Mtego wa kwanza wa wahafidhina ndani ya CCM Rais Samia amenasa. The worst is to come

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Nakumbuka kauli ya JK na hapa namnukuu "Wanaccm hawaachiani maji ya kunywa mezani" kauli hiyo ni ya kijasusi na yenye mlengo wa kuwafanya wanachama na viongozi wandamizi kutoaminiana.

Leo gazeti la chama UHURU limerusha jiwe gizani na wote tumeyasikia makelele na sauti za kupatwa na jiwe hilo. Mfumo huu umeandaliwa kwa weledi wa hali ya juu na wahafidhina ndani ya chama.

Mtego wa kwanza wa kujua mipango ya Rais umekamilika na tayari wahafidhina washajua malengo ya bi mkubwa. Na baada ya mpango kukamilika wameamua kuupotezea kwa kushauri hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa wahariri but tayari malengo yao yameshakamilika. Jambo linalofuata ni kuwajua walio nyuma yake na mpango huo umeanza kusukwa kuanzia kwenye kupinga Chanjo.

Gwajima hayupo peke yake na yupo pale kuwajua walio upande wao tayari kuanzisha misukosuko. Taget ya mwisho itatoka nje kabisa ya chama nayo ni Katiba mpya.

HAKUNA JIWE LITABAKI JUU YA JIWE JINGINE.
 
Nakumbuka kauli ya JK na hapa namnukuu "ccm haachiani maji ya kunywa mezani" kauli hiyo ni ya kijasusi na yenye mlengo wa kuwafanya wanachama na viongozi wandamizi kutoaminiana...
Acha haraka,letetaarifa kwa hatua ina onyesha unayo taarifa ya maana.
 
Ashachoka, na alifikiri uraisi ni kazi ndogo.
Ndani ya CCM ana maadui watatu;
  • wale waliokosa nafasi 2015
  • wale wanaojifanya wapo upande wake huku nyuma ya pazia wanausaka uraisi. Hapa kuna February
  • wale wa utawala uliopita
Pole yake, Ila tatizo pia uwezo wake ni mdogo sana.

Sema ukishakuwa Rais ndani ya CCM unakuwa na nguvu zaidi ya mjeruhiwa mbogo , hakuna atakayeleta fyoko 2025 mama akichukua form.
 
Sema ukishakuwa Rais ndani ya CCM unakuwa na nguvu zaidi ya mjeruhiwa mbogo , hakuna atakayeleta fyoko 2025 mama akichukua form.
Exactly....

Wasisahau Mama ana Dola nyuma yake.

Wakikuyu Kenya walimdharau Moi baada ya kuchukua mikoba ya Kenyatta, na alivyokuwa mpole mara ya kwanza wakadhani ni feather weight, alipoanza kuwang'ata hawakuamini.

Usimdharau Simba kisa tu anakuchekea, hili la Mbowe[right or wrong] ni ujumbe kwa wanaomchukulia poa. She can be ruthless wakabaki wanashangaa.
 
Kwa tabia ya huyu Mama hata akionewa kwangu nitaona sawa sawa kama kifo cha Jiwe ilihitaji huruma ila tabia za jiwe hata kama aliondoshwa kimakusudi me niliona poa tu katiri yeyote mimi simthamini nachukulia my enemy of my enemy is my friend... Mama nawewe nenda tu huna cha kutufaa Watanzania
 
Anaongea kwa kuhema! Ahahahah na,yaani hakyamungu CCM kwenye Urais siyo masihara, yaani mama hana ubavu wala mbinu kukabiliana na wataalam wa siasa za ndani na mikakati.

Yaani mbinu iliyoanzishwa na gazeti la Uhuru nimeielewa dah!

Hii nchi ngumu sana..kwa taarifa yake CC yote ya akina Mangula haiko naye hata kidgo! Tena awe makini sana, kama anasoma hii meseji narudia AWE MAKINI SANA MAANA NAMBA ZINAZOELEKEZEWA NA MSHALE KWAKE ZINAHESABIKA!
 
Sema ukishakuwa Rais ndani ya CCM unakuwa na nguvu zaidi ya mjeruhiwa mbogo , hakuna atakayeleta fyoko 2025 mama akichukua form.
Magu pamoja na ubabe wote ila Kuna kundi lilimtikisa, huyu bibi ushungi anavyoonekana hakuna analojua ndio watamtikisa hadi atakimbia mwenyewe. Subiri uone. We unafikiri wapo tayari kusubiri hadi 2030?
 
Back
Top Bottom