Elections 2010 Mtei na Makani wapo kimya tu

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,876
2,748
Hawa waasisi wa CHADEMA wako wapi na wanafanya nini?

Nao tunataka watoe tamko lolote ama neno lolote kumsapoti Slaa. Hii vita sio ya Slaa na waleta habari peke yao. Waje hadharani tuwasikie nao wanasema nini kuyakabili haya majitu. Wakiachwa, wananchi wanaweza kuaminishwa kuwa Slaa kweli ni mchochezi.

Nakumbuka kitabu cha Hendrick Ibsen cha An enemy of the people. Maudhui yalikuwa hayahaya ila mazingira tofauti. Waasisi wetu hao wana mchango mkubwa sana katika hali ya sasa
 
Chadema huwa si watu wa kukurupuka.

Unapoyawaza hayo, wao walishawaza kabla yako.

Kwanza Dr. Slaa ni Katibu wa chama. Automatically Slaa (PhD) ni msemaji wetu. Hawezi kusema kitu bila kupata maelekezo ya hawa wazee wenye hekima.

Tulia.
 
Nao waje hadharani japo waweke nguvu. Huko nyuma ya pazia waliko ni wachache tunafaham hayo
 
Dr.slaa yuko juu kama mlima Kilimanjaro.Nilichogundua mimi ni kwamba Watanzania wengi tu wepesi wa kusahau, niwakumbushe kuwa Dr.SLAA aliwahi kuhojiwa kuhusu kushindwa kwake ktk uchaguzi na alisema;Kama nitashindwa kihalali sina tatizo na matokeo na bado nitakuwa na kazi nyingi sana za chama.Dr.Slaa ni tofauti na makatibu wengi wa vyama Tanzania wengi wao wanaona kama nafasi ya mzaha ndiyo maana CCM wamekiacha kiti hicho kwa msanii Makamba matokeo yake amekivuruga chama hadi kimeadhibiwa na wananchi 31 oct japo wamechakachua.

Naamini kuanzia sasa Dr.atakuwa katika heka heka za kuimarisha chama mbacho mara bunge likiapishwa CHADEMA ndiyo kitakuwa chama KIKUU CHA UPINZANI.Bado peopleeeeeeeeeeees power hadi mjengoni.Najiandaa kugombea udiwani 2015 kwa tiketi ya CHADEMA hakuna kulala hadi kieleweke
 
Ndugu lumaga unayasema hayo ukiwa na imani kabisa kuwa jk ndio keshakuwa rais. Hutaki kuyaona haya yanayoendelea. Au ushakata tamaa na huu mchakato wa ripoti kivuli ambayo ndio taswira halisi ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom