Mtela Mwampamba ni mzushi wa kawaida, Apuuzwe!!.


Deus F Mallya

Deus F Mallya

Verified Member
Joined
Jul 28, 2011
Messages
706
Likes
4
Points
0
Age
34
Deus F Mallya

Deus F Mallya

Verified Member
Joined Jul 28, 2011
706 4 0
Katika e.mail yangu nimetumiwa ujumbe na mmoja wa viongozi wa chama (CHADEMA) akiniomba kutolea ufafanuzi suala hili la kizushi na la kipuuzi lililowahi kuandikwa kwenye mitandao ya kijamii na kujadiliwa sana siku zilizopita.

Kwnza napenda kuwajulisha watanzania hususan WanaJamiiforums kuwa sijawahi kuonana uso kwa uso na huyo kijana anayejiita Mtela Mwampamba. Kwa maana hii ni kwamba obviously alichokisema amekipika kutoka kwenye vyanzo dhaifu vinavyojifanya kunifuatilia kwa muda mrefu sasa.

Amekuwa akitumia nafasi ambazo mimi huwa busy kwenye shughuli zangu za ujasiriamali ama kunichafua mimi moja kwa moja na ama kuniunganisha na dots za kijinga kuichafua CHADEMA. Niliwahi kumkanya mara kadhaa kule facebook lakini naona hakunielewa. Kwa andiko langu hili naomba nimpe onyo kwa mara ya mwisho juu ya kutumia jina langu popote kwenye tender za kashfa ambazo amekuwa akipewa.

Kwa ufupi sana kutokana na habari yake ni kwamba;
1. Sijawahi kwenda Russia
2. Safari zangu za Libya hazikuratibiwa na CHADEMA na wala Sikuiwakilisha CHADEMA popote
3. Sikuwahi kufanya kazi Makao makuu ya CHADEMA.

Deus F Mallya
14.12.2013
_____________Mtela Mwampamba aliandika...."Napenda nianze kwa kuwaambia kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kuwakana wapambanaji wao na vijana waliokuwa wanajitolea hali na mali, wanajitolea nafsi na uhai kuipigania Chadema. Nitawaambieni juu ya wachache waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama ifuatavyo:-

i) DEUS MALLYA:

Kwa mara ya kwanza nakutana na DEUS ilikuwa ni mwaka 2007, nikiwa nimejiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo nilishakuwa mwanachadema kabla ya kuingia Chuo Kikuu, hivyo nilipofika chuo nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa Chadema hasa wale waliokuwa wanatumikia Makao Makuu ndipo nilipokutana na DEUS MALLYA ambae alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa vinabeba ujumbe wa Chadema na falsafa mbalimbali za Ukombozi ambazo chadema ilikuwa ikinajinasbisha nazo.

Nilipokutana na DEUS tulipanga na kupeana ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae aliniunganisha na JOHN MNYIKA ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa Vijana na Afisa wake akiwa Marehemu Regia Mtema, ambapo DEUS alikuwa ni mtu wa karibu na maafisa hao, hasa MNYIKA.

Na walikuwa pamoja na kufanya mambo mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;

a) Safari ya DEUS mallya kuelekea LIBYA katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijana kutoka chadema chini ya usimamizi wa Mnyika.
b) Safari ya RUSSIA ambapo DEUS alinieleza kuwa alienda kwa mafunzo maalum.

Lakini Mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008, baada ya kutokea kwa kifo cha kutatanisha cha Mheshimiwa CHACHA WANGWE ambapo DEUS alikuwa ni Dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile, JOHN MNYIKA alimkana DEUS mara mbili, mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi juu ya kijana DEUS akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.

Hata baada ya kesi ya DEUS kumalizika na kisha DEUS kuachiwa huru, nilizungumza na DEUS juu ya kukanwa na MNYIKA na DEUS alinijibu kuwa mshikaji alimuomba radhi na kumtaka asahau yaliyopita na DEUS alikiri kumsamehe na imebaki hivyo mpaka hivi sasa (hili anaweza kulithibitisha DEUS MALLYA mwenyewe kwakuwa yu-hai)

Lakini haikuishia kwa MNYIKA pekee bali hata BENSON KIGAILA ambae ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo aliwahi kumkana na anaendelea kumkana mpaka leo hii, kiasi kwamba DEUS akienda pale Makao Makuu na akikutana na BENSON huwa anamuambia kuwa asiwe anakuja Makao Makuu maana Chama kitachafuka kwa kuonekana MALLYA pale.

Ni mtu ambae hafikiri sawasawa tu ndie atakayeweza kusema USALITI huu hauna asili ya ndani na kuwa ni hulka za viongozi wakuu wa Chadema kuendelea asili yao hiyo.

ANGALIZO:
Nitasema kama nilivyokutangulia kusema hapo awali juu ya hatma ya vijana ndani ya chadema, na leo nitasema hivi;
IKIWA HII MITI MIBICHI INATENDEWA HIVI., JE NINYI MITI MIKAVU MTATENDEWA VIPI..? ambao hata makao makuu ya Chama hamyajui wala hakuna anayewajua zaidi ya kuwatumia kwenye maandamano na mikakati yao".
 
bucho

bucho

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2010
Messages
4,788
Likes
943
Points
280
bucho

bucho

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2010
4,788 943 280
Damu ya chacha wangwe haitaenda bure dogo. Watch and c .
 
MUSSA ALLAN

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2013
Messages
18,953
Likes
7,590
Points
280
MUSSA ALLAN

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2013
18,953 7,590 280
We Deus watanzania wanakutazama tu, usidhani wamesahau!
 
