Mtei: Zitto Hahitajiki ndani ya CHADEMA, Uamuzi wa Kamati Kuu ni wa Mwisho!

Suala kwamba nimesoma ama sijasoma halihusiani na mada tajwa. Toa hoja, kama huna bora ukae kimya kuliko kuanza kuporomosha matusi.

Basi kweli hujui unachokifikiria pamoja unachokiandika! Reference: Angalia threads zinazotolewa humu hii ni pamoja na yako: What is your intention and what do you want to achieve with this kind of unjustifiable arguments! Pls try to think before to pass such kind of commenst to JF!
 
Sitaingia sana maana zito ni kama marehemu aliyepoteza pumzi iitwayo chadema.Ila nimejifunza kwamba ramadhani ighondu ni zaidi ya ibilisi na kikwete sio mtu wa kumwamini hata kidogo na mwisho kama zitto anahisi yeye ni mzito hivyo, kwanini asihame tuione hiyo cdm inavyopasuka.chadema itasimama tu.na zitto ni mwepesi tu kama ubua.
 
chadema is too superior to be judged from DULUTI-USARIVER, na hapa ndipo zzk anapoamua kudeal na mama za vifaranga na kuwadharau vifaranga.
in the centre of chrisis is where you can find hidden details.
zzk..
 
Sitaingia sana maana zito ni kama marehemu aliyepoteza pumzi iitwayo chadema.Ila nimejifunza kwamba ramadhani ighondu ni zaidi ya ibilisi na kikwete sio mtu wa kumwamini hata kidogo na mwisho kama zitto anahisi yeye ni mzito hivyo, kwanini asihame tuione hiyo cdm inavyopasuka.chadema itasimama tu.na zitto ni mwepesi tu kama ubua.

Kwanini hampendi kukubali hata mambo yaliyo wazi ama ndo mwendo wa TOMASO?
 
Mtei yupo sahihi, hata Zito alilijua hilo huwezi kumshitaki kiongozi wako hafu ukasalia kuwa mwananchama, kama ni kuhusu cham kuwa mali ya mtu hata Baba wa Taifa CCM ilikuwa mali yake hadi anafariki kiongozi yoyote wa cham akitofautiana na chama alikuwa nafukuzwa au kupotezwa mifano ipo inajulikana, Muulizeji John Samweli ilikuwaje atoswe ktk nfasi ya PM kisa alikuwa ktk kundi la G55 na ilimgharimu hadi kwenye bio zake za kuwa Rais wa Tz, chezea waanzilishi wa vyama utaumia.

Waku, Katika pitia pitia katika magazeti ya mtandaoni, nimekutana na kauli kutoka kwa mwasisi wa CHADEMA Mzee Edwin Mtei kwenye gazeti la Mwananchi. Pamoja na mambo mengine, taarifa inasema

"Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde chama chake
au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa kwa sasa hana nafasi.
Pia ameshauri kuwa kama ana ndoto za kuwania urais ni vizuri akatafute
vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki.
Mtei alisema kuwa kama anataka kubakia na uanachama wa Mahakama wao hawana shida...
“Lakini huwezi kuwapeleka viongozi wako kortini na bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu.
”
Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali ndani ya Chadema na hata kuzua
mitafaruku ya hapa na pale huku akisema kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa mwisho."
Mwisho wa kunukuu.

My take: Je CHADEMA kama chama ni mali binafsi ya Mzee Mtei ama Wananchama? Kama ni mali ya wanachama, huo ujasiri wa Mzee Mtei kudai kwamba mwanachama fulani hatakiwi ndani ya chama anatoka wapi? Tujadili.​

source:
Zitto aibuka kidedea mahakamani - Kitaifa - mwananchi.co.tz


Update: Kauli nyingine iliyopatwa kutolewa na Mzee Mtei dhidi ya Mhe. Said Arif alipojivua Umakamu mwenyekiti kwa kutuhumiwa kumsaidia Mhe. Pinda kupita bila kupingwa uchaguzi wa 2010 na Kupinga Mzee Mtei kumchagulia watu wa kufanya nao kazi. "Aache Kulalamikia, kwasababu wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, mimi nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, alipaswa kujichunguza kwanza."

Source: Mwananchi
 
Mwenye chama ndiyo kashasema sasa. Yeye Mtei ndiyo HAYATOLLAH wa CHADEMA kama hamtaki basi, lakini huo ndiyo ukweli.

Hta Nyerere alikuwa ndo Ayatollah wa CCM, tatizo vijana hamjamkuta mwalimu, muulizeni John Malecela na kundi lake la G55, aliishia wapi, au hayati Kolimba.
 
Mwenye chama ndiyo kashasema sasa. Yeye Mtei ndiyo HAYATOLLAH wa CHADEMA kama hamtaki basi, lakini huo ndiyo ukweli.
hapana ndugu, mzee katoa yaliyo ya moyoni. maamuz ya mwisho yapo baraza kuu. na yeye ni member, so ikifika wakati wa kupiga kura zitto afukuzwe atapiga kura kama wengi wakisema aondoke au la., will decide destiny ya zitto.
 
Pole sana (my take),mwananchi wanafurahasha watawala,hawawezi sema kweli! Unategemea Mtei atoe kauli gan kwa huyo mnafiki anayesumbua?Waweza sema ni ukanda,saw a lakn unafiki,ujuaji haukubaliki sehemu yeyote hats ingekuwa ww , CDM mtoen huyo aende jimbo LA Juba
 
Kwa kauli hiyo naamini Mzee Mtei kafikia kikomo cha kufikiri au anasumbuliwa na uzee. Hata mkeo wa ndoa ukitaka kuachana naye kuna taratibu za kufuata. Kama yeye ni mwenye chama basi wanachama wawe ndugu zake na wakwe zake tu.
 
Kwa mara nyingine tena Mtei anathibitisha maneno ambayo yamekuwepo kwa muda sasa kuwa CHADEMA ni Saccos ya kikundi cha kina Mtei, Mbowe, Slaa na wachache wanaofanana nao-UDINI, UKABILA, UENEO, UCHAGA nk.Maandalizi yafanyike kwa ajili ya mazishi ya CDM
 
Wakati Nyerere alipomkataa Malecela au kama Malecela anaingia basi yeye anarudisha kadi chama kilikuwa ni chake au??
Wakati anamtoa baru Lowassa chama kilikuwa chake.
Acheni kujitoa akili nyie, na mnavyojitoa akili ndiyo hivyohivyo mnavyoishia kuwa.
Ni shida sana kumuelimisha mtu anayejitia Ujinga mwenyewe.


Sasa kama CCM na CDMni sawa kwa nini tupoteze ruzuku si muungane tujue moja kuliko kuliko kuchezea kodi zetu!!!!!!
Ebhooo jingaz sana wewe tetea hoja acha kufufua wafu hapa!!!!!
 
Hta Nyerere alikuwa ndo Ayatollah wa CCM, tatizo vijana hamjamkuta mwalimu, muulizeni John Malecela na kundi lake la G55, aliishia wapi, au hayati Kolimba.

Kwahiyo unakubali kuwa Mtei ni Ayatollah wa CHADEMA kama ambavyo Nyerere alivyokuwa CCM. So Role model ya CHADEMA ni CCM.
 
Heshima ya Mzee Mtei ndani ya CHADEMA ni kubwa sana na msisahau Mwl.JK Nyerere alijua umakini wa Mwenye kuanzisha CDM ndio maana alitamka wazi CHADEMA ndio chama mbadala cha kushika Dola.

Hata siku moja kama una akili timamu huwezi mpe heshimu Zito na ukamnyima Mtei Heshima mpaka na uhuru wa kusema chochote kwa ajili ya mambo yanayoendelea ndani ya chama.

Vinginevyo labda uwe Mwendawazimu ndio utamsifu Zito kwa kwenda Mahakamani na Kumwona wa Maana Zaidi ya Mwanzilishi wa Chadema.
 
Iko wazi hata kwa kipofu kwamba Ccm inamtumia Zitto kuchezea siasa chafu Chadema,
Lakini hakuna tatizo,au kama lipo ni kidogo sana, Hii ni ka vile tumeshamgundua na tulishamgundua hivyo hawezi kushinda mission yake na wanaomtumia.

Chadema imejaa watu wenye akili nyiingi sana kumzidi bw mdogo zito, anazoleta ni mbinu za kizamaani kabisa ambazo mwisho zitaisha kwa yeye Zitto kuisha kqbisa kisiasa na akiacha wanamageuzi tusiochoka tukiwa washindi!

Chadema haishabikiwi na wapuuzi, haiungwi mkono na wananchi wasiona kitu kichwani, washabiki na wanachama woote wa Chadema ni werevu sana na waliochoka kuiona Ccm ikiwafanya vibaya itakavyo!

Kwa jinsi hii Chadema kuloose itakuwa ngumu sana, kwa kuwa tunaoisupport tumeichoka na tunaichukia Ccm na wanachama wake kutoka moyoni.

Tunasubiri kwa hamu kubwa tuonyeshe kivitendo kwenye chaguzi zijazo kuwa ni jinsi gani Ccm tunavyoichukia!!
 
duh sauti nzito za maamuzi zimeanza sikika baba wa chadema family ametoa kauli nzito IPO siku atamkataa lisu na msigwa ukabila @work
 
Back
Top Bottom