Mtego aliotegewa Abdul Nondo na "watekaji" wake,hauna tofauti na ule wa Odwang Odwaa mwanafunzi Mganda UDSM

hiyo story yako haiendani na ya huyo dogo,kadogo haka kalikuwa kanatafuta huruma ya kisiasa akajua akienda na mapigo ya sasa ya hali ya kutekanatekana yatampa kiki,na jinsi kalivyo kajinga eti mchana kanaandika nipo kwenye hali mbaya then kanaleft kwene magroup ya whatsapp ,jioni kanatekwa kesho mijusi wenzake wanaita press na kusema mjusi mwenzao ametekwa.

hata siku haijaisha ,taarifa zinasema dogo kaonekana iringa akiwa hajielewi amefikaje,yani ni utoto,utoto,utoto then mijusi mingine huku urainani na hapa jf inakuja na hoja eti apewe nafasi ya kuzungumza as if mtuhumiwa anahaki ya kuzungumza chochote wakati yupo kwenye uchunguzi.

ushauri wa bure,kweli wengi tumechoswa na aina ya serikali tuliyonayo,kuminywa kwa demokrasia hali ya usalama kuwa mbaya nakadhalika,inakuwa jambo la ajabu eti kajitu kamoja huko kasicho na impact yeyote ile katika nchi hii kanazungumza tu etu "mwigulu ajiuzulu kuwajibika kwa kifo cha akwilina " eti ndo atekwe.

pengine mimi sijui zaidi hivi kati ya rais wa daruso na huyo mjusi na kataasaisi chake uchwara nani anaimpacti akitoa tamko?
 
I remember wakati wa yale maandamano kuelekea viwanja vya Jangwani nilikuwa first year. It was hot by then, all in all Odwang was far tougher than hutu tujamaa unatotuzungumzia hapa, usimlinganishe Odwang na hawa madogo
 
hao jamaa waliongoza pia maandamano ya 2008/2009....ule mgomo ulisababishwa chuo kufungwa kama miezi miwili then baada ya hapo Odwang hakuonekana tena...
Ila ninachokumbuka Owawa ndiye alikuwa kinara, Odwang hakuwa muongeaji sana zaidi ya kupaza sauti "Odwaa" pengine alikuwa vizuri kwenye mikakati.

ila cha kusikitisha rev square haipo tena, lile eneo limeota nyasi kabisa!!
Watu wanashangaa Bush kuajiriwa na chuo.

Huyo Ally Hapi wa Kinondoni nae alikuwa mtu wa Rev Square. Ndio ujue mnapofanya maandamano kuna wenzenu wapo kazini.

Hata hayo makundi ya kuhamasisha maandamano kuna watu wapo mbelembele kumbe wapo kazini. Subiri vijana wakamatwe kama kuku.
 
Owawa namkubali sana alinifundisha as temporary teacher o'level somo la civics jamaa yuko vzr sana cjui jamaa saiv yuko wap
 
mh!!Mabibo hii hii ninayoijua?
We nawe, sio mabibo sokoni au uswahilini kwenye mateja, mabibo hostel! Kijana yule binafsi sitamsahau, ilikuwa ukisimama 'kariakoo' unaskia sauti moja ghafla kutokea juuu hall 2 "Odooooooooooooong....." halafu ma hall yote ya karibu hall 3, 1 wanaitikia kwa hamasa kuu "Odwaaaaaaaaaaaa....."!
 
Ha haaaa.....ilikuwa burudani sana wakati wa muganda huyu...mtu anaropoka saa 8 usiku kutokea block D "Odwaaang" halafu mwingine anaitikia block E...ha haa. Kule main campus ilikuwa ni Hall 2 na Hall 5...
Hahahaaa, mi sikuwa mtu wa purukushani ila huyu bwana alivyokuwa maarufu nikataka nimuone yukoje...daaadeki km Idd Amin, mweusiii tiii, nikasema hapa kazi ipo! Ila alijua kukinyoosha chuo na serikali. Watu watafanya fujo, watavunja ila mwisho wa siku Mkandala anakuja kuongea Nkurumah kwa upole, heshima, nidhamu na taadhima! Na changes mnaziona!
 
Aisee naomba nipate matukio mengine ya huyu ODWAAAA!! hahahahah sim jui ila nime furahi kusikia historia yake... UDSM walikua na ujasiri.
Aaaaahhh, Odong alikuwa mtu mwingine aisee! Aliwajaza ujasiri wanafunzi kiasi kwamba mkiamua jambo wooote lenu linakuwa moja! No politics na upuuzi, ukiskia "kunji" ujue hakuna kurudi nyuma! Nakumbuka ffu walikuwa wanawahi kukizingira chuo kila wakiskia kuna kunji lkn watu wanaandamana mbele yao! Na wakirusha mabomu ya machozi, mvua ya mawe inawanyeshea, duh! Hapo hapo wanafunzi wakorofi wanatake advantege ya kunji kulipa visasi kwa ma lecturer wakorofi wakorofi, yalimkuta Karamagi wa bcom, anafundisha huku nje kuna kunji, watu wakavamia, tia mikwaju wasaliti wote mle ndani, Karamagi kuona vile kakusanya vitu vyake na majina ya 'waliohudhuria pindi', waja wakamuona wakamkimbilia, 'sir tupe hiyo 'attendence' uende kwa amani...' jamaa kakataa, kilichompata hapo naona hajasahau mpaka leo, walimfinya, wakamtia makofi mwisho wakamchania kila kitu! Ila na yeye jasiri, alimkamata mmoja akamwambia mi 'ntazaa na wewe tu' ...... hahahaaaa!
 
Damn! Haha noma sana.
 
Hivi kwa sasa hivi au tunakoelekea tutawapata tena wanafunzi kama hawa kweli?
 
Asante sana, kwa historia muhimu kwa vijana wetu. Kama ulivyosema, picha iliungua, kwa maana kamanda Mambosasa anasema polisi ndio waliomkamata kwa mpenzi wake.

Kwa kuwa, Kijana wetu Nondo, atafikishwa mahakamani tutasikia utetezi wake. Uongo unaweza kusafiri haraka na kuifunika nusu ya dunia ndani ya muda mfupi, lakini wakati huo huo ukweli huwa unafunga kamaba za viatu na husafiri kila mahali ambapo uongo ulipita na kukalia kiti cha enzi. Hizo ni za wahenga.
 
Ujinga wa smartphone. Unapotaka ujinga wa namna hii usitumie smartphone. Walifuatilia kwa GPS. La sivyo walishawini.
 
Wakishindwa kukufanyia Discrimination basi watakufanyia Victimization. Hizo ndio retaliations kubwa zinazoweza kumkuta Mwanaharakati yeyote Duniani. Pole Odwaaang, Pole Chuma(Nonddo)
 
mitando inatusaidia sana ,...jana nilisema hapa yule mpenzi ni kachero wa polisi aliyemvuta jamaa hadi Mafinga..ni mbinu za kitoto na utaona mahakamani jinsi Jamuhuri itakavyodhalilishwa
 
Back
Top Bottom