Mtazamo wangu : Rais/serikali live imeleta faida kuliko Bunge live

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
1: Wananchi wametatuliwa matatizo yao kwa wakati.

2: Watendaji na macontractors wanaofanya kazi na serikali hawana uhakika wa kudanganya na kukwepa mkono wa serikali muda wote.

3: Wabunge wamepata fursa ya kuwa maarufu majimboni kwao kwa uwepo wao huko sio kupitia vipaza sauti vya vya Bungeni bila kukanyaga jimboni mara kwa mara.

4: Mikutano maalumu yakisekta na Rais live imeleta mwanga na utatuzi wa haraka.

5: Kilele cha Bunge live ni siku ambapo report za kifisadi na za kutikisa serikali zinajadiliwa kwa hisia na hamasa kali lakini hakuna kinachotekelezwa baada ya hapo. Hata maazimio yasipofanyiwa kazi hakuna hatua ya pamoja inachukuliwa. Hii ni tofauti na Rais live.


Nakubali live zote mbili zimekuwa na faida na hasara lakini Rais live imeleta faida zaidi.
 
Back
Top Bottom