W

wauwau

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
705
Likes
0
Points
33
W

wauwau

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
705 0 33
Malya tuel;eze ulivyomwua Wangwe, ulitumwa na nani na ulilipwa shilingi ngapi. La sivyo damu ya Chacha itakuandama popote ulipo. Nenda kanisani utubu na mwambie kasisi unataka umma wa Watanzania na dunia ijue kisa cha kufariki ghafla kwa Chacha kwenye ajali na wewe ukatoka mzima. Period
 
Mapi

Mapi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
6,864
Likes
179
Points
160
Mapi

Mapi

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
6,864 179 160
huyo kiongozi "UMESHAMJIBU???"
 
Apolinary

Apolinary

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Messages
4,726
Likes
68
Points
145
Apolinary

Apolinary

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2011
4,726 68 145
Na. vile vile msisubir mpaka uongo huo uenee, Toeni ufafanuzi Mapema ili kuondoa hali ya sintofahamu Deusi Mallya
 
Last edited by a moderator:
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
22,181
Likes
890
Points
280
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
22,181 890 280
Malya tuel;eze ulivyomwua Wangwe, ulitumwa na nani na ulilipwa shilingi ngapi. La sivyo damu ya Chacha itakuandama popote ulipo. Nenda kanisani utubu na mwambie kasisi unataka umma wa Watanzania na dunia ijue kisa cha kufariki ghafla kwa Chacha kwenye ajali na wewe ukatoka mzima. Period
Kwasababu CCM sera yenu ni kuuwa viongozi wenu hivyo mnaamini ana chadema ndiyo ilivyo, namlilia Salome Mbatia.
 
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
8,386
Likes
5,192
Points
280
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
8,386 5,192 280
Na. vile vile msisubir mpaka uongo huo uenee, Toeni ufafanuzi Mapema ili kuondoa hali ya sintofahamu Deusi Mallya
Mimi sidhani kama ufafanuzi tu unatosha. Hii itawafanya watu wawe wanatunga uongo wakijua kuwa kinachofuatia ni ufafanuzi tuu. Njia sahihi mtu anapozusha mambo ya uongo ni kumpeleka mahakamani...
 
REMSA

REMSA

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
2,577
Likes
44
Points
145
REMSA

REMSA

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
2,577 44 145
Huwezi kuwa ccm kama si muongo na mzushi,ni sifa mojawapo za kuwa mwanachama'
 
Deus F Mallya

Deus F Mallya

Verified Member
Joined
Jul 28, 2011
Messages
706
Likes
4
Points
0
Age
34
Deus F Mallya

Deus F Mallya

Verified Member
Joined Jul 28, 2011
706 4 0
Malya tuel;eze ulivyomwua Wangwe, ulitumwa na nani na ulilipwa shilingi ngapi. La sivyo damu ya Chacha itakuandama popote ulipo. Nenda kanisani utubu na mwambie kasisi unataka umma wa Watanzania na dunia ijue kisa cha kufariki ghafla kwa Chacha kwenye ajali na wewe ukatoka mzima. Period
......Vimbe wengine napata tabu kujua sayari mlizotokea kabla ya kuja hapa duniani,
 
kilght

kilght

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Messages
633
Likes
95
Points
45
kilght

kilght

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2012
633 95 45
mwampamba hana lolote afu ana akili ndogo sana wala hana ushawishi wowote mbele ya jamii
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,602
Likes
3,893
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,602 3,893 280
Deus,

The boy is paranoid.......!

Huyu ni mtu wa kumpuuza maana ni kwa bahati mbaya tu na mfumo mbovu wa siasa za mfumo wa vyama vingi uliomuwezesha mtu kama huyu kuwa katika siasa zetu.Ni fedheha kubwa sana kushiriki jambo linaloitwa siasa kwa watu wenye fikra za kijima kama huyu

Alipozusha kuwa mimi ndiye niliyemrekodi Lwakatare nilimuonya.Alipozusha tuhuma za Sumu nilimuonya lakini yeye na timu yake wakamdanganya mhariri wa Mtanzania Charles Mulinda na kumponza.Leo mhariri huyo maskini amefukuzwa na jukwaa la wahariri.Wao wamepoteza relevancy ya kisiasa ndani ya chama chao na nje ya chama

Well,Let's leave gutter politics for uninformed and the stupid!
 
K

kdc

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2013
Messages
638
Likes
135
Points
60
K

kdc

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2013
638 135 60
Ukiwa Muongo jaribu kua na kumbukumbu.kabla ya kujibu ungetafuta kwanza majibu ya Mnyika endeleeni kujichanganya.
 
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
8,418
Likes
3,926
Points
280
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
8,418 3,926 280
Mtela Mwampamba ni mganga njaa pale Lumumba, amekataa kufanya kazi aliyoisomea ya ualimu na sasa amekuwa Msukule wa Mwigulu Nchemba kwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi ambao hata kufundisha angeupata. Mkuu Deus Mallya mpuuze huyo dogo mliberali, ni njaa ndo inamponza akipata Job Security atatulia.
 
Exaud Mamuya

Exaud Mamuya

Verified Member
Joined
Jul 26, 2011
Messages
403
Likes
2
Points
35
Exaud Mamuya

Exaud Mamuya

Verified Member
Joined Jul 26, 2011
403 2 35
Huyu bwana mdogo Mwampamba ni mpuuzi sana. Namfahamu vizuri.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
523
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 523 280
R. I. P Chacha Wang'we...
 

Forum statistics

Threads 1,237,320
Members 475,533
Posts 29,284,515