Bajeti ya kunguru
JF-Expert Member
- Sep 21, 2014
- 1,371
- 1,041
Habari zenu wakuu.
Kumekuwa na upotoshaji mkubwa wa historia hasa linapokuja suala la uwezo wa Mwafrika kutokupewa sifa zinazotakiwa kama ilivyo kwa hayati J.K. Nyerere na Nelson Mandela. Afrika inaaminishwa Mandela ni zaidi ya Nyerere hiki ni kituko.
Kuna hili pia la Chief Mirambo na chief Mkwawa eti sifa kubwa anapewa Mkwawa ili tumuone ndio shujaa wetu na pia alipambana akashindwa na wazungu. Nadhani wanataka kutujengea mazingira ya kuwasujudia na kuwaogopa. Itawezekanaje uniamnishe shujaa wangu wa kuigwa ni yule aliyepigwa wakati kuna waliopiga?
Baada ya kuifatilia historia ya mtemi Mirambo a.k.a. Napoleon wa Afrika kama alivyojulikana na wazungu nimegundua kuna upotoshaji mkubwa wa historia.
Chief Mkwawa japo naye si haba ila kwa chief Mirambo hatii mguu hata kucha.
Nguvu za jeshi la Mirambo kwa Afrika mashariki alikuwa hana wakumlingasha. Ndiye aliyetawala eneo kubwa kuliko machief wengine. Tabora mpaka Kigoma eneo lake lilipakana na ziwa Tanganyika japo aliona haitoshi akaingia mpaka Burundi akapiga himaya ya Urundi akasambaratisha.
Wakati Mkwawa anasilaha za jadi kabla hajaletewa bunduki moja na Mwarabu, Mirambo alikuwa anatengeneza bunduki yeye mwenyewe na alimiliki jeshi lilikowa na active personnel zaidi ya 10000.
Hapakuwa na cha mzungu wala mwarabu aliyeleta fyoko kwenye himaya yake aliua kama anau panzi tu ikabidi wafate masharti yake kila wanapopita kwenda Zambia na Kongo walimlipa kodi kwa kuikanyaga ardhi yake huna kodi mzigo wote unabaki na kuwa mali yake.
Wafipa walijichanganya hawakumjua vizuri kichwa chake kikoje. Huyu jamaa alikuwa hana masihara kabisaa!
Wazungu baada ya kubanwa sana waliomba nguvu ya jeshi kutoka kwa sultan wa Zanzibar wakimwambia kwamba Napoleon wa Afrika anataka kuiharibu biashara yako kwakuwa ndiye alikuwa mnunuzi mkubwa wa pembe za ndovu na watumwa kutoka Zaire na Zambia.
Sultan akatuma askari 3000 kuja kuongeza nguvu kwa wazungu wakishirikiana na jeshi la snitch wa Mirambo alikuwa anaitwa Chief Mkasiwa. Jamaa walinyoosha mikono sultan akaona anamaliza watu wake akaamuru jeshi lake lililosalia lirudi Zanzibar haraka walikuwa wamebaki 1500 ndio waliokuwa wamesalimika na jeshi la awali la Mtemi Mirambo lililokuwa likiitwa Luga Luga (walugaluga).
Mtemi Mirambo alikuwa na majeshi matatu ambayo aliyapanga kwa ubora kutoka la kwanza hadi la tatu. Jeshi kali kabisa lenye mafunzo na uwezo wa juu kabisa liliitwa Abaoko kama sijakosea herufi.
Sasa Mkwawa aliuza mali zake kwa Mwarabu pembe za ndovu na kuletewa nguo Mirambo hakuuza mali zake bali alichukua za wazungu walizokuwa wamekusanya sehemu mbalimbali.
Mirambo alichukua watumwa kutoka mikononi mwa wazungu na waarabu na kuwasajili kwenye jeshi lake. Yaani unapomtaja Mirambo jua unataja habari kubwa.
Sasa historia za namna hii zinafichwa na kuoneshwa historia dhaifu ya kumtukuza mzungu kuwa ni bora.
Mtemi Mirambo alifariki kwa ugonjwa wa rovu miaka ya 1880.
Nimeweka hapa kwa kifupi sana. Kwa mwenye interest anaweza kufatilia ahakikishe mwenyewe.
MAGUFULI4LIFE.