Uchaguzi 2020 Mtemvu kuvuliwa uanachama wa CCM baada ya kujiapiza kuchukua fomu jimbo la Temeke?

Hiyo fomu atapewa na Nani?
Hahaaaa swali zuri sana mkuu.

Fitna zinapigwa nje na ndani. Nimekumbuka wale wa Tanga waliokuwa wanarudisha fomu kufika njiani wakapigwa mkono mtu aliyewasimamisha akachukua fomu akapotea. Wengine wakafika ofisini wakashindwa kujua chumba cha kurudisha hadi muda ukaisha, huu mchezo hautaki hasira inabidi ujipange hasa.
 
Kuna Kipindi niliona watu flani wanaitwa Nyumbu sijui kama kweli Nyumbu ni wale au ni wapi sijaelewa vizuri kutokana na matukio haya meengi ya ajabu ajabu,..Naamini pia kwamba Asilimia 95 ya Viongozi katika nchi hizi za Afrika kizazi cha leo kingetuuza Tusipate uhuru..Hawa wasingepigania Uhuru kabisa ni aibu
 
Habari ndio hiyo wakuu , inasemekana Salim Chicago amekubaliana na mpango wa Polepole ambao kimsingi umo kwenye mkataba wa manunuzi ya wabunge wa upinzani ( tunakununua na tunakurudisha tena ) , Lakini Abass Mtemvu na wapambe wake wakiwemo viongozi wa ccm wa wilaya wamejiapiza kwamba Patachimbika !

nimekuletea hii ili uwe wa kwanza kufahamu .
Mtemvu usikubali katiba yenu kukanyagwa,nina vijana wa KUSHATO jimbo la temeke,nimeongea nao wote wanasema wamechoshwa na mtolea wanataka kukurudisha wewe maana wameona mtolea kawaangusha kwa upuuzi wake,wanasema wapo nyuma yako wanakupa support,wanasema chukua form watakuunga mkono hata kama kina polepole wasipokupitisha,wanasema ukikatwa nenda hata chama kingine watakupigia kura tu.
 
Mtolea atapata uteuzi kwa hati ya dharura kama ulivyokuwa kwa mollel, mtulia, Ole Millya, Gekul, Kalanga nk binafsi nawatakia kila kheri katika safari yao ya kisiasa.
 
Ndo maana ukihama wanakukata mkia ukirejea wanakuwa wanakutambua. Sijui huyu Waitara katoa wapi mkia maana alikuwa ng'ombe na mkia akahama karudi tena.
 
Mtemvu usikubali katiba yenu kukanyagwa,nina vijana wa KUSHATO jimbo la temeke,nimeongea nao wote wanasema wamechoshwa na mtulia wanataka kukurudisha wewe maana wameona mtulia kawaangusha kwa upuuzi wake,wanasema wapo nyuma yako wanakupa support,wanasema chukua form watakuunga mkono hata kama kina polepole wasipokupitisha,wanasema ukikatwa nenda hata chama kingine watakupigia kura tu.
Acha kumdanganya mtemvu! Nakushauri Alhaji mtemvu kama utabahatika ukiona comments yangu! Fuata miongozo ya viongozi wakuu ktk chama kwa kadri watakavyopendekeza na sio vinginevyo! Kama Mtolea atapitishwa ni vyema ukamuunga mkono!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom