Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Kwanini unashindwa kuelewa kuwa Speaker ndio alikuwa wa kwenda Ikulu na kumuona Rais na kutoa hoja zake

Lakini alipoamua kwenda public hiyo inadhihirika kabisa kulikuwa na bifu kali kati yao
Ila alichosahau Job ni kuwa alikuwa anamnanga CiC hapo ila kwa hasira zake yote hayo aliyasahau

Wote tunajua mbio za miaka mitano huwa zinaanza mapema na tumeshuhudia marais waliopita wakiongelea hilo mara kwa mara kuwa jamani Kipenga bado

Hapo pamoja na yote job ajishushe tu au aachie ni moja kati ya hayo
 
Hii busara ilitakiwa ianze kwa Supika kwenda kumuona Rais na kumpa dokezo kiuongozi, kwenda public na kuhoji huku ukikebehi "nchi itapigwa mnada" zaidi ya hapo unasema wataamua 2025 mkitaka kuweka wa kukopakopa, huku kulikuwa ni kupungukiwa busara kwa hali ya juu.

Na retaliation yake ndio hii watu msije kumuona Rais amekosea kumjibu public kwasababu yeye aliongea public basi naye acha ajibu public ndio waende huko ndani wakamalizane, hauwezi kuharibu image ya mwenzako yeye akae amekuangalia tuu.

Unaelewa maana ya busara na utu uzima dawa? Utu uzima dawa maana yake sio kila lisemwalo hujibu.... samia ni raisi na Amiri kesho sio Sawa yeye kujibu jibu hovyo hii ilikuwa kazi ya mwigulu waziri wa fedha aje na ufafanuzi kwa wananchi inatosha, wao wangeombana msamaha yangeisha na maisha kuendelea hii inampunguzia heshima samia kama raisi!!!! Na mbaya zaidi naye analeta mipasho aise ndugai wenda kakosea lakini sio sahihi raisi kukosea zaidi!!! Ukisikia mtu anaomba Mungu ampe hekima ogopa sana hekima mkuu wangu ukiwa raisi jiandae kukwepa mishale mingi pengine ile ndugai katest lakini wenye nia na Kiti cha uraisi wapo karibu na mama awe makini wanamcheki tu
 
Hiyo siyo nguvu ya sukuma gang huo ni upumbavu wenu wenyewe nguvu ya sukuma gang ipo kwa wananchi na wazalendo waliopo serikalini huyo zuzu ndungai sisi atumtambui hata kidogo ,
Nawashangaa sana hawa wanaotaka kuifanya vita ya Mama na Ndugai iwahusishe pro-JPM. As if kuna kitu chochote alichowahi kukifanya Ndugai kujenga na kulinda heshima ya JPM baada ya kifo chake. Ndugai huyu huyu ndiye alipigia debe ujenzi wa bandari ya Bagamoyo mara baada ya JPM kuondoka. Huyu mtu wala hatumtambui hata kidogo.
 
Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali... CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili.

Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama.

Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia, kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.

Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi.

Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?

Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.

Hekima itatamalaki? Ya nani?
Wenye akili wameliona hili na wameshauri ila ila kuna wakati lazima uwache jambo litokee ili alie lisababisha aone mwenyewe nadhani mtakumbuka mm siamini JPM alikufa kwa sumu au nini ila naamini ubishi na kuona anajuwa kila kitu kuna wakati alijikuta amekosea na amesha toa amri... Hivyo alikufa kwa presha maana binadam anakipimo cha kuimili mambo yani nikama gari ukiibebesha mzigo mnzito unauwa engine same binadam akizidiwa na stress kufa ni sekunde mbili tu.
Musa alikuwa akisikiliza kila kitu kutoka kwa israel Mungu akamtuma ndugu ya amwambie atafute watu wenye hekima miongoni mwa Israel wasikilize mashauri ya watu kwasababu atakufa ikiwa atabeba kila kitu yeye.
Serikali ni watu na sio mtu ukifikiri serikali ni mimi ukaona unaweza fanya lolote basi unapata majibu unayo yataka......
 
Now you are back.
We missed you bro.

Hoja hii makini sana.

Samia ameshatishwa na tetesi zinazoenea kwa kasi hivyo ameona wacha aoneshe makali kidogo..
Mzeemwakijiji mbona yupo ila alokosa hoja baada ya kuhamia Kwa Jiwe Sasa anafurahia anguko la mama!
 
ila mama kakosea,haiwezekani mtu kaomba msamaha wewe bado unamsimanga tu. Ndio haya tunayosema hana uwezo wa kiuongozi
Binafsi Spika amechelewa sana kuomba Radhi, ilipaswa asubuhi yake alivyoona watu wanasambaza habari yake awahi kuita waandishi wa habaru akanushe, wakati huo ameshaenda kwa Rais kuongea nae.
 
Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali... CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili.

Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama.

Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia, kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.

Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi.

Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?

Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.

Hekima itatamalaki? Ya nani?

Ndugu yangu natamani ungeamua kuona mbele zaidi. Tunachopenda wengi ni nchi yetu kuimarika kitaasisi zaidi. Mhesh sana Rais aliepo kitini na Spika ni wadogo tu. Kubwa lao ni Tanzania. Taasisi na mihimili iliyopo zinasimamiwa na watu. Wao sio wakubwa kuliko mihimili/taasisi zile. Akiondolewa mmojawapo au wote wawili Tanzania ipo pale pale na labda ikawezeshwa kwa hilo kusonga mbele zaidi. Maandiko/mabandiko yako tukufu nayakumbuka. Ndani yake limo la kansa ya RUSHWA adui wa haki. Alie msafi na mchafu chamani sio siri!! Tunahitaji watoke. Bila wao bado tutasonga mbele pia. La demokrasia, haki na uhuru wa RAIA je? ya taasisi imara hayo. basi tunahitaji wale ambao wanaweza simama imara bila kupeperushwa na makandokando ya upuuzi kama ulivyo kwenye rekodi za wengi tu waliomo madarakani. Vimeumana sasa, safi sana.
 
Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia, kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.
Umemiss the point. Samia kasema wazi kwamba kasamehe. Alichofanya kwenye maelezo yake ni kuweka wazi kiini cha tatizo ambacho ni Urais. Ilikuwa muhimu taifa zima lijue kwamba kuna hilo tatizo ambalo halimuhusu Spika tu bali vigogo wengine kadhaa wenye mitazamo hasi kuhusu urais wake SSH.
 
Lazma mmoja wapo ang'oke ili utawala uendelee kuwa salama,la sivyo watawindana sana kuelekea 2025 na hqta ufanyaji kazi wao utakua mgumu kuanzia sasa
 
Unaelewa maana ya busara na utu uzima dawa? Utu uzima dawa maana yake sio kila lisemwalo hujibu.... samia ni raisi na Amiri kesho sio Sawa yeye kujibu jibu hovyo hii ilikuwa kazi ya mwigulu waziri wa fedha aje na ufafanuzi kwa wananchi inatosha, wao wangeombana msamaha yangeisha na maisha kuendelea hii inampunguzia heshima samia kama raisi!!!! Na mbaya zaidi naye analeta mipasho aise ndugai wenda kakosea lakini sio sahihi raisi kukosea zaidi!!! Ukisikia mtu anaomba Mungu ampe hekima ogopa sana hekima mkuu wangu ukiwa raisi jiandae kukwepa mishale mingi pengine ile ndugai katest lakini wenye nia na Kiti cha uraisi wapo karibu na mama awe makini wanamcheki tu
Mkuu hili lilikuwa ni shambulio dhidi ya hadhi ya Rais...yes naliita shambulio maana kama angekaa kimya Rais watu wangeamini sababu aliyeongea si mtu mdogo kimadaraka ndio maana nasema busara zinanielekeza kuwa angemuona Rais privately na kama asingesikia basi wangedili kwenye vikao vya ndani katika chama.
 
Ushawahi sikia Samuel Sitta anaomba msamaha kwa mkuu mwenzie wa muhimili! (enzi hizo alikua JK)

Kwa kifupi Job Ndugai kakosea alitakiwa aendelee kuvimba, yeye ni muhimili tofauti, na inashangaza mwanaume gani anakuwa mwepesi mwepesi kuomba msamaha tena kwa she!
Ugali mtamu mkuu
 
nakumbuka Kuna waziri aliambiwa nonsense,kwa kusema kwa nn tununue sukari nje ,na kwetu bado ipo kwenye ghara yakutosha,tunamnufaisha Nani!!??

NAMNUKUU: tukijiamini tunaweza kujitegemea!!!? weeee bi mkubwa alimuwashia Moto balaaa,.
Sasa hii policy ya kujitegemea nadhani inamgogoro na bimkubwa. Ukitaka mkorofishane na bi mkubwa akupe mipasho,njoo na hii policy ya kujitegemea !!! refer na kwa ndugai!!
 
Kwanini unashindwa kuelewa kuwa Speaker ndio alikuwa wa kwenda Ikulu na kumuona Rais na kutoa hoja zake

Lakini alipoamua kwenda public hiyo inadhihirika kabisa kulikuwa na bifu kali kati yao
Ila alichosahau Job ni kuwa alikuwa anamnanga CiC hapo ila kwa hasira zake yote hayo aliyasahau

Wote tunajua mbio za miaka mitano huwa zinaanza mapema na tumeshuhudia marais waliopita wakiongelea hilo mara kwa mara kuwa jamani Kipenga bado

Hapo pamoja na yote job ajishushe tu au aachie ni moja kati ya hayo
Ukiona mtu anayefahamu taratibu zote kafanya jambo kinyume na utaratibu fahamu kwamba nia yake ni kuwa anataka wananchi wafahamu kinachoendelea.

Hapa spika alitaka Raia tuelewe jambo.
 
Ukiona mtu anayefahamu taratibu zote kafanya jambo kinyume na utaratibu fahamu kwamba nia yake ni kuwa anataka wananchi wafahamu kinachoendelea.

Hapa spika alitaka Raia tuelewe jambo.
Inawezekana kabisa kuna kitu hakiko sawa Job ndugai sio mjinga wa kuhatarisha wadhifa wake tunamponda tutakuja kumkumbuka.
 
Ukiona mtu anayefahamu taratibu zote kafanya jambo kinyume na utaratibu fahamu kwamba nia yake ni kuwa anataka wananchi wafahamu kinachoendelea.

Hapa spika alitaka Raia tuelewe jambo.

Ambalo wengi tulikuwa tunalijua
Lakini mbona hakutumia njia ya mtangulizi wake Mr Standards and Speed alipokuwa anawatumia opposition?

Sasa yeye na Cheo kikubwa hivi kuwa against na Boss wake alikuwa hajua anajitega mwenyewe?
 
Naunga mkono hoja kwamba mama kajiweka katika mtego mbaya. Ila ipo wazi yataibuka makundi mawili hatari kwa chama ambayo yatakuwa yanasuguana, kiungozi bi mkubwa ataongoza nchi kwa pressure sana, coz mda mwingi atadeal na makundi ndani ya chama. Vile vile hiyo ni karata kwa vyama vya upinzani, kadri CCM wanavyosuguana na wao watapata mda wa kujipanga haswa hoja ya katiba, kwa sasa tunakoelekea katiba mpya itakuwa inapiganiwa pia na kundi litakalokuwa linasuguana na mama hapo patakuwa patamu, naungana na mtoa hoja bi mkubwa hakupaswa kuchukua maamuzi aliyochukua wangemaliza kichama lkn sio kusema sema hovyo anawapa faida wasiomtakia mema lakini anatengeneza zaidi uadui na watu waliomzunguka ktk chama haswa kundi linalojihisi kuonewa ndani ya chama au linaloona mambo hayaendi sawa
 
Lakini katika mkutadha huohuo Rais SSH akisema Kuna mtu alienda kumpa pole na hongera na akamshari kwamba wabaya wako wapo ndani ya kijani (CCM) na sio Upinzani!

Kwa maneno hayo Ina leta tafsiri gani ,hasa ikishudiwa Mwenyekiti wa CHADEMA akiwa malango ya magereza??

Kwamba amekumbuka kauli hiyo na ameingiwa na majuto kumuweka jera Mbowe bila kosa na nini atafanya kwako???

Ikumbukwe kwamba Kuna watu wamekuwa rais ana shauriwa vibaya na baadhi ya watu wake hasa Hilo la Mbowe inasemwa alidanganywa ili amdhibiti Mbowe na Chama chake then wahuo hao baadaye watamtoa Samia kwenye reli na kuchukua nafasi yake .

Hii inamaana Samia anatumika bila kujua dhamila ya jamaa hao.
 
Back
Top Bottom