi. Alinipiga la kwanza kabla sijakaa sawa akanipiga la pili. Waliokuwa karibu walimtaka aache kunipiga ndio akaacha,” amesema Ndumba huku Sharifa Rashid aliyeshuhudia tukio hilo akisema kitendo kilichofanywa na mtendaji huyo sio cha kiungwana.

Kwa upande wake Mwenda alikiri kufanya hivyo kwa madai kuwa alipomuuliza Ndumba alikana kuvuta sigara.

"Nilipofika kituo cha afya nikasikia harufu ya sigara na nikamuona Athumani anazimia sigara yake chini nilipomuita akaleta ubishi ndio tukaanza kuvutana" amesema Mwenda.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho, Gidion Edward amesema hajapata taarifa zozote za malalamiko kutoka kwa Ndumba kauli iliyotolewa pia na mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomari Satura.

“Tukio hilo silijui lakini kama limetokea mtu aliyeshambuliwa anatakiwa akaripoti polisi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake,” amesema Satura.

Chanzo: Mwananchi
Hizi ndio habari za magazeti yaliyobaki.
Tanzania Daima uko wapi utupe habari?
 
Back
Top Bottom