Mtendaji Arumeru akamata Wake wa wanaume wasiolipa mchango

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
577
1,000
Wanaume wa kata ya Olturument katika halmashauri ya Arusha DC,wilayani Arumeru mkoa wa Arusha,wamelazimika kuzikimbia familia zao kukwepa kukamatwa au kuchukuliwa Mali zao baada ya kushindwa kulipa mchango wa lazima wa sh,15000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya sekondari .

Zoezi hilo limelalamikiwa na wakazi wa kata hiyo kwa jinsi mtendaji wa kata hiyo Goodluck Chilya akiwa wameambatana na barozi wa nyumba kumi na Migambo kadhaa ,kuwakamata baada ya kushindwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

Mmoja ya wananchi hao amedai kuwa mtendaji huyo na kikosi chake amekuwa na tabia ya kuwakamata wake zao au msichana wa Kazi na kuondoka nao hadi ofisini kwake ili kushinikiza baba mwenye nyumba aje kumkomboa kwa kutoa kiasi hicho cha fedha

"Mtendaji huyo pindi anapofika kwenye kaya na kumkosa baba mwenye nyumba huamrisha kuondoka na mtu yoyote akiwemo msichana wa Kazi au Mke ili baba mwenye nyumba atakaporejea aje kumkomboa kwa kulipa mchango huo" Alisema mkazi huyo ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa

Pia mtendaji huyo na kikosi chake wanadaiwa kuchukua Mali za wakazi hao yakiwemo magodoro,TV,Radio na samani zingine za ndani na kuondoka nazo kwa maana baba mwenye nyumba atakaporejea aende kukomboa kwa kulipa mchango huo, jambo ambalo linalopingana na agizo la Rais John Magufuli la kutaka wananchi wasinyanyaswe kwa kuchangishwa michango.

Hali hiyo imewalazimu wanaume wengi kuzikimbia familia zao kwa kuogopa kukamatwa ama kuchukuliwa Mali zao za ndani.

Akiongelea suala hilo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Dkt Wilson Mahela alikiri kupokea malalamiko juu ya uendeshaji wa zoezi la kuchangia ujenzi wa madarasa na kumtaka mtendaji wa kata hiyo kumpatia maelezo juu ya uendeshaji wa zoezi hilo.

Alifafanua kuwa wananchi hao kupitia mikutano yao ya hadhara walikubaliana kuchangishana fedha ili kukamilisha ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya sekondari .

Alisema hakubaliani na namna ya uendeshaji wa zoezi hilo kwa kuwa nimekuwa na dosari nyingi wananchi kulalamikia kukamatwa ama kuchukuliwa kwa Mali zao na kusema kuwa linawachafua wao kama viongozi wa halmashauri hiyo na kwamba amemwagiza mtendaji huyo kumpatia maelezo ya kina.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata hiyo,Goodluck Chilya alisema ni kweli amekuwa akiendesha zoezi la kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Alisema walilazimika kufanya msako wa nyumba kwa nyumba katika kitongoji cha Kishori baada ya wananchi wa vitongoji vingine katika kata hiyo kulalamikia wenzao wa Kitongoji hicho kutochangia chochote.

Alisema kuwa wananchi walikubaliana kuchangishana sh,15,000 kwa kila mwanaume na yeye kama mtendaji anatekeleza kukusanya michango hiyo.

"Ni kweli tumekuwa tukiwachukua watu tunaowakuta hapo nyumba na kuondoka nao lakini si kwa kuwapeleka Polisi Bali tunawapeleka ofisini ili watoe maelezo ya ulipaji wa fedha hizo baada ya baba mwenye nyumba kutoonekana" Alisema Chilya

Ends.....Sent using Jamii Forums mobile app
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,400
2,000
Si mnasemaga maendeleo hayana chama
Tufanye Maendeleo bhana
Acheni siasa
 

Diason David

Verified Member
Aug 2, 2018
7,567
1,995
Sijui hili gazeti la wapi hili
IMG-20190217-WA0014.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom