Mtego: Hivi serikali ilifikiria nini mpaka kuja na wazo la kukata kodi mafao ya mbunge?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,591
36,004
Nadhani na ndivyo ilivyo kuwa kila mfanyakazi mwenye ajira rasmi analipa PAYE. Hii ni kwa hata wabunge na viongozi wengine.

Lakini ukienda mbali zaidi wabunge huwa wanamalizana na serikali baada ya utumishi wao wa miaka mitano. Hawa hawana pensheni kama rais, waziri mkuu Makamu wa rais majaji na viongozi wengine ambao wanalipwa 80% ya mshahara wa cheo kinacholingana tena kwa muda huo.

Kuna mtego ambao serikali hii isiyo sikivu imeuweka na kama utanasa basi kilio kitakuwa kikubwa sana mwaka ujao wa fedha!

Umejiuliza ni kwa nini kodi inayopendekezwa kukatwa mwaka 2020 iwasilishwe kwenye bunge la bajeti mwaka 2016? Huu ndiyo hasa mtego wenyewe.

Kwamba endapo kama serikali itafanikiwa kufyeka mafao ya mbunge mbali na ile PAYE basi itakuwa imejirahisishia njia ya kufyeka mafao ya kina kabwela na pangu pakavu wengi hapo mwakani. Kuna uwezekano mkubwa kama bunge la mwaka huu litaridhia kujilipua kwa kukubali kukatwa kodi kwenye mafao basi bunge la mwakani litakuwa na kazi rahisi ya kufyeka kodi kwenye mafao ya watumishi wengine ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii e. g NSSF, PSPF na mingine. Hapo ndipo mtego utakuwa umekamilika!

Sasa unajua ni kwa nini walete mwaka huu na siyo mwaka 2019? Hii ni kwa sababu watumishi wengi ni wa mikataba na hawana pensheni hivyo wengi huchukua mafao yao baada ya miaka miwili ya mikataba! Sasa kama watafanikiwa kuanza na wabunge, watakuwa wamejipa uhakika wa kuwapata wengine mwakani na hapo watakuwa wamefaidi mapema kuyakata mafao ya makabwela wengi wanaoishi maofisini kwa mikataba.

Mimi binafsi sihafiki kabisa mbunge kukatwa kodi kwenye mafao kwani haitakomea hapo! Kama serikali itafanikiwa mwaka huu, basi vile visenti vyako unavyopigia hesabu kila siku kule NSSF jiandae kulima asilimia hiyohiyo itakayolimwa kwa mbunge! Usibishe!

Aidha badala ya kuweka mtego huu wa kukata mafao ya wengi wasio na pensheni, ni vyema wakaondoa posho za bunge na kupunguza ile 80% wanayokula kina Kikwete, Mkapa, Bilal na watafunaji wengine wengi ambapo mfano; utakuta Kikwete mbali na kugharamiwa kila kitu na serikali bado anaingiza zaidi ya milioni 15 kila mwezi kama pensheni.

Hii serikali isiyo sikivu inaturudisha wapi?
 
Ni baada ya kubaka democracy ya Mtanzanyika na kuwekewa vikwazo na wafadhili na na serikali ya CCM ilitumia pesa nyingi sana kwenye uchaguzi uliopita sasa bajeti haitoshi inabidi warukeruke kukata kodi na kukata viuno.

swissme
 
hii ni kweli hata mimi nimehisi huu ni mtego..

serikali inayatamani sana mafao ya wafanyakazi ndio wanayapigia denge kwa sarakasi tofaut tofaut mara ppf wamesitisha mara kodi mara nini..

yaani mafao ya mfanyakazi ni full zengwe...

huu mchezo hauhitaji hasira....

mda si mrefu tunachukuliwa mafao yote na serikali
 
Mbona yanakatwa kitambo tu
 
Jamani mambo ya kodi hayatakiwi kuingizwa kwenye malumbano ya kisiasa. Wewe mfanyakazi angalia pay slip yako utaona mafao hukatwa katika gross salary. Ni kawaida na nibutaratibu kuwa kila kipato kinatakiwa kukatwa kodi, mafao ni deductions ya mishahara ilikuwa haijalipiwa kodi. WALIPE KODI HAPO HAMNA SWALA LA SIASA.
 
"Wapinzani tunapendekeza posho zote za wabunge yani seating allowance zifutwe kwakuwa mshahara unatosha kabisa"

:D:D:DHii kauli imewafanya wahuni wa Lumumba wamepanic saana.
 
Anzeni kukataa posho kama Zitto kama huo ujasiri ukawa mnao...
"Wapinzani tunapendekeza posho zote za wabunge yani seating allowance zifutwe kwakuwa mshahara unatosha kabisa"

:D:D:DHii kauli imewafanya wahuni wa Lumumba wamepanic saana.
 
Jamani mambo ya kodi hayatakiwi kuingizwa kwenye malumbano ya kisiasa. Wewe mfanyakazi angalia pay slip yako utaona mafao hukatwa katika gross salary. Ni kawaida na nibutaratibu kuwa kila kipato kinatakiwa kukatwa kodi, mafao ni deductions ya mishahara ilikuwa haijalipiwa kodi. WALIPE KODI HAPO HAMNA SWALA LA SIASA.
Mkuu, hayo makato yapo kwa kila mfanyakazi (kwenye gross) ambako kuna PAYE! Sasa kuna yale makato ya kwenye mafao yanayopendekezwa!
 
Sijaelewa mkuu. Nilichosema hukatwi, unakatwa siku ya mafao.
Yanakatwa mwanzoni unapolipwa mshahara na sio mwishoni unapolipwa hayo mafao. Angali salary slips zako.

Mkuu inakatwa gross pay siyo net pay. Wakikatwa katika net watakuwa wanadaiwa nini tena?
 
Ni baada ya kubaka democracy ya Mtanzanyika na kuwekewa vikwazo na wafadhili na na serikali ya CCM ilitumia pesa nyingi sana kwenye uchaguzi uliopita sasa bajeti haitoshi inabidi warukeruke kukata kodi na kukata viuno.

swissme
Acha kukariri demokrasia demokrasia, lipeni kodi na tunataka na posho ya makalio nayo ikatwe
 
Back
Top Bottom