Mtekwaji, usikubali kutekwa bila kuacha taharuki, fanya vurugu, ogopa gari usiogope bunduki kimbia

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Kukubali kuchukuliwa bila kuacha taharuki na kuwajulisha raia eneo hilo kuwa unakamatwa na watu wasio sahihi.

Hii inatokea mara Nyingi, mtekwaji anachukuliwa kwa kuaminishwa na Watekaji kuwa ni Maofisa Sahihi kwakuonyeshwa Vitambulisho.

KOSA: Ni kuamini kila Ofisa ni Mkamataji mwema, Watekwaji wanakosa muda wa Kuomba watu wa jirani hata wapita Njia
> Kuongozana naye
> Kufuatilia gari
> Kuwataka Maofisa hao waende naye kwa pamoja kituo cha jirani cha polisi
> Kushindwa kuomba wqpita njia wapigie simu Ndugu,jamaa na Marafiki

BADALA YAKE
Mtekwaji anategemea kupata Haki hizo au ushirikiano huo huko anapopelekwa

MAKOSA 10 TUNAYOFANYA WAKATI TUNATEKWA

1. Watu wanaokuja Kututeka mara Nyingi, huwa tunawaona hawapo katika utaratibu Rasmi wa Ukamataji kama Wanavyofanya Jeshi la polisi.

> Hawavai Uniforms
> Huja na magari ya kiraia
> Hawaonyeshi Vitambulisho
> Hutumia Nguvu badala ya Mashauriano au Maelewano.

KOSA: Ni kukubali kutoa Ushirikiano kwa watu hao, Kuogopa watakudhuru au kukuumiza wakati wa Mvutano

Wakati Ukweli ungepiga kelele kuita watu, au kuburuzwa au kujaza watu ungepata Msaada.

Ikibidi kama watakuua Bora wakuue Mwenge tuokote Maiti, kuliko kudhani bunduki zile aziwezi kukudhuru huko unakokwenda

4. KOSA LA NNE

Wale wenye Wasi wasi au Mashaka na Mwenendo wao kuhusika na utekwaji kukosa kampani katika Matembezi

Hawa ni
> Waandishi wa habari za Uchunguzi
> Wakosoaji wa mitandaoni
> Wanasiasa wa upinzani
> Watumashuhuri wasio kubakiana na Matendo au Mwenendo wa Serikali

Kama Upo Kwenye kundi hilo kwa nini Utembee Peke yako hata unapokuwa jirani na Maeneo au Makazi yako

Kumbuka kesi nyingi za Utekaji ni
> Kukosekana kwa taarifa za haraaka
> Kukosekana mtoa taarifa wa haraka
> Kukosekana anaye kariri namba za usafiri uliochukuliwa nao
> Kukosekana mpiga picha wa Matukio ya utekwaji

Basi kwa Namna hiyo, Usikubali kuwa katika Matembezi binafsi na kukosa Kampani kila Mara, mpaka pale hali ya hatari itakapo tulia

3. KOSA LA TATU

Kutaka mashauriano, mabishano ya kisheria, na maridhiano badala ya kujihami

Wanaokuja kukuteka wanajua wanavunja Sheria, Wanajua we unajua PGO na sheria zote za Makosa ya Jinai na Mwenendo wake, Achana na ubishi

SULUHU NI KUKIMBIA

Ndio naongelea Mbio, hizo hizo unazojua, je unakimbia kwenda wapi?

