Mteja NHC ajenga ghorofa kwenye nyumba aliyopanga

babuwaloliondo

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
378
174
KATIKA hali isiyo ya kawaida mpangaji mmoja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Leila Visram, amejenga nyumba nyingine ndani ya eneo alilopangishwa na shirika hilo.
Visram ambaye anaishi maeneo ya kata ya Hananasifu, mtaa wa Muungano, nyumba plot namba 67 Kinondoni, jijini Dar es Salaam, amefanya hivyo huku akiwa mmoja wa wadaiwa sugu wa shirika hilo.
Zoezi hilo lilikuwa kama sinema kwani mmoja wa wafanyakazi wa mwanamke huyo aliamua kuwafungia geti kwa ndani watu waliokuwa katika zoezi la ukaguzi huo kisha kutokomea kusikojulikana.
Meneja wa Kitengo cha Kukusanya madeni wa NHC, Japhet Mwanasenga, aliongozana na waandishi wa habari katika eneo hilo ili kumtolea vitu vyake nje kutokana na kuwa miongoni mwa wadaiwa sugu kwani anadaiwa sh milioni 17.4 hadi kufika Machi mwaka huu.
Alisema mdaiwa huyo sugu amejenga nyumba hiyo ndani ya eneo lao bila ruhusa.
Alieleza kuwa sababu ya kushindwa kumchukulia hatua mapema hadi kufikia jana ni kutokana na Visram kuweka zuio la mahakama katika kesi namba 42 iliyounguruma katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo NHC ilishinda hivyo kuamuru mwanamke huyo kutolewa.
Alisema mwanamke huyo anadaiwa deni hilo tangu mwaka 1996 na hata walipowekeana mkataba naye wa kulipa alishindwa badala yake alilipa sh milioni nane pekee.
Wakati zoezi la kumtolea vitu likiwa likiendelea, mdeni huyo wa NHC alisikika akizungumza kwenye simu na meneja huyo kumtaka kutomtolea vitu nje ili akamalize deni lake jambo ambalo halikuzaa matunda.



h.sep3.gif
source : Mteja NHC ajenga ghorofa kwenye nyumba aliyopanga

Kweli Bingo shamba la bibi
 
Hebu jiulize, wapo wengi tu wa namna hii, tukisema ukweli mnatuita wabaguzi, kama wahindi wanashindwa kulipa wapeni Watanzania hizo nyumba. kwani nani kasema watashindwa kulipa.
 
NHC wmeifaidi hiyo gorofa kwani huyo mpangaji hakuwa na haki ya kujenga bila kibali cha mwenye nyumba.lau aukiweza aibebe hiyo gorofa.kisheria hana haki ya kuishi ktk hiyo gorofa.
 
Back
Top Bottom