Mtemi Mirambo VS Mtemi Mkwawa

Wakati Legend Mirambo anapambania uhai wake kwa kulishwa kichwa cha mbwa, Legend MKWAWA alikua anakunywa supu ya mbwa tena supu ya kichwa.

Yote kwa yote nimejifunza kitu kipya, shukrani mlugaluga
Uongo mkubwa!
 
Habari zenu wakuu.

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa wa historia hasa linapokuja suala la uwezo wa Mwafrika kutokupewa sifa zinazotakiwa kama ilivyo kwa hayati J.K. Nyerere na Nelson Mandela. Afrika inaaminishwa Mandela ni zaidi ya Nyerere hiki ni kituko.

Kuna hili pia la Chief Mirambo na chief Mkwawa eti sifa kubwa anapewa Mkwawa ili tumuone ndio shujaa wetu na pia alipambana akashindwa na wazungu. Nadhani wanataka kutujengea mazingira ya kuwasujudia na kuwaogopa. Itawezekanaje uniamnishe shujaa wangu wa kuigwa ni yule aliyepigwa wakati kuna waliopiga?

Baada ya kuifatilia historia ya mtemi Mirambo a.k.a. Napoleon wa Afrika kama alivyojulikana na wazungu nimegundua kuna upotoshaji mkubwa wa historia.

Chief Mkwawa japo naye si haba ila kwa chief Mirambo hatii mguu hata kucha.

Nguvu za jeshi la Mirambo kwa Afrika mashariki alikuwa hana wakumlingasha. Ndiye aliyetawala eneo kubwa kuliko machief wengine. Tabora mpaka Kigoma eneo lake lilipakana na ziwa Tanganyika japo aliona haitoshi akaingia mpaka Burundi akapiga himaya ya Urundi akasambaratisha.

Wakati Mkwawa anasilaha za jadi kabla hajaletewa bunduki moja na Mwarabu, Mirambo alikuwa anatengeneza bunduki yeye mwenyewe na alimiliki jeshi lilikowa na active personnel zaidi ya 10000.

Hapakuwa na cha mzungu wala mwarabu aliyeleta fyoko kwenye himaya yake aliua kama anau panzi tu ikabidi wafate masharti yake kila wanapopita kwenda Zambia na Kongo walimlipa kodi kwa kuikanyaga ardhi yake huna kodi mzigo wote unabaki na kuwa mali yake.
Wafipa walijichanganya hawakumjua vizuri kichwa chake kikoje. Huyu jamaa alikuwa hana masihara kabisaa!

Wazungu baada ya kubanwa sana waliomba nguvu ya jeshi kutoka kwa sultan wa Zanzibar wakimwambia kwamba Napoleon wa Afrika anataka kuiharibu biashara yako kwakuwa ndiye alikuwa mnunuzi mkubwa wa pembe za ndovu na watumwa kutoka Zaire na Zambia.

Sultan akatuma askari 3000 kuja kuongeza nguvu kwa wazungu wakishirikiana na jeshi la snitch wa Mirambo alikuwa anaitwa Chief Mkasiwa. Jamaa walinyoosha mikono sultan akaona anamaliza watu wake akaamuru jeshi lake lililosalia lirudi Zanzibar haraka walikuwa wamebaki 1500 ndio waliokuwa wamesalimika na jeshi la awali la Mtemi Mirambo lililokuwa likiitwa Luga Luga (walugaluga).
Mtemi Mirambo alikuwa na majeshi matatu ambayo aliyapanga kwa ubora kutoka la kwanza hadi la tatu. Jeshi kali kabisa lenye mafunzo na uwezo wa juu kabisa liliitwa Abaoko kama sijakosea herufi.

Sasa Mkwawa aliuza mali zake kwa Mwarabu pembe za ndovu na kuletewa nguo Mirambo hakuuza mali zake bali alichukua za wazungu walizokuwa wamekusanya sehemu mbalimbali.

Mirambo alichukua watumwa kutoka mikononi mwa wazungu na waarabu na kuwasajili kwenye jeshi lake. Yaani unapomtaja Mirambo jua unataja habari kubwa.

Sasa historia za namna hii zinafichwa na kuoneshwa historia dhaifu ya kumtukuza mzungu kuwa ni bora.

Mtemi Mirambo alifariki kwa ugonjwa wa rovu miaka ya 1880.

Nimeweka hapa kwa kifupi sana. Kwa mwenye interest anaweza kufatilia ahakikishe mwenyewe.

MAGUFULI4LIFE.
Tupe na historia ya Zimbabwe pia.
IMG_20201123_093401.jpg

Sent from my ANE-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Mirambo badooo sana kumuwekea battle na mkwawa. Kwa wasiojua hadi leo kuna medan ya kivita aliitumia mkwawa kijj cha LUGALO kwenye battle na kamanda VON ZELEWSKY, tactic hii inatumiwa na kufundshwa pia na JWTZ.. hadii leo staitaji ni siri za jeshi..So miramboo hakuwaa genious kuliko mkwawa...big no . Japo naweza kukubali geographically mirambo alikuwaa na sehem kubwaa with lillte resistance.
Livingstone na John Speke hawatokuelewa walichokiona.. Mana waarabu walijichanganya wakataka kumvamia wakati alishawaacha aliingia kambi Yao piga watu wote akawaacha wazungu maana hakuwa na beef nao huo wakati
 
Ni kuna mnyamwezi mmoja tu....
Ameamua kulisifu kabila lake ( si vibaya, kama hutobagua wengine).

Mirambo hasimami sehemu moja na Mkwawa kamweee.....
Kama ni kodi kwenye misafara, mkwawa pia alitoza...
Kama ni ujasiri wa Ajabu, Mirambo hatoshi kwa mkwawa.
Ila tujiulize ni lini Mirambo aliwashinda wazungu ( Umesema walimuogopa, Si kweli na kamwe isingewezekana Eti mjerumani Super power wa Dunia amuogope Mirambo).

Uliwahi fikiria Resistance ya miaka nane dhidi ya wazungu ( Resistance ya mkwawa ilikuwa ni 8 yrs).

Si bure wazungu wachukue kichwa chake, wakipeleke makao makuu lazima kuna Namna.

Kwenye eneo lake ( Mirambo) kulikuwa na Chief mwingine pia ( huyo snitch) hii ni ishara kuwa alikuwa weak Sana na alipenda kujitwalia maeneo makubwa yaliyokaliwa na wachovu.
Waangalie wahehe waleo ( itikadi zao) na wanyamwezi, ndio utajua kuwa yupi alikuwa imara.
Hapa naona mnaleta ego kubwa each one alipigana vita yake kwa ustad mkubwa.. Hakuna kiongozi after ukoloni anayeweza kuwafika hata robo ya Hao miamba ya mkwawa na Mirambo hamna aliyebora ya mwenzake wote ni majembe sana
 
Wewe bhana ni ama huifahamu historia ya Mtemi Mirambo au unaifahamu lakini unaamua kuipotosha kwa makusudi kama ilivyo ada yetu!!

Mosi, Machifu/Watemi wengi wa Kiafrika walikuwa ni wafanyabiashara ya Watumwa, na Mtemi Mirambo ni miongoni mwa Watemi ambao walibobea sana kwenye biashara hii!!

Pili, ni kweli Mtemi Mirambo alikuwa very powerful kijeshi na alitumia jeshi lake ku-block route kuu ya Msafara wa Watumwa kutoka Magharibi! Hata hivyo, hakufanya hii blocking kwa sababu alikuwa anapambana na biashara ya utumwa bali alikuwa analinda interests zake dhidi ya Wafanyabiashara wa Kiarabu!!

Umemshusha sana Mkwawa kuhusu uwezo wake kivita compared to Mirambo! Unafanya hivyo huku ukisahau au labda hujui kwamba Mkwawa alikuwa anapambana na Watawala (Wajerumani) wakati Mirambo vita zake nyingi kama sio zote zilikuwa ni dhidi ya Watawala wenzake wa Kiafrika au Wafanyabiashara wa Kiarabu!

Unlike Mkwawa, Mirambo hakuwahi kupigana na madola makubwa ya magharibi kwa sababu mwaka aliokufa ndio huo huo ambao Mabeberu walikutana kumegeana bara letu!!

Kwamba, unlike Mkwawa aliyekuwa na silaha duni kabla hajapewa bunduki moja na Mwarabu huku Mirambo akitengeneza bunduki hizo mwenyewe, hapo unaonesha upotoshaji wako mwingine ama kwa makusudi au kwa kutojua!!

Ukiisoma historia ya Mirambo wala hutachelewa kufahamu Mirambo kapewa sana bunduki na Wafanyabiashara wa Kizungu, na hivyo kuchangia sana kuwa na jeshi lenye nguvu!

Ni kumkosea heshima Mkwawa kudharau uwezo wake simply because alishindwa vita dhidi ya Mjerumani aliyekuwa sio tu Mtawala bali alikuwa na zana za kisasa za Kivita!! Mjerumani ambae hata leo bado ana uwezo wa kututwanga taifa zima let alone a portion of the country!

Aidha, nikukumbushe kwamba, hao ambao umesema "Hapakuwa na Wazungu wa kuleta fyoko"; nikifahamishe tu kwamba, hao hawakuwa Wazungu Watawala bali Wazungu Wafanyabiashara na Mawakala ambao hawakuwa na dola wala jeshi ndani ya ardhi yeu! Na ndio maana hata wewe mwenyewe unakiri kwamba:-
Wazungu baada ya kubanwa sana waliomba nguvu ya jeshi kutoka kwa sultan wa Zanzibar wakimwambia kwamba Napoleon wa Afrika anataka kuiharibu biashara yako kwakuwa ndiye alikuwa mnunuzi mkubwa wa pembe za ndovu na watumwa kutoka Zaire na Zambia.
Huo ni ushahidi tosha kwamba hao Wazungu unaosema hawakuleta fyokofyoko ni Wazungu ambao hawakuwa na jeshi wala dola na ndio maana wakaomba msaada kwa Sultani...

Hawa sio Wazungu aliopambana nao Mkwawa unyemdharau ambae yeye alipambana na Wazungu wenye Jeshi la Kisasa na Dola!!

Mkwawa unayemdharau hakupigana na Wazungu Wafanyabiashara/Mawakala wasio na dola wala jeshi bali alipigana na Wazungu wenye dola na jeshi lenye silaha za kisasa!!

Kwamba,
Bila kufa mapema Chief Mirambo huenda mpaka sasa Afrika mashariki ingekuwa nchi moja.
Kifupi Mirambo alikuwa mpingaji wa biashara ya watu. Mzungu sio tu kulipa kodi kwa wananchi wa Mirambo, alikuwa akifanya fyoo mali zote zinachukuliwa na Mirambo.
Man, sio kwamba tunawasujudia Wazungu lakini uhalisia sio rahisi kama unavyodhani! Kudai kwamba endapo asingekufa mapema huenda bado Afrika Mashariki ingekuwa moja unamaanisha Mirambo angewashinda Wajerumani kivita!!!

Yaani unatuambia Mirambo aliyekuwa anatumia mikuki na pinde angeweza kumshinda Mjerumani ambae hadi anaingia Tanganyika, tayari alikuwa ameshafanya uvumbuzi wa mambo mengi tu huko kwao ikiwa ni pamoja na treni ya umeme?!

Hicho ni kichekesho!

Kwamba eti kuna Mtemi mmoja kutoka Afrika Kusini alitaka kuja kupigana na Mirambo ili achukue himaya yake, hicho ni kiroja kwa sababu hai-make sense Chifu avuke nchi kadhaa zilizopo Kusini mwa Afrika hadi aingine Tanzania ya leo, kisha aendelee kuvuka milima na mabonde hadi central Tanzania eti ili akapigane na Mirambo ili apore Dola la Mirambo!!

Ukweli ni kwamba, Mtemi unayemsema hakutoka South Africa ili kwenda kupambana na Mirambo bali alikuwa ni Kiongozi wa Wangoni ambao mwanzoni walitoka South Africa baada ya kushindwa vita, na hivyo wakatimuliwa!! Kundi la Wangoni lililokuwa linaongozwa na Zwangendaba ndilo lilivuka milima na mabonde na kuingia Tanzania!

Kundi hili liligawanyika, na moja wapo likaongozwa na Mpangalala na ndilo liliingia hadi Kanda ya Ziwa. Kabla ya kuingia Tabora, walianzia Usukumani, na Tabora walianza kupigana na Dola Dogo lililokuwa chini ya Dola ya Unyamwezi!

Dola hili dogolilikuwa chini ya Mtoto wa Chifu Fundikila ambae alikuwa ameolewa na mtoto wa Tippu Tip! Nadhani kwa mara ya kwanza baada ya kushinda vita kadhaa huko nyuma, hapa Wangoni walikula kichapo kichapo, possibly kutokana na huyo Binti kuungwa mkono na Waarabu!!

Baada ya kukimbia Kichapo huko Unyamwezini, ndipo Mpangala na watu wake wakaingia Urambo iliyokuwa inaongozwa na BABA YAKE Mtemi Mirambo na sio Mtemi Mirambo!!! Hapa napo Wangoni wa Mpangala wakachezea kichapo lakini walifanikiwa kutoroka mateka kadhaa including huyo Mirambo ambae by the time alikuwa just a boy!

Aidha, kumbukumbu zinaonesha kwamba, ni hawa Wangoni ndio ambao walimfundisha Mirambo mbinu za Kivita wakati akiwa mateka wao, na ndio maana hata pale Mirambo alipotwaa madaraka, jeshi lake lilikuwa linafahamika kama Warugaruga lenye asili ya Wangoni.

Na hata hiyo unayosema eti hao jamaa walichapwa wakaamua kuomba poo na kuungana nao, kimsingi hawa walikuwa Washirika wenye common interest dhidi ya Waarabu ambao hapo kabla walimsaidia mtoto wa Fundikira kupigana na Wangoni; na ni Waarabu hao hao ambao mara kwa mara walikuwa wanakwaruzana na Mirambo kugombea umiliki wa trading route!
 
Kwahiyo huyo Mirambo chamtoto tu kama alishindwa kumsambaratisha huyo Cheif mwenzake snitch wa Tabora
Wakati amewaelemea na waarabu wa sultan kuamua kurudi tayari chief Mkasiwa alikuwa mikononi mwa Mirambo ila Mirambo haikujulikana kwanini aliamua kumuacha salama. Ila tayari alikuwa kakamatwa kama kuku na wakumsaidia Mkasiwa hakuwepo.

MAGUFULI4LIFE.
 
Umekuza sana story za Mtemi Mirambo.
Jamaa alikuwa mtemi wa kawaida sana, ila alikuwa anajimwambafai kama Magufuli.

Hivi unajua Mirambo ndio mtemi maarufu aliyekuwa akipenda hongo?

Hivi unajua Mtemi Mirambo alikuwa mfanyabiashara maarufu wa watumwa kwa huku bara?

Hivi unajua Mtemi Mirambo alikuwa mtemi aliyekuwa na mikataba mingi zaidi ya kibiashara za kilaghai ambayo alifanya na waarabu, wajerumani.

Kuhusu Mtemi Mkwawa hiyo ni level nyingine kabisa. Misimamo yake isiyoyumba, nidhamu ya askari wake na mbinu za medani za kivita alizokuwa nazo, mpaka leo hii wajerumani wanampigia saluti.

Kama hujui tu, Mkwawa aliwachinja mpaka wamisionari wa kizungu waliofika kwenye himaya yake ambao kiasili walikuwa hawaguswi maana enzi zile walionekana kama wajumbe wa amani (malaika!).
Huyu mkwawa huyu aliyeteka bunduki akazichimbia stop hadi wajerumani waliporudi na kumpiga na kukuta bunduki zao ziko sawa kwa idadi kwa ujinga huo lzm Mirambo Ni zaidi.
 
Wakati amewaelemea na waarabu wa sultan kuamua kurudi tayari chief Mkasiwa alikuwa mikononi mwa Mirambo ila Mirambo haikujulikana kwanini aliamua kumuacha salama. Ila tayari alikuwa kakamatwa kama kuku na wakumsaidia Mkasiwa hakuwepo.

MAGUFULI4LIFE.
Ahahahaha
 
Ngoja niongezee nyama kutoka kwenye maandishi ya Henry Morton Stanley.

Stanley, akiwa katika safari yake ya kwenda Ujiji alipofika Tabora akaambiwa njia ya kwenda Ujiji imefungwa na Chief Milambo baada ya wafanyabiashara wa kiarabu waliokuwa wakiishi unyanyembe kugoma kulipa hongo (kodi) ili kukatiza katika himaya ya Chief Milambo na kuelekea Ujiji.

Basi Chief wa unyanyembe Chief Mkasiwa, waarabu na Stanley wakapanga mkakati wa kwenda kuvamia himaya ya Chief Milambo.

Mapambano yalipopamba moto waarabu wakakimbia wakamwacha Stanley mstari wa mbele...milambo akateka sehemu kubwa ya jeshi la waarabu Stanley na wajakazi wake walifanikiw kutoka. Kwenye kitabu chake aliwalaumu sana waarabu kwa kutomwambia ukweli Juu ya uwezo wa Chief Milambo na Pia aliwatukana sana kwa kitendo cha kukimbia wakati wa mapambano. Hivyo akaamua kuzunguukia Rukwa ili aweze kufika kigoma.
 
Uwezo wa Mowawa sikudhani kama unaweza kubezwa kiasi hiki, Mkwawa alikuwa mtu na akili nyingi sana katika utawala wake, inasemekana Mkwawa angekuwa hai basi kusini mwa Tanzania yote ingekuwa yake.

Isike baada ya kuogopa kupigwa na Mkwawa basi akamtoa binti yake aje kuolewa na Mkwawa ili asishambuliwe na huyo binti alikuwa anaitwa Sekilonge, Mkwawa hakuwa anafanya biashara ya watumwa ila alikuwa anatoza kodi kwa kila mtu anayepita kwenye himaya yake, mpaka hiyo njia ya biashara ya kwrnda Tabora Mkwawa pia alikuwa anaishikiria na ndicho chanzo cha wajerumani kukasilika zaidi. Si hivyo tu mkwawa alikuwa Mwanadiplomasia mzuri maana aliwahi kutuma ujumbe wa kwenda kujadiliana na wajerumani japo wajerumani waliwauwa wajumbe wale. Mkwawa inasemekana katika maongezi yake yeye alisema kabakiza vita moja tu nayo ni ya wamasai
 
Battle ya miaka nane mzee! Vita ya France na Germany (Franco-Prussian war) ilidumu kwa mwaka mmoja tu! (1870-1871). Hata vita za dunia hazikudumu miaka yote hiyo ambayo Mkwawa alimhenyesha mjerumani!

Si bure walitwaa kile kichwa chake wakipeleke kwao.
Yaani ilibidi wachukue kichwa kwa ajili ya uchunguzi... Kwamba huyu jamaa alikuwa Mwafrika halisi au...

For sure, Mkwawa alikuwa mtemi... Salute kwake...

Von Bolowisky si ndo aliuwawaga na huyu mwamba au?
 
