Mtazamo Wangu: Kwanini Kicheere ana fursa ya kuwa CAG bora kuliko Assad

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
319
510
Nimetazama CV ndeeeeefu ya Profesa Assad anayemaliza muda wake mwisho nikabaini udhaifu mdogo unaofunika utaalamu wake wote.

Profesa ni kama Maprofesa wengine tu, aliisoma dhana ya finance na audit kwa kina lakini ndio wale wale muda mrefu aliutumia kuchambua nadharia wa wazungu kuhusu audit.

Hakuwahi kutoka hapo na kuishi kama Mkaguzi na kuyaona magumu ya ukaguzi na namna ya kusimamia ukaguzi "practically."

Hii inaweza kukueleza pia tofauti ya CAG Utouh na CAG Prof Assad. Utouh kabla ya kuwa CAG alikuwa "technocrat" Prof. alikuwa "academician."

Nimesoma wasifu wa CAG mteule Kichere nikapata matumaini makubwa kwani alianzia chini zaidi akiwa Mkaguzi mpaka kupanda kuwa Mkaguzi Mkuu.

Ni mtu anayeijua sanaa na sayansi ya ukaguzi si tu kwa kuisoma katika BA na MBA yake tu bali kwa kuifanyia kazi tena katika taasisi kubwa na busy kama Unilever na Tanroads.

Zaidi kanikosha, Kichere akaenda kusoma Sheria (LL.B) kabisa. Hapa ndio kaji-arm vyema; anaijua audit na atakuwa anazijua sheria zinazosimamia audit na mawanda yake. Maana yake nini, anakwepa dhana ya kugombana na watu kwa kutokufahamu sheria. Mungu amsaidie.

Namtakia kila la kheri Prof. katika kurejea kwake kwenye "theory." na natamkia kila la kheri Charles Kichere anaporejea katika "practical."
 
Assad hamna kitu , kazi yake ilikuwa kususbir report ambazo vijana wake hawakupewa rushwa
 
Kacheru atakuwa CAG mtiifu na submissive wa kwanza kutokea.
Tegemea utendaji legelege wa kufurahisha mamlaka kama kulipa fadhila
 
Kacheru atakuwa CAG mtiifu na submissive wa kwanza kutokea.
Tegemea utendaji legelege wa kufurahisha mamlaka kama kulipa fadhila
Labda Kwa sababu "NCHI ILIYOPATA MAENDELEO FEDHA HAINA SAMANI" jamaa anamkwanja Sana atakuwa anadharau report Kwa sababu ni story "FEDHA KUINGIA KWENYE MZUNGUKO"
 
Mimi nadhani hata angekuwa na CV iliyoanzia na ukaguzi wa mahesabu ya kiosk, akaja kukagua duka, halafu supermarket, akaja kukagua mradi, then Idara akapanda hadi wizara na sasa serikali nzima.

Hata kama alisoma ukaguzi wa fedha kuanzia certificate, akaja diploma, halafu bachelor, baada ya hapo masters nakuendelea hadi proffeseri

Hata kama alianza kusoma sheria za ukaguzi kuanzia certificate, akaja diploma, halafu degree nakadhalika

Hata kama masomo yake hayo aliyosomea Havard na akawa best graduate na akapewa special award

Yoooote hayo yatategemea aliyemchagua anataka nini na sio professional yake inataka nini!

Tanzania haiko kama ilivyo kwa sababu haina wasomi au watafiti wazuri, la hasha! Iko kama ilivyo kwasababu mwanasiasa hata kama aliishia darasa la saba ana nguvu ya maamuzi kuliko professor!

Afrika itapiga hatua siku ikaamua kuwaweka wanasiasa ngazi ya pili! Yaani wanasiasa wafuate maelekezo ya wataalamu na sio wao kuwapangia wafanye nini
 
Back
Top Bottom