Mbio zako ziwe kuelekea
> Kituo cha jirani cha polisi
> Au kwa Polisi ofisa
> Kambi za jeshi
> Ofisa wa Jeshi
> Kama upo barabarani nenda hata kwa trafiki Ofisa

Hawa wote wakishuhudia ukamatwaji wako, Dhama itakuwa juu yao

Pia unaweza kukimbia kuelekea katika Maeneo au Majengo ya umma
> Ingia Sokoni
> Ingia Vyuoni au shuleni
> Ingia kanisani au Msikitini
> Ingia katika vituo vikubwa au vidogo vya daladala

Huko kote watakuwa na uwezo wa kukukamata wala siyo kukuteka, utapata support ya wananchi

6. KOSA LA SITA TUNALOFANYA WATEKWAJI

Kuendelea Kutumia Njia za Mawasiliano na Usafiri zile zile hata wakati tupo kwenye alert ya hatari

> Unaendelea kutumia Simu hiyohiyo
> Unaendelea kutumia line ya simu hiyohiyo
> Unaendelea kutumia Magari au Pikipiki zilezile hata baada ya kusikia fununu ya kufuatiliwa na watu usio wajua
> Kuendelea kupita njia zile zile wakati wa kurudi Nyimbani au kutoka Nyumbani hata wakati wa taarifa za kufuatiliwa kwako
> Kuendelea kutembelea Maeneo ya Starehe au Vijiwe vile vile hata wakati wa hatari

> Huo ni uzembe, Simu yako ikiwa inawaka ujue Watekaji wanakuona moja kwa moja.

> Kama unabadili line basi hakikisha unabadili na simu,na usiweke line ya zamani katika simu Mpya kwa sababu,Taarifa za mabadiliko ya line yako katika simu yatasomeka katika taarifa Mpya ya IMEI chequer124

Itaonyesha Mtumiaji wa simu fulani sasa ameweka line fulani kwenye simu fulani baada ya kutoa ile line fulani.
(Acha kutumia simu na line ya zamani zilizozoeleka)

> Usitembee nayo simu ya zamani katika gari yako hata kama umeizima,kwa sababu simu za kisasa zinaendelea kuonekana katika GPS hata kama hazipo ONLINE

7. KOSA LA SABA TUNALOFANYA WATEKWAJI.

Kuitikia wito wa watu tusiowajua kwa Tamaa ya fedha au Ngono

Watekaji ukijihami, No3, No4 na No5 kwa Maana kuepuka kukaa ameneo hatarishi,na kisha ukawa una kampani ya kutembea nayo wakati wote

Huja na Njia ya Kukuita kupitia
1. Kukutamabisha Deal za Biashara na kujifanya kuwa mnajuana katika biashara zako,hivyo angependa muonane Mpange namna nzuri ya kufanya biashara

Na wakati unasogea eneo hilo linakuwa limezungukwa na watu hao wanakuona kuanzia unakuja mpaka unakaa na kisha wao uamua wakuchukuaje

Mara Nyingi wanakuita Maeneo ambayo yanaendana na No4 na No 5 ili kufanikisha zoezi la wao kukuchukua bila kupata upinzani kwa watu wakiozunguka eneo hilo

2. Kama si Mtu wa Baishara, basi hutumia njia ya kukutamanisha NGONO, kwa kumtuma Mdada Mwenye sauti Nyororo kukuomba Mkutane huku akijifanya anakujua Sana.

Kwa Tamaa ya Ngono, mrembo au Mwanaume huyo humuita Mlengwa sehemu ileile ambayo haitakuwa rafiki kwa No4 na No5 ili kusaidia kukukamata kirahisi.

Wakati wote wa mazingira hatarishi,wakati matukio yabutekwajo yameshamiri epuka kupokea wito na kuitikia wito w MTU usiye mfahamu au kuwahi kumuona

5. KOSA LINGINE NI KUKAA/KUSHINDA MAENEO HATARISHI

Wewe upo katika kundi tajwa namba 4 hapo juu,

usikubali kwenda kutembea Maeneo yafuatayo
1. Maeneo yenye Watu wahache
2. Maeneo au Majengo ya Vyombo vya Serikali, ni rahisi kuficha taarifa zao
3.Maeneo yenye Misitu,Vichaka au Mapori, ambayo utakosa Msaada wa haraka
4. Maeneo ya Kiza au Ukimya, sababu Kelele na Mbio hazitokusaidia
5. Maeneo yenye makazi Machache, wanatabia kutokutoka nje kusaidiana na Majirani
6. Maeneo uliyozoea kutembele,badili hapo kipindi hichi cha hatari
7. Chagua maeneo Machache ya kutembelea hasa wakati wa hatari, Iwe rahisi kujua wanaokufuatilia

PUNGUZA MIZUNGUKO,SHINDA MAENEO SALAMA no3 Juu

8. KOSA LA NANE LA WATEKWAJI

> Kushinda eneo Moja kwa Muda Mrefu,Vijiweni,kumbi za starehe au Kazini

Ni jambo dogo lakini kubwa Sana,kwa watu wenye taaluma ya utekaji au Ufuatiliaji wa watu basi watu wenye tabia ya kukaa eneo moja zaidi ya Masaa 2 au 3 ni rahisi sana katika operwsheni za kuwachukua

Wanampatia Adui
> Muda wa kujipanga
> Muda wa kusoma idadi ya watu ulio nao
> Muda wa kuwakadiria nguvu au Nyenzo mnayoitegemea endapo wataanzisha ambush ya kukuchukua
> Unampa Adui Muda wa kuita wenzie pale anapogundua kuwa zoezi la kukuchukua litachukua Muda Mrefu au litakutana na Upinzani,basi huita Vikosi zaidi
> Unampa adui namna ya kuanza Kuyazoea maeneo hayo na Kujifunza tabia za watu au eneo la tukio

Mfano
- Pana walinzi?
- Pana mtu mwenye silaha?
- Pana Mtu anayeweza kuzia kwa nguvu?
- Kuna Camera zitaona?

Njia Pekee ni kuwa na Machale,tumia mida Michache Sana, katika Cikao au mikutano yako kila sehemu unayoenda na Unapoondoka eneo hilo

> Acha kinywaji Mezani wajue unarudi
> Ondoka kwa style ya kujifanya unaongea na Simu pembeni
> Ondokea njia ya kwenda Chooni,wajue unarudi
> Jifanye unampokea Mtu parking
> Omba wenzio wakusindikize mpaka kwenye gari
> Acha kulioa billi hadharani,acha pesa Mezani, wasikadirie Tendo lako linalofuata

9. KOSA LA 9 LA WATEKWAJI

Kushindwa Kuishi Mazingira sawa na hadhi ya kazi anayofanya

Hapa naongelea tena wale wote walengwa wa kundi la Utekwaji siyo tuh Tanzania bali Duniani,

> Wakosoaji wa Serikali
> Wakosoaji wa wanasiasa
> Wakosoaji wa wafanyabiashara wakubwa
> Wakosoaji wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
> Waandishi wa habari za Uchunguzi
> Wapigania Haki za Binadamu
> Wakosoaji katika Mitandao ya Jamii
> Wapelelezi wa kujitegemea na
> Watu Mashuhuri wanaotangaza Misimamo yao hadharani kinyume na Watu wenye mamlaka

Wanafanya kazi Hatarishi lakini wanaishi na kupenda kukaa Maneo yasiyo na Ulinzi au hadhi ya wapambanaji kama wao

Wanafanya makosa Sana pale
1. Wanapokosa magari,Unasikia wamekamatwa kwenye kituo cha Daladala
2. Wanaishi maeneo ambayo hayana Ulinzi maalum,Siyo getini tuh hata Mitaani hakuna sungusungu
3. Wanaishi Nyumba ambazo hazina Camera za kunasa Matukio
4. Magari yao hayafungwi Camera za mbele na nyima za Kuchukua Matukio
5. Simu wanazotumia kufanyia Ukosoaji in Public ndizo wanazo tumia kwa Shughuli zao binafsi
6. Wanashinda maeneo yasiyo na Ulinzi na hata camera za matukio
7. Wanakosa Hata silaha Ndogo za kujihami kwa Sababu zinauzwa ghali
8. Wanakaa kwemye makazi yanayoendana na Kipato siyo yanayoendana na kazi zao
9. Wanataka waishi Maisha ya starehe na huru kama Raia wa kawaida bila kujali hatari ya kazi au shughuli anayofanya
10. Wanarespond mazungumzo na watu wageni wasiowajua wakidhani ni kwa sababu ya umaarufu wao wala awajui kuwa ni Maadui zao

10. KOSA LA UOGA POTOFU

Watekwaji wanapaswa kujua kuwa, wanaokuja kuwateka hawajaja kuwaua.

Actually zoezi la kuwaua watekwaji ni rahisi kuliko zoezi za kuondoka na uhusika

Kama watekaji Nyara wangetaka kukuua
> Wasingekuja wengi
> Wasingeshuka kwenye gari,wange shoot
> Wasinge subiria wakufuate Mtaani,wangekufuata Nyumbani kukuua

Watekwaji wengi wanadanganyika na Silaha za watekaji ambazo katika zoezi la Utekwaji wao,naziona kama Mapambo

Silaha kubwa na mbaya Wakati wa Kutekwa ni GARI YA KUKUBEBA siyo BUNDUKI

zingatia utakapokuwa unaanzisha Varangati au mbio,ondoa kabisa Wasiwasi kwamba wata ku shoot kukuua

Kuwa huru kimbia Usilisogelee gari lao

Kimbia kabisa wasikuongize ndani ya gari

Kimbia kabisa Wakati unaongea Pawe na Distance na Mlango wa wewe kutupwa ndani ya gari,mfano ruka Mtaro kaa ng'ambo ya pili,vuka barabara pambana upande wa kulia wa gari pasipo na Mlango

Katika zoezi la kutekwa Ogopa gari usiogope Bunduki

Hata hivyo ni heri tukukute umejeruhiwa ua kuuwawa barabarani kwa Sababu hata huko unapopelekwa huna uhakika kama utarudi ukiwa hai.


Kumbuka: Ukitekwa ndo muda sahihi wa kutumia silaha yako. Piga ya kichwa, choma kifuani. Jihami. Self defense.
 
,
Nyongeza: Kwa mazingira tuliyonayo ya kutekana, human rights activists, ni vema mtu ukatembea na bussiness cards mfukoni kama 20 hiv. Wakikuteka unapiga kelele na kutoa hizo bussiness cards unawarushia wapita njia wasaidie kuwa umetekwa wawapigie ndugu zako. By that, lazima bussiness cards ziwe modified kuweka jina la ndugu zako! Piga kelele ukitamka, wasiojulikana, wasiojulikana , wasiojulikana wananiteka... etc au neno lolote unaloona litaamsha ari ya watu kutaka kujua kulikoni na kuzua taharuki
 
Retired,
Sasa hiyo business card ina namba zako au za watu wanaopaswa kupigiwa? Kama ina namba zako, mtu akiokota hiyo business card, si ataishia kukupigia wewe(labda kama simu yenye hiyo line wanayo ndugu zako).
 
Sasa hiyo business card ina namba zako au za watu wanaopaswa kupigiwa? Kama ina namba zako, mtu akiokota hiyo business card, si ataishia kukupigia wewe(labda kama simu yenye hiyo line wanayo ndugu zako).
Swali zuri sana na idea nzuri, Ndiyo maana nimeweka specifically kwa wanaharakati wa haki za binadamu. In that case lazima uweke namba za ndugu zako! Lazima kuwe na modification za bussiness cards katika mazingira ya sasa!
 
Maelezo mazuri sana. Ni wazi wabaya wetu wanaofanya tabia hiyo tumewajua maana umesema hatari ya kutekwa ni kwa wakosoaji wa serikali na wakosoaji wa wanasiasa.

