GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Mtazamo wangu kwa Media Tanzania: Waandishi Makanjanja nao ni Gamba Jingine
Kwa Muongo mmoja sasa naweza kukiri kuwa Tanzania tumepiga hatua kubwa sana katika sekta ya habari kutoka ukiritimba wa RTD na masafa yao ya Kati hadi masafa ya FM na hatimaye sasa kuelkea mfumo mpya wa Kidigitali.
Haitii shaka kuwa huu ni ushindi mkubwa katika sekta ya Habari Nchini ambapo uwekezaji huu uende sambamba na kuajiri waandishi wa Habari walioelimika na kupevuka katika maadili ya Tasnia hiyo.
Katika Kipindi hiki Taifa linahitaji MEDIA kufanya majukumu yake kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu na si mchezo huu wa kuigiza ninaouona katika media zetu, habari moja kila mwandishi anaonyesha ushabiki na mawazo yake bila kujali misingi na miiko ya Taaluma hiyo.
Media inaendeshwa kwa mfumo kama chama cha siasa, unakusanya wapambe ambao hawana hata taaluma wao kazi yao ni kupiga debe ili kuganga njaa, Taifa halihitaji waandishi wapiga Debe. Wanahitajika waandishi wadadisi wa mambo na wenye kuakisi mustkbali na majaaliwa ya Taifa na Utaifa.
Nasukumwa na haya baada ya kusikiliza Hotuba ya Jana ya JK masjid Gadaffi Dodoma, nilitarajia leo kila mwandishi ataibuka na Ushabiki wake na ndio limetokea leo.
MY TAKE:
ADIOS

- Mgogoro ni nini? Owners mnapenda cheap na hamtaki kuajiri professionals au ni njaa iliyokithiri Sekta ya MEDIA Tanzania?
- Hali hii ikifumbiwa macho tunaelekea Kubaya
Owners leteni mabadiliko sasa
ADIOS