Mtela Mwampamba ni mzushi wa kawaida, Apuuzwe!!.

Watu bwana. Unatukana ungali umejificha uvunguni mwa kitanda. Si toka huko chini, njoo kwa jina lako halisi halafu mtukane mtesi wako?
 
katika e.mail yangu nimetumiwa ujumbe na mmoja wa viongozi wa chama (chadema) akiniomba kutolea ufafanuzi suala hili la kizushi na la kipuuzi lililowahi kuandikwa kwenye mitandao ya kijamii na kujadiliwa sana siku zilizopita.

Kwnza napenda kuwajulisha watanzania hususan wanajamiiforums kuwa sijawahi kuonana uso kwa uso na huyo kijana anayejiita mtela mwampamba. Kwa maana hii ni kwamba obviously alichokisema amekipika kutoka kwenye vyanzo dhaifu vinavyojifanya kunifuatilia kwa muda mrefu sasa.

Amekuwa akitumia nafasi ambazo mimi huwa busy kwenye shughuli zangu za ujasiriamali ama kunichafua mimi moja kwa moja na ama kuniunganisha na dots za kijinga kuichafua chadema. Niliwahi kumkanya mara kadhaa kule facebook lakini naona hakunielewa. Kwa andiko langu hili naomba nimpe onyo kwa mara ya mwisho juu ya kutumia jina langu popote kwenye tender za kashfa ambazo amekuwa akipewa.

Kwa ufupi sana kutokana na habari yake ni kwamba;
1. Sijawahi kwenda russia
2. Safari zangu za libya hazikuratibiwa na chadema na wala sikuiwakilisha chadema popote
3. Sikuwahi kufanya kazi makao makuu ya chadema.

Deus f mallya
14.12.2013
_____________



mtela mwampamba aliandika...."napenda nianze kwa kuwaambia kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa chadema kuwakana wapambanaji wao na vijana waliokuwa wanajitolea hali na mali, wanajitolea nafsi na uhai kuipigania chadema. Nitawaambieni juu ya wachache waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama ifuatavyo:-

i) deus mallya:

kwa mara ya kwanza nakutana na deus ilikuwa ni mwaka 2007, nikiwa nimejiunga na chuo kikuu cha dar es salaam, ambapo nilishakuwa mwanachadema kabla ya kuingia chuo kikuu, hivyo nilipofika chuo nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa chadema hasa wale waliokuwa wanatumikia makao makuu ndipo nilipokutana na deus mallya ambae alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa vinabeba ujumbe wa chadema na falsafa mbalimbali za ukombozi ambazo chadema ilikuwa ikinajinasbisha nazo.

Nilipokutana na deus tulipanga na kupeana ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae aliniunganisha na john mnyika ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni mkurugenzi wa vijana na afisa wake akiwa marehemu regia mtema, ambapo deus alikuwa ni mtu wa karibu na maafisa hao, hasa mnyika.

Na walikuwa pamoja na kufanya mambo mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;

a) safari ya deus mallya kuelekea libya katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijana kutoka chadema chini ya usimamizi wa mnyika.
B) safari ya russia ambapo deus alinieleza kuwa alienda kwa mafunzo maalum.

Lakini mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008, baada ya kutokea kwa kifo cha kutatanisha cha mheshimiwa chacha wangwe ambapo deus alikuwa ni dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile, john mnyika alimkana deus mara mbili, mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi juu ya kijana deus akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.

Hata baada ya kesi ya deus kumalizika na kisha deus kuachiwa huru, nilizungumza na deus juu ya kukanwa na mnyika na deus alinijibu kuwa mshikaji alimuomba radhi na kumtaka asahau yaliyopita na deus alikiri kumsamehe na imebaki hivyo mpaka hivi sasa (hili anaweza kulithibitisha deus mallya mwenyewe kwakuwa yu-hai)

lakini haikuishia kwa mnyika pekee bali hata benson kigaila ambae ni mkurugenzi wa oganaizesheni na mafunzo aliwahi kumkana na anaendelea kumkana mpaka leo hii, kiasi kwamba deus akienda pale makao makuu na akikutana na benson huwa anamuambia kuwa asiwe anakuja makao makuu maana chama kitachafuka kwa kuonekana mallya pale.

Ni mtu ambae hafikiri sawasawa tu ndie atakayeweza kusema usaliti huu hauna asili ya ndani na kuwa ni hulka za viongozi wakuu wa chadema kuendelea asili yao hiyo.

Angalizo:
Nitasema kama nilivyokutangulia kusema hapo awali juu ya hatma ya vijana ndani ya chadema, na leo nitasema hivi;
ikiwa hii miti mibichi inatendewa hivi., je ninyi miti mikavu mtatendewa vipi..? Ambao hata makao makuu ya chama hamyajui wala hakuna anayewajua zaidi ya kuwatumia kwenye maandamano na mikakati yao".

hivi hakuna sheria ya kuwakamata hawa watu ambao wanazunguka nchi nzima kukichafua cmd na kwafunga jela.?chadema ni chama kikubwa kushinda hata ccm kwa maana kupendwa.ifike wakati sheria zitumike.itatokea siku wanacdm wakachua sheria mkononi.
 
Back
Top Bottom