Hivyo watekaji ni Serikali na Wanasiasa, ndio adui wa maisha yetu.

Somo limehusu jinsi ya kujihami mtekwaji. Mimi nadhani sasa tutor elimu kwa Watanzania nao "wasiotekwa" kuanza kuacha kushangaa. Tulishaona wakisikia neno mwiziii, basi wezi hao watazingirwa kwa kila namna na mwisho kupokea kipigo hadi kuchomwa moto pamoja na kuwa wanakuwa na silaha.

Tutangaze vita! Vita dhidi ya watekaji na wanasiasa hao wanaotuma watekaji. Lazima tunawajua tuwakomeshe.
Kama serikali nayo imeingia kwenye njia hiyo nayo adhabu ni kuiondoa na wapo watumishi wema watakuja wataja tuu watu hao na sheria itawaangukia, tuwatoe kwanza.

Popote ulipo ukisikia mtu anapiga kelele "natekwa" toa msaada hata wa kublock njia kwa gari na watu washambulie kwa kila dhana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali zuri sana na idea nzuri, Ndiyo maana nimeweka specifically kwa wanaharakati wa haki za binadamu. In that case lazima uweke namba za ndugu zako! Lazima kuwe na modification za bussiness cards katika mazingira ya sasa!
Hata kusaidia tuu kujua huyu aliyetekwa ni nani maana sio kila uendako watu wanakufahamu.
Ni wazo zuri kutupa utambulisho huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unanikumbusha kisa kimoja.

Mama mmoja alitupa uchafu stand ya moshi akakamatwa na wale mgambo...mama aligoma kwenda hadi akaja jamaa mmoja akalagai.

Maana mama anajua kule akienda ni faini tu na ni 50,000.
Jamaa akamwambia wewe twende ukawe balozi wetu wa usafi....kuna vipeperushi tutakupa utahamasisha usafi kila uendako yaan ni kasemina tunakupa.

Mama kaenda ofisini tena alifurahi na kutangulia mbele.

Kilichotokea huko nadhan hakuadithia hata mume wake
 
Swali zuri sana na idea nzuri, Ndiyo maana nimeweka specifically kwa wanaharakati wa haki za binadamu. In that case lazima uweke namba za ndugu zako! Lazima kuwe na modification za bussiness cards katika mazingira ya sasa!
Your name says it all ! RETIRED. yaani business card yako uweke namba za nduguzo !😳
 
Your name says it all ! RETIRED. yaani business card yako uweke namba za nduguzo !😳
Yes, why not in this era of kutekana. nimesema for human rights activists as they are the ones in danger of these atrocities! Lazima kubadiliha set up/design ya card zao! ( au linakubabaisha neno bussiness card)
 
Asee ,asante sana kwa Elimu hii.Nna aamini kwa wale wazembe watafuata hii kanuni walau itawasaidia kuwaepuka Maadui.Nna wasisitizia mkiweza fanyeni Mazoezi ya kutumia Silaha ndogo kama Visu ni Muhimu sana inasaidia kwa Sehemu。

Poleni sana mliowahi kufikwa na haya mabaya kutoka kwa Watu wabaya.
 
Yes, why not in this era of kutekana. nimesema for human rights activists as they are the ones in danger of these atrocities! Lazima kubadiliha set up/design ya card zao! ( au linakubabaisha neno bussiness card)

Ameshindwa kujua wakati wa tahadhari unatakiwa kuishi tofauti ,kila kitu ni mbinu
 
Ameshindwa kujua wakati wa tahadhari unatakiwa kuishi tofauti ,kila kitu ni mbinu
asante for clarification and understanding, yeye anajua classical definition ya business card na ndiyo maana nimesema kuwa katika era hii, design ya kadi lazima ibadilike!

One should not be obsessed with this classical def of a business card: Business cards typically include a person's name, e-mail address, phone number, website, and company name.
 
Back
Top Bottom