Historia ya Mkwawa inajulikana hapo juu. JF kwa majungu wanangoza yaani mtu anatunga uongo hadharani. Kongoli hapo juu upate ukweli.
Ni mwana "MAGUFULI 4 LIFE" mwenzako huyo... si unajua nyie majamaa mlivyo waongo!!! Yaani jamaa bila aibu anamshusha Mkwawa simply because alishindwa vita bila kuangalia Mkwawa alishindwa vita dhidi ya nani, na huyo Mirambo alikuwa anashinda vita dhidi ya nani!!!

Bila aibu anadai eti "hakuna mzungu aliyeleta fyokofyoko". Sasa sijui Wazungu gani anaowasema hawakuleta fyokofyoko mbele ya Mirambo!!
 
Mkuu usipotoshe historia. Mtemi Mkasiwa ndiye alikuwa anauza watu wake na ndiye aliye wakaribisha waarabu Tabora. Kuhusu Napoleon wa Afrika ni bahari kubwa usisikilize propaganda mkuu. Mtemi Mirambo akisikia unauza watu kama watumwa anakuja kukupiga nakuchukua himaya yako inakuwa yake. Ndicho kilichomfanya Mtemi Mkasiwa kuwaalika waarabu aishi nao akimuhofia Mtemi Mirambo.
Hiki nacho kieleza sio propaganda za Magumashi. Ndio ukweli 100%.

MAGUFULI4LIFE.

Can you explain why Mirambo had a very close relationship with Tip Tip?
 
Afu kama kuna watani wangu wanyamwezi humu. Nitawaambia kitu kimoja. Msijivunie Mirambo sana kwani sio mtu wenu. Mababu wa Mirambo ni watu wa kutoka katika milima ya Usagara iliyopo Morogoro. Waliokuja huko kuwinda tembo na kufanya biashara na kuanzisha kijiji cha Usagali....Hivyo mtupe heshima nyie...
 
Uwezo wa Mowawa sikudhani kama unaweza kubezwa kiasi hiki, Mkwawa alikuwa mtu na akili nyingi sana katika utawala wake, inasemekana Mkwawa angekuwa hai basi kusini mwa Tanzania yote ingekuwa yake.

Isike baada ya kuogopa kupigwa na Mkwawa basi akamtoa binti yake aje kuolewa na Mkwawa ili asishambuliwe na huyo binti alikuwa anaitwa Sekilonge, Mkwawa hakuwa anafanya biashara ya watumwa ila alikuwa anatoza kodi kwa kila mtu anayepita kwenye himaya yake, mpaka hiyo njia ya biashara ya kwrnda Tabora Mkwawa pia alikuwa anaishikiria na ndicho chanzo cha wajerumani kukasilika zaidi. Si hivyo tu mkwawa alikuwa Mwanadiplomasia mzuri maana aliwahi kutuma ujumbe wa kwenda kujadiliana na wajerumani japo wajerumani waliwauwa wajumbe wale. Mkwawa inasemekana katika maongezi yake yeye alisema kabakiza vita moja tu nayo ni ya wamasai
Mkuu hatumbezi Mkwawa ndio maana kuna aya nilisema naye si haba ila kwa Mirambo Mkwawa hagusi. Mirambo aliua wamisionari wawili na hakuna mzungu aliyeenda kuhoji. Jamaa hakuwa na maneno mengi. Jinsi alivyo fanya Mirambo ingewekwa wazi watanzania wote wakajua hakuna mtanzania ambaye angemuogopa na kumsujudia mzungu.
Wewe unasema Mkwawa angechukua kusini yote ya Tanganyika wakati Mirambo kachukua Shinyanga,Mwanza, Kagera, Kigoma na Burundi yote.

Aliyeuwa wanajeshi akiwemo kamanda mkuu Von nzelewsky na aliyeuwa wamisionari wasio hata na kisu nani anatakiwa kuohopwa hapo?
 
Ukishashiba makande basi unakaa unaamua leo utoe story gani. Form four mitihani mnaanza lini?

Back
Top Bottom