Mtego wa mfanyakazi wa kike kwa mfanyakazi mwenzie mwanamme safarini

babalao

Forum Spammer
Mar 11, 2006
427
58
Kuna rafiki yangu mmoja wa kiume alinisimulia kisa kimoja kilichomkuta aliposafiri kikazi na dada mmoja ambaye wanafanya naye kazi pamoja na wanaheshimiana sana kama ifuatavyo. Walikodi vyumba viwili na Guest house zote zilikuwa zimejaa.

Ilipofika saa 4 usiku yule dada alipiga hodi kwenye chumba cha yule kaka akidai kuwa chumbani kwake kuna mdudu nge na anaogopa kulala kwenye chumba hicho. Yule kaka alijitahidi kumulika kwa tochi uvunguni mwa kitanda na kila mahali ili amuue yule nge lakini hakuonekana.

Baada ya hapo yule kaka alimshauri yule dada ahamie chumbani kwake kwa kuwa kitanda kilikuwa kimoja walikubaliana kulala mzungu wa nne yaani kila mmoja akilala kichwa kimoja kwenye mchago na kingine kwenya tendegu ili kukwepa kupata kishawishi.

Yule kaka alipata shida sana lakini alimudu mtihani kwa kujizuia na tamaa ya mwili, alifikiri mambo mengi kwamba yawezekana ni mtego wa yule dada kutaka kumpima au pengine huenda alikuwa na nia mbaya kama angeshindwa kuvumilia amwingize kwenye kesi ya kubaka.

Wana JF naomba mchango wenu Jee yule dada alikuwa na lengo gani kwa huyo kaka, kwani kama alikuwa anampenda au anamtaka si angemueleza kuliko kumtia majaribuni?

Karibuni mwenye hoja atoe hoja yake kwani suala hili bado lina mtesa yule rafiki yangu.
 
mmh jaman asi ashapas huo mtihan sasa unaumia nini tena?
pole sana lakin yashapita ..usiwaze n tak t easy sema ikitokea tena itabid umuulize dada ana nia gan..bt 4nw haina haja ya kuwaza cz USHAMSHINDA SHTEAN.
HONGERA SANA KWA KUMUEPUKA SHETAN.
 
Mbona mambo ya kawaida hayo. Waweza kulala kitanda kimoja na mtu wa jinsia nyingine bila kumfanya lolote. Haya Mambo usilazimishe kama mvuto upo itatokea tu. Na utapata roho kitu inapenda bila kubaka
 
Yap naungana na Rose coz yameshapita,ila pia huyo jamaa ni hero wa ukweli,congratulation bro maana sisi wanaume bwana...........!!!!
 
hamna kitu hapo bana fix tu hizo na nyinyi .sasa nge si angeenda reception kuwaambia
 
mmh jaman asi ashapas huo mtihan sasa unaumia nini tena?
pole sana lakin yashapita ..usiwaze n tak t easy sema ikitokea tena itabid umuulize dada ana nia gan..bt 4nw haina haja ya kuwaza cz USHAMSHINDA SHTEAN.
HONGERA SANA KWA KUMUEPUKA SHETAN.


sasa hapo Rose shetani ni nani?
 
Yaliyoendelea kujiri baada ya usiku huo wa nge ndo yanaweza kutoa picha ya nia ya huyo bibie japo kwa muhtasari. Je kuna vimitego vingine viliendelea, ama yaliishia pale pale? Btw, kalikuwa ni kamtihani flani it seems
 
hao wote walitegana na wote wakashinda vishawishi kwani kama chumba kina nge na huyo mkaka aliona nge hayupo angeenda kulala yeye kule kwenye nge na kumwachia binti chumba chake au la wangetoa taarifa kwa uongozi wa hotel au angesgusha net nge asingeingia kwenye net
 
Mbona mambo ya kawaida hayo. Waweza kulala kitanda kimoja na mtu wa jinsia nyingine bila kumfanya lolote. Haya Mambo usilazimishe kama mvuto upo itatokea tu. Na utapata roho kitu inapenda bila kubaka

Halohalooooo. Huyo dada nadhani hakupata usingizi maana ndie aliandaa mpango mzima. Nimemkubali kijana kwa kuweza kumshinda ibilisi:A S-baby:
 
hao wote walitegana na wote wakashinda vishawishi kwani kama chumba kina nge na huyo mkaka aliona nge hayupo angeenda kulala yeye kule kwenye nge na kumwachia binti chumba chake au la wangetoa taarifa kwa uongozi wa hotel au angesgusha net nge asingeingia kwenye net

Umenimalizia maneno kabisaaa!!!!
 
sasa hapo Rose shetani ni nani?

kwan we wadhan nani anaweza kuwa mtumwa wa shetan kat ya dada na kaka?
karibu chai babu leo samak wa kubanika +ndimu+pilipili na chaii swafi yenye tea masala ...karibu
nimekumiss jaman...nilipika mlenda juz wacha nkumbumbuke nkasema angejua nafanya nin apa angenichokoza...!!!
 
Yap naungana na Rose coz yameshapita,ila pia huyo jamaa ni hero wa ukweli,congratulation bro maana sisi wanaume bwana...........!!!!

nkweli
yashapita ..ameshashinda sasa anawaza nini?au anajutia kutoitumia chance vyema?
sion cha kuwaza apo as far as anaonekana ni mkaka strong mweny msimamo thabiti...I LIKE T
apo angekutana na watoto wa mbwa mbona ata nusu saa isingepita angerukiwa...angepewa alicholiitaj...
he z hero
 
Si mkaka angehamia chumba cha mdada, logical hii ni another Shigongo's copy n' paste story
 
HA HA HA HA Hata mimi nashangaa sijui kwanini huyu NGE kwanini aende chumbani badala ya kwenda reception

Siyo nge anamaana mdada angeenda kuwataarifu wahudumu wa reception kuwa chumbani kwake kuna nge na wala sii kwa mkaka eeh
 
kwan we wadhan nani anaweza kuwa mtumwa wa shetan kat ya dada na kaka?
karibu chai babu leo samak wa kubanika +ndimu+pilipili na chaii swafi yenye tea masala ...karibu
nimekumiss jaman
...nilipika mlenda juz wacha nkumbumbuke nkasema angejua nafanya nin apa angenichokoza...!!!

asante dia kwa hiyo breakfast,mmmmh mbona leo mapema sana!jana usiku ulipiga desh nini?nimependa hapo kwenye red: moyo wangu umefarijika na nadhani hata chai leo sio lazima tena, nimeshiba kwa hiyo kauli yako tu!!!!
 
Kuna rafiki yangu mmoja wa kiume alinisimulia kisa kimoja kilichomkuta aliposafiri kikazi na dada mmoja ambaye wanafanya naye kazi pamoja na wanaheshimiana sana kama ifuatavyo. Walikodi vyumba viwili na Guest house zote zilikuwa zimejaa. Ilipofika saa 4 usiku yule dada alipiga hodi kwenye chumba cha yule kaka akidai kuwa chumbani kwake kuna mdudu nge na anaogopa kulala kwenye chumba hicho. Yule kaka alijitahidi kumulika kwa tochi uvunguni mwa kitanda na kila mahali ili amuue yule nge lakini hakuonekana. Baada ya hapo yule kaka alimshauri yule dada ahamie chumbani kwake kwa kuwa kitanda kilikuwa kimoja walikubaliana kulala mzungu wa nne yaani kila mmoja akilala kichwa kimoja kywenye mchago na kingine kwenya tendegu ili kukwepa kupata kishawishi. Yule kaka alipata shida sana lakini alimudu mtihani kwa kujizuia na tamaa ya mwili, alifikiri mambo mengi kwamba yawezekana ni mtego wa yule dada kutaka kumpima au pengine huenda alikuwana nia mbaya kama angeshindwa kuvumilia amwingize kwenye kesi ya kubaka. Wana JF naomba mchango wenu Jee yule dada alikuwa na lengo gani kwa huyo kaka, kwani kama alikuwa anampenda au anamtaka si angemueleza kuliko kumtia majaribuni? Karibuni mwenye hoja atoe hoja yake kwani swala hili bado lina mtesa yule rafiki yangu.

huo siyo mtego na wala si majaribu, dada alitaka kulizwa baada ya uchovu wa safari. Mkiwa safarini lazima mjaliane ili kazi iende vizuri.
 
Kama alijua nge ni story geresha tu basi angemwachia room yake na yeye ahamie kwenye chumba cha huyo dada, simpo!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom