Mtemvu ana nia gani kupeleka watanzania Uarabuni

kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,867
2,746
Leo jamaa alitaka kutoa shilingi kwa sababu wizara ya mambo ya nje imezuia watu kwenda Uarabuni kufanyiwa vitendo vya kinyama! Lakini bado anangangania kupeleka watu!

Je ni muuzaji wa watu huyu jamaa!?
 
Ni upumbavu kuwaza kuuza watu wako utumwani (watu wanaopelekwa ni wale wasio na ujuzi muhimu na hivyo uwezekano wa kudhalilishwa kitumwa ni mkubwa).
Angepambana na wageni wasio na ujuzi wala sifa wanachukua ajira za watu wake hapa nchini pamoja na wamachinga na mafisadi wa kigeni wanaotorosha raslimali za wananchi wake ingekuwa faida zaidi.
Kwa watu wenye akili nzuri hiyo ni biashara haramu!
 
Huyu Mtemvu sioni anachokifanya Temeke zaidi ya biashara ya wadada ndio akili yake uwezo wa kufikiri umeishia hapo.
Anafikiri atachaguliwa kwa ukuhadi anaofanya.
 
Hivi, inakuwaje mbunge kabisa anafanya kazi ya kuwatafutia raia wake kazi za uhousegirl dubai? nimemwona mbunge mmoja kwenye luninga mara nyingi, hivi inakuwaje? dubai imesifika kutesa sana wafilipino na wahindi, ni mahali ambapo ni utumwa kabisa. hivi hapo hakuna kosa la jinai hapo wazee? mbona aibu kwa tz na bunge?
 
Unamzungumzia mbunge gani? Mchomvu?

Mchomvu anajishurisha na biashara nyingi sana sio hiyo ya slave trade pekee.
 
Leo jamaa alitaka kutoa shilingi kwa sababu wizara ya mambo ya nje imezuia watu kwenda Uarabuni kufanyiwa vitendo vya kinyama! Lakini bado anangangania kupeleka watu!

Je ni muuzaji wa watu huyu jamaa!?

cha kushangaza WAOMBA KAZI HIZO WANATOKA MAENEO DUNI SANA ! WENGI NI KUTOKA YOMBO DOVYA , TANDIKA MAGURUWE NA MBAGALA KIBURUGWA .
 
Badala kufikiria kuzalisha ajira kwa vijana wanafikiria kuwapeleka utumwani yaani kuna watu wamepewa akili na wengine funza kichwani.
 
Badala kufikiria kuzalisha ajira kwa vijana wanafikiria kuwapeleka utumwani yaani kuna watu wamepewa akili na wengine funza kichwani.

Watu wajue hana nia Nzuri

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom