Mtego wa Rais Samia Suluhu Hassan ni upi kwa mawaziri

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Rais alipohutubia mara ya pili na mara ya Tatu alipokuwa akiwahotubia Mawaziri na Makatibu wakuu alizungumzia habari ya Uonevu, kesi na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua maramoja, akaongeza bango litakalo onekana DC au Mkurugenzi hawana kazi sisi hatujamuelewa vizuri hili swala la bango linaenda hadi kwa Mawaziri wateule.

Kumeibuka malalamiko mengi kuhusu Mawaziri na Makatibu wengine kurudishwa mahala ambapo walikuwa na si kubadilishwa, binafsi naweza kutafsiri yafuatayo:

1. Hao mawaziri walikuwepo na wanaelewa mambo mengi yanayoendelea katika jamii ikiwamo malalamiko, sheria ambazo hadi sasa bado wananchi wanazilalamikia na kero ambazo wananchi wanakutana nazo

Kuwaacha hapo hao mawaziri kwa maoni yangu ni kama Rais anawapa mtihani na pia ni mtego wa kuwategua kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi na kuwajibika. Alisema mmeanza na mimi sasa malizeni kero zote ni kwamba wasifikiri bado wapo kwenye zama zile wameteuliwa sasa ni wajibu wao kumaliza malalamiko na kero.

Kwenye mitandao kuna kero nyingi kama vile:

1. Malalamiko ya Sheria zinazoonekana kuwa kandamizi
2. Kesi zilizoweka watu Gerezani ambazo hazina mashiko na zingine kucheleweshwa kusikilizwa makusudi...Rais Samia Suluh Hassan Baada ya kuwateua sasa anawaangalia hawa mawaziri watafanyaje kuhusu haya kwa awamu yake maana tayari ni kero na je watayafanyia kazi?

Niwashtue tu kwamba kuna Mawaziri na viongozi wengine ambao tayari amesha wateua wataachishwa kazi kwa sababu ya kutosikiliza na kutofanyia kazi kero zote hizi. tutegemee mabadiliko tena ya uongozi.

USHAURI: Ni vema mawaziri hawa wajiongeze wamfuate wampe wazo kuwa kuna sheria tulitunga ambayo wananchi wanailalamikia sana tuiondoe au tufanyeje ili isiendelee kulalamikiwa . hii itakuwa hekima zaidi ya mengine yote.
 
Back
Top